Uchaguzi 2020 Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri awataka wanasiasa wanadi Sera badala ya kupambana na Vyombo vya Habari

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,177
Deodatus Balile (Makamu mwenyekiti jukwaa la wahariri): Kumetokea jambo wiki hii ambalo limefanywa na mchungaji Peter Msigwa kwenye mkutano alioufanya wiki hii anawaambia wafuasi wa chama chake cha CHADEMA kwamba waandishi wa habari wamesusia mkutano wake pale Iringa nadhani alikuwa anampokea mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu aliyekuwa ameenda kutafuta wadhamini.

Akawahamasisha wananchi wasuse vyombo vya habari, akawauliza kama wana smartphone, watumie mitandao ya kijamii. Sisi hatuna shida na yale aliyoyazungumza kuhusu uhuru wa vyombo vya habari. Uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kusikilizwa hilo hatuna shida.

Shida tuliyoipata ni pale alipowaambia wafuasi wao kwamba wavisuse vyombo vya habari, wazisuse Tv, wayasuse magazeti.

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amewataka wanasiasa kutopambana na vyombo vya habari badala yake vinadi sera zao. Wakianza hivi kidogo kidoko, tuna historia kipindi cha uchaguzi waandishi kupigwa, kuchomewa nyumba. Tusipotoa kauli kukemea kitendo hiki kiovu ambacho ni jinai mwisho wa siku atahamasisha wafuasi wake wawapie kidogo waandishi wa habari.


Sisi hatupo kwenye siasa, hatufanyi siasa isipokuwa tunaandika ukweli juu ya jambo lilitokea. Inawezekana waandishi wa habari hawakwenda kwenye mkutano wake lakini hakutuambia kama aliwaalika au La, tuwe wazi haiwezekani kama tutakuwa kwenye kila mkutano.

Tunaomba wasitumie uwanja wa siasa kupambana na vyombo vya habari, mwaka 2005 Jangwani waandishi wa TBC walipigwa kutokana na uhamasishaji wa viongozi wa kisiasa, Tarime waandishi walipigwa 2010, mwaka 2000 waandishi Zanzibar walipigwa, hatutaki kupigwa kama wawanahari, kazi yetu si kushiriki siasa.

Tutaripoti mikutano yote kwa mujibu wa ratiba itayokuwa imetolewa na tume ya uchaguzi. tutahakikisha vyombo vya habari tutaratibu. Pia iwapo vyama vya siasa vitakuwa na mikutano vihakikishe vinawasiliana na vyombo vya habari kwa sababu sisi si wanachama wa vyama hivi.

Hatutarajii mwanasiasa aanze kuwazungungumza watu, haitusaidii. Sisi vyombo vya habari tutakuwa tuna-monitor ni nani anaezungumza kututoa katika maadui watatu wa nchi hii. Ujinga maradhi na umaskini na tumejipanga kuripoti sera wanazozisema na nasisitiza hatutaripoti matusi.

Hii inaleta shida sana kwenye live coverage, kuna watu wanashutumu televisheni hazitaki kuwapa live coverage. Matusi hayatatuoa hapa tulipo.
=======

Kwa dalili ninazoanza kuziona sasa nadhani nahitaji Kuzidisha tu 'Dua' kwa Mwenyezi Mungu ili Wazee wa Upanga na Oysterbay wasimezwe Kisiasa.
 
Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile amewataka wanasiasa kutopambana na vyombo vya habari badala yake vinadi sera zao.

Clouds Media

Kwa dalili ninazoanza kuziona sasa nadhani nahitaji Kuzidisha tu 'Dua' kwa Mwenyezi Mungu ili Wazee wa Upanga na Oysterbay wasimezwe Kisiasa.
Hiyo ndo hoja kama .kama mwanasiasia anahisi atendwi haki na media basi anzishe vyombo vyake..ili warushe wanachokitaka
 
Hahaha ashukuru kiboko yake Ruge Mutahaba alifariki, alimyoosha kwenye mgogoro wao na Makonda.
Sasa kesha shiba amevembewa anaanza kutucheulia hovyo hovyo.

Siku zake sio nyingi atatoka hapo alipo ndio atajua uandushi ni nini?!
 
Huyo Balile anajisumbua tu, watu siku hixi hawapotezi hela zao kununua vijarida vya propaganda vya CCM anavyoviita ni. magazeti

Na pia wananchi wengi siku hizi hawana hela ya kuweka bando simu yake kisha alipie ving'amuzi. Siku hizi watu wanatumia vipesa kidogo walivyonavyo kuweka bando kwenye simu zao waangalie dunia inavyokwenda, hawana mpango na mi TV yenu inayoimba propaganda daily!
 
"mchungaji Peter Msigwa kwenye mkutano alioufanya wiki hii anawaambia wafuasi wa chama chake cha CHADEMA kwamba waandishi wa habari wamesusia mkutano wake"
 
Kizazi hiki bado kuna mtu anasoma gazeti?
Idadi yao ni ndogo sana, haina athari kwenye habari za Lussu
JInga kabisa wewe hata hapo ulipo mtaani kwako kuna watu wana vi smartphone lakini hawajui tweeter wala Facebook na jamiiforum, kuna washabiki wa vyama hata kuigia kwenye social network hawana muda alafu wewe unajibaragua hapo.
 
Back
Top Bottom