Makampuni ya ulinzi

Makampuni ya ulinzi

JOESKY

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
823
Reaction score
2,044
Wadau mimi ni mhitimu wa shahada ya kwanza ya ualimu BAED mwaka 2016 nimejaribu kutafuta kazi kwa udi na uvumba lakini mambo bado ya moto.

Nimepost uzi huu ili muweze kunisaidia kujua baadhi ya mambo muhimu kuhusu haya makampuni ya ulinzi na namna wanavyowapata wafanyakazi na mishahara na promotion zao pia. Binafsi nimtokea kuvutiwa sana na kampuni la G4S vipi kwa wale wenye details za kutosha kuhusu hili kampuni linaweza likanipa ajira hata bila ya kupitia mgambo au jkt kisa tu nina vyeti vya elimu ya juu?

Maana niliwahikusikia uvumi kwamba hawa jamaa wao wanaangalia smartness ya mtu kuliko nguvu yaani ni kampuni ambalo linajali zaidi matumizi ya akili ndio maana kampuni mara kadhaa lina wapeleka wafanyakazi wake vyuoni kuongeza elimu hasa masomo ya psychology nk

Ajira serikalini zimekuwa kaa la moto nataka mwaka unaoanza hapo mbele nijikite tu kwenye kutafuta ajira nje ya career yangu hasa huku kwenye makampuni ya ulinzi ya kimataifa.

karibuni kwa mjadala
 
kama ukiamua kwenda kuajiliwa kwenye ayo makampuni...tumia cheti kidogo...kuanzia kidato cha nne kushuka chini...karibu garda...ujaribu ila hapa ni lazima uwe mrefu
 
Kwani nikianzia cheti cha form six au chuo kabisa kuna ubaya wowote?
 
Hawa garda wanapatikana mikoa ipi mkuu?
 
Duu 2016 mbali

Nenda Garda wapo Mikocheni Warioba uko G4S sifa za kuomba kazi zakiduanzi yaani mpaka nani na nani anajua sijui shekhe wa nini ramani ya geto nk

Ila peleka mahombi shule kadhaa kwanza then sikilizia mwaka wa masomo unaisha huu peleka shule ndogondogo then mwezi wa kwanza fanya Followup kuulizia
 
As

asante kwa ushauri wako mkuu. Ngoja nifanye hivyo
 
Kwani nikianzia cheti cha form six au chuo kabisa kuna ubaya wowote?
Hivi sasa kuna vugu vugu la watu wote walio ajiriwa walipwe kulingana na elimu zao hivyo ukiweka vyeti vyako vya elimu ya juu kabisa kwenye hiyo sekta ya ulinzi hutopata ajira kwa sababu hakuna kampuni ya ulinzi itakayokuwa na uwezo wa kukulipa kulingana na vyeti vyako...{ila hizo ni akili za kuambiwa tu changanya na zakwako kila mtu na bahati yake}
 
Nimekupata mkuu asante sana hapo naanza na cheti cha form four na six tu basiii kama ipo ipo tu hakuna haja ya kuwa mwoga
 
Achana na six....weka cha form four...
wenzako huwa bahati zinawakuta wakisha pangiwa kazi...unaweza ukapelekwa kufungua geti au kulinda sehemu ambayo inaendana na elimu yako...huko sasa unaweza kuweka cv yako ukiambatanisha navyeti vyako...ila kwa kuanzia kwenye kampuni za ulinzi tumia cheti kidogo...ikiwezekana kama unacho cha lasaba kitumie
 
achana na six....weka cha form four...
wenzako huwa bahati zinawakuta wakisha pangiwa kazi...unaweza ukapelekwa kufungua geti au kulinda sehemu ambayo inaendana na elimu yako...huko sasa unaweza kuweka cv yako ukiambatanisha navyeti vyako...ila kwa kuanzia kwenye kampuni za ulinzi tumia cheti kidogo...ikiwezekana kama unacho cha lasaba kitumie
Mkuu madini haya ulionipa hakika nimeyaelewa sana nitayafanyia kazi mkuu nashukuru sana kwa ushauri huu.
 
Kwa mwanza wapo pembeni ya rockbeach Yani kile kibarabara cha kamanga ferry
Nipo Dodoma hapa mkuu ila sijajua kama na hapa wapo au vipi maana hao G4s wao wapo Dar Mwanza Arusha na Mbeya nafikiri mikoa mingine hakuna
 
Nipo dodoma hapa mkuu ila sijajua kama na hapa wapo au vipi maana hao G4s wao wapo dar mwanza arusha na mbeya nafikiri mikoa mingine hakuna
Kuna ajira hizi apa za ualimu shule private
 
Back
Top Bottom