Makampuni ya simu ni wezi sana

Makampuni ya simu ni wezi sana

sawa braza endelea kupunguza hasira ila washalipia VAT na kila kitu kwenye huo muamala, watafte na wa VAT nao wambie wamekuibia. mistake haiwezi kuwa error japo error ni mistake.
usiponielewa hapo ndio basi tena.

We jamaa una exposure ndogo sana. Hivi unelewa kuwa hata miamala tu ukikosea hurudisha pamoja na hizo VAT zako unazoona kuwa ni kikwazo.

Mtoa mada amewapa challenge, wao ndo wanamaintain account zote eg tigo pesa na muda wa hewani. Vp washindwe ku reverse huo muamala? Hapo ndipo hoja ilipo.
 
Karibu makampuni mengi yanayofanya mobile money ukikosea muamala imekula kwako ,nilishawahi kununua kifurushi cha azam mara mbili kwa kukosea kuingiza pwd kwenye tigopesa app kumbe ikakata 35 ya kwanza ikaja ikakata mara ya pili ,nikawapigia tigo wakasema imeshaenda Azam niwapigie wao ,nikanyanyua simu nikawapigia azam wakasema hawawezi kurudisha kwasababu salio halijazidi laki kwahiyo hicho kifurushi kitatumika miezi miwili,daa nikachoka hoi.

Siku nyingine Pia nilitaka kulipia maji kumbe nikajisahau nikanunua umeme daaa kurudisha haiwezekani ikabidi nilipie maji kwa kuongeza salio jingine, TCRA inabidi wawaambie hawa makampuni kuwe na window atleast 30mins kama umekosea uweze ku-rollback.
 
Haiwezekani eti mtu umenunua salio kwa tigopesa ukakosea badala ya 2500 ukaweka 250000 alafu wakakukata salio la laki mbili na nusu.

Alafu eti unawapigia wanakuambia eti haiwezekani kurudisha hela yako
Duuh
Hapo utakuwa umenunua kifurushi cha siku 3 au 7 kwa 250k🥱
Waambie angalau waongeze muda wake uwe mwaka, kabla haija expire kesho kutwa.
Uwezo wa kukupa angalau long term bundle wanao.
Itabidi uende ofisini kwao physically, kwa simu tu hamtaelewana
 
Back
Top Bottom