101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,057
- 2,257
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka Walimu Mkoani humo kutumia fursa ya kutafuta mikopo kutoka Taasisi rasmi za kifedha ikiwemo benki ili kuachana na mikopo yenye masharti magumu maarufu kama kausha damu kutoka Taasisi zisizo rasmi za kifedha.
RC Sendiga ametoa wito huo wakati akifungua warsha ya MWALIMU SPESHO iliyohusisha Walimu zaidi ya 200 wa Shule za Msingi na Sekondari kwa lengo la kuwawezesha na kuwainua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa za mikopo kwa ajili ya biashara, kilimo na ada iliyoandaliwa na Benki ya NMB .
"Ndugu zangu Walimu mikopo rasmi inapatikana kwenye Taasisi za fedha rasmi tuache tabia ya kwenda kukopakopa mikopo ya kausha damu, eneo kubwa ambalo limeadhirika na mikopo hii ni Kada ya Elimu na Afya, Watu wanaweka bondi kadi zao za benki, tuache haya mambo yanatufedhehesha na kufedhehesha taaluma"
Mwalimu mmoja aliyeshiriki kongamano hilo ameiambia @ayotv_ kuwa wanakopa kausha damu kwakuwa kipato chao hakikidhi mahitaji “Unakuta Mtu ameshakopa benki lakini bado mkopo haujakidhi mahitaji"
Kwa upande wake Meneja wa Kitengo cha Wateja Maalum kutoka Benki ya NMB Queen Kinyamagoha amesema lengo la Kongamano hilo ni kutambua umuhimu wa Walimu na kujadili fursa mbalimbali pamoja na kuwapatia elimu ya fedha, huku wakiahidi kuendelea kuja na masuluhisho bora kwa Watanzania.