elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philipo Mpango leo amepokea gawio na ziada nyingine kwa Makampuni 58 ambayo yalikuwa hayajatoa gawio kwa serikali ambapo Rais Magufuli alitoa siku sitini (60) wawe wametoa gawio.
Pia Waziri Mpango ameagiza Makampuni na taasisi ambazo bado hazijatoa gawio la serikali ifikapo January 23 mwakani bodi na Wakurugenzi wa Kampuni na taasisi hizo ambazo zitakuwa hazijatoa gawio bado na Wakurugenzi watakiwa wamejifuta wenyewe.
Akizungumza wakati wa gawio hilo leo Jijini Dodoma, Waziri Mpango amesema tayari mpaka sasa makampuni 58 yametoa gawio la jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 12.12, ambazo awali hazikutoa gawio hilo.
"Kiukweli siku ya leo ninafuraha Sana kwa sababu, kutoa gawio ndio kunafanya nchi iweze kujitegemea, na Leo nimepokea gawio kwa makampuni 11 lakini kiujumla makampuni ambayo yameleta gawio ambao Awali hawakuleta ni 58, ambao jumla wametoa Bilioni 12.12" amesema Dkt Mpango.
Aidha ameyataka makampuni na taasisi zote ambazo serikali imewekeza na bado hawajatoa gawio la Serikali hadi ifikapo January 23 mwakani wawe wametoa na ambao watakuwa bado bodi zake na Wakurugenzi wake watakuwa wamejiondoa rasmi kwenye nafasi zao.
Amesema serikali imewekeza katika makampuni hayo ili ipate faida na lengo likiwa ni kuondoa utegemezi wa serikali kwa Mataifa ya nje ambayo yamekuwa yakiweka masharti magumu lakini njia pekee ni kuwekeza katika makampuni na taasisi ili kuweza kujitegemea na sio kutegemea misaada ya nje.
"Sio vizuri kuona Waziri wenu kila siku naenda kukinga bakuli huko nje, huko nje niende kukopa na ninapokopa niwe na uhakika wa kulipa madeni hayo lakini Kama tutakuwa hatutoi magawio kwa serikali tutaendelea kwenda kuomba misaada nje ya nchi" amesema.
Amewahakikishia watanzania kuwa fedha hizo zitatumika vizuri ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi na miradi hiyo mnayoiona sio hiyo tu serikali italeta miradi mikubwa zaidi ili kuleta tija kwa watanzania.
Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka, amesema awali ni Makampuni 79 tu ndio waliotoa gawio kwa serikali, na baada ya maagizo ya Rais Kuna makampuni yamekuwa yakitoa gawio na mpaka Leo makampuni na taasisi hizo zinafikia 58, na kutoa jumla ya shilingi bilioni 12.12.