Utaratibu wa kuvipa majina Viwanja ama mitaa huwa mikononi mwa Wananchi kupitia Mamlaka husika ili kuhuisha majina hayo katika matumizi rasmi kesheria na kitaratibu. Na wasiwasi kama mfumo huu utaendelea kwa "kupoka" majina ya maeneo na kuwapa "first time" Wanasiasa tena wasio na "legacy" yoyote. Hizi ni fujo na ni sawa na "uhaini" wa kimapinduzi hasa katika nchi huru, ya kizalendo na yenye Mamlaka kamili kama Tanzania.
Wafuasi ama Wanachama wa vyama vya siasa ni wachache sana kuliko Wananchi ama Wapiga kura. Hivi inakuwaje uchache huu, tena wa kikundi cha watu wenye itikadi moja kuiamulia jamii. Hii ndio demokrasia tunayoitaka? Je! TLP Jogoo, kesho wakiuita uwanja huo kama Augostino Lyatonga Mrema mtasemaje?
Acheni kuwachanganya wananchi kwa "mihemko" ya kisiasa, pia zingatieni taratibu.