Makamba: Wabunge tumejitoa sadaka kukatwa kodi, wananchi jitoeni sadaka pia msimsubirie Rais

Mbona mimi nalipa kodi miaka mingi tu kumbe huwa najitoa mhanga bila kujua, asante Makamba kwa kunifumbua macho.
 
Hivi hii nchi kumbe kuna watu wao wakilipa kodi ni sadaka na wengine kulipa kodi ni wajibu wao.
 
Hiv ushahid wa hawa watu kukatwa kod unapitikana wap kuturidhisha ma Thomaso
 
Hıvı mfano raıa ukıkımbıa nchı yako kwa maısha magumu pıa utaıtwa mkımbızı au mhamıajı?maana me najua mkımbızı huwa nı vıta tu!naomba kueleshwa nıjue nı nchı ıpı nzurı kwenda kuıshı
 
Nimesikia hiyo statement nikamdharau sana January, kwamba kulipa kodi ni kujitoa sadaka!!? Sisi wananchi tumekuwa tukilipa kodi bila msamaha wowote, huku wao wakipata kipato kikubwa kwa kupiga porojo. Leo akisema wamejitoa sadaka kila mtu anabaki kinywa wazi. Anaweza kutuambia ni jambo gani la maana amelifanyia taifa hili mpaka apatiwe msamaha wa kodi? Ni jambo gani la ubunifu kafanya mpaka awe mtu maalumu wa kutokulipa kodi hivyo siku akilipa igeuke kuwa sadaka?
 
Rais chonde chonde tunakuomba sana uzifute na posho zote za Wabunge,walipwe mshahara tu unawatosha. Mbona watumishi wengi wa serikali hawalipwi posho wawapo kazini? Bungeni ni mahali pao pa kazi kwanini walipwe posho? Kwani wapo kwenye semina pale?
 
1. Kulipa kodi ni kutimiza wajibu, sio kujitoa sadaka.

2. Wabunge wa CCM walikataa kukatwa kodi kiasi baadhi mf Kangi Lugora wakatoa kauli za mkwara kwa Waziri wa fedha, naye akawa anachekacheka.

3. Halafu wakasema kuwa hawakubali kukatwa kodi, kwamba mbona rais, makamu, waziri mkuu, wakuu wa mikoa na wilaya hawakatwi?

4. Uamuzi bora wa rais kusema kuwa kuanzia sasa rais, makamu, waziri mkuu, wakuu wa mikoa na wilaya wanaanza kukatwa kodi ndio umewafanya wapiga mkwara hao kuufyata.
 
Mfumo mbovu wa kuchagua watoto wa viongozi walipita ndio unazalisha watu wenye uwezo mdogo kuwa katika balaza la mawaziri na mawazo yao finyu....
 
Yaani kutimiza wajibu na kutiii sheria ya kodi, unasema kujitoa sadaka??? Wewe ni kiongozi unatakiwa kuongoza kwa mifano!! Acha kujisahau namna hiyo, wananchi sisi tunalipa kodi kila uchao.
 
Back
Top Bottom