Makamba: Wabunge tumejitoa sadaka kukatwa kodi, wananchi jitoeni sadaka pia msimsubirie Rais

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira January Makamba amesema mabadiliko ya kweli yanaletwa na uthubutu wa kweli, na uthubutu huo umeanza mwaka huu.

Ameongezea maendeleo yanahitaji kujitoa sadaka na wao wamejitoa sadaka kwa kuamua kukubali kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo na kutaka wananchi wajitoe hivyo hivyo ili nchi ifanikiwe na sio kusubiria rais atawafanyia nini.

Unajua wakati mwingine uwa najifunza namna binadamu tulivyo wabinafsi kupitia matukio kama haya. Kwa muda mrefu kwa mfano, wafanyakazi wamekuwa wakilia juu ya kodi kubwa wanayokatwa kwenye mishahara yao.

Hawa wabunge walikuwa wanaona ni kama kawaida. Baada ya kuambiwa nao watakatwa kodi wakafura utadhani kifaru.

Kibaya zaidi, kauli nyepesi kama hizi zinatolewa na wabunge hawa. Ati wamejitoa muanga kwa lipi? wanapokea mamilioni ya hela hata kama wangekatwa asilimia 50 bado wangebakia na fedha nyingi.

Ni aibu kwa kweli kusema kuwa ati kukatwa kwao kodi wamejitoa mhanga.
 
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira January Makamba amesema mabadiliko ya kweli yanaletwa na uthubutu wa kweli, na uthubutu huo umeanza mwaka huu.

Ameongezea maendeleo yanahitaji kujitoa sadaka na wao wamejitoa sadaka kwa kuamua kukubali kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo na kutaka wananchi wajitoe hivyo hivyo ili nchi ifanikiwe na sio kusubiria rais atawafanyia nini.

Huu ni ulimbukeni! Kulipa kodi ni wajibu na sio kujitoa sadaka!!! Tena utakuta wakati sheria hiyo ya fedha/kodi ilipokuwa ikijadiliwa waliipitisha haraka haraka wakijua kuwa wao haiwahusu, sasa wameondolewa exemption wanaanza kulia eti kuwa wamekubali kujitoa sadaka!!! Kumbe mkuki kwa nguruwe mtamu ila kwa binadamu ........!!!!!!!
 
JM anaropoka nae kaugonjwa kamempata nini? Sadaka kulipa kodi ambayo mlikuwa mnaiba serikali na walipa kodi? Sadaka ya aje hapo sasa?? Bado posho za kitako....nazo zitolewe hazina sababu kuwepo!!
 
Posho ya Vikao Bungeni ni wizi wa mchana mchana. Mtu anakuwa eneo lake la kazi analipwa kwa kazi anayoifanya kisha anapewa na posho kwa kazi ile ile ambayo amelipwa mshahara kuifanya!!! Wizi!!! Narudia tena, ni WIZIIIIIIIII.

Wafanyakazi wengine pia wakidai posho itakuwaje??? Mh. Rais futa hii kitu inaitwa POSHO maana ndiyo inaonekana kuwavutia watu kuingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge hadi tunapata wenye kutaka Ijengwe sanamu yako (teh teh teh) eti kwa kupiga Push Up!!!

Hima hima Mh. Rais, ukifuta hii posho utakuwa umelikomboa taifa na wizi wa mchana kweupeeeeeeeee
 
Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira January Makamba amesema mabadiliko ya kweli yanaletwa na uthubutu wa kweli, na uthubutu huo umeanza mwaka huu.

Ameongezea maendeleo yanahitaji kujitoa sadaka na wao wamejitoa sadaka kwa kuamua kukubali kukatwa kodi kwenye kiinua mgongo na kutaka wananchi wajitoe hivyo hivyo ili nchi ifanikiwe na sio kusubiria rais atawafanyia nini.

Kama kujitoa sadaka sisi tayari siku nyingi maana miaka yote tulikuwa tunalipa kodi,hasitake kumfundisha mtoto wa samaki kuogelea
 
kujitoa mhanga ni wafanyakazi ambao hata mshahara unalimwa kodi sio wao ambao wanasuburi viunua mgongo baada ya miaka mitano.
 
JM anaropoka nae kaugonjwa kamempata nini? Sadaka kulipa kodi ambayo mlikuwa mnaiba serikali na walipa kodi? Sadaka ya aje hapo sasa?? Bado posho za kitako....nazo zitolewe hazina sababu kuwepo!!
Haswaaaa! Mbunge anafanya kazi za kibunge, na awapo bungeni hastahili kulipwa malipo ya ziada. Naweza kukubali walipwe perdiem kwa kuwa wengi wao husafiri ili kuja vikaoni...lakini hilo la posho mtu anapokaa kufany kazi yake ni double-payment. Na kwa jinsi walivyokuwa wakali kuambiwa watakatwa kodi kwenye mafao yao, sijui kama kutakalika wakiambiwa vikao vya bunge havitakuwa na sitting allowance.
 
Mkuu unajua kuwa huyu jamaa ndiye aliyesimamia katika kupitisha cyber crime so hilo neno lako uliloandika hauhisi kuwa utakuwa hatiani kwa hii sheria?
Sijawahi kumchukia jamaa kama alivyiopitisha hii sheria tumekuwa limited kwenye baadhi ya mambo kwa kweli.
Mkuu Mimi naongelea upuuzi anaotuambia eti kulipa kodi ni ku-sacrifice. Does that make sense? Kama siyo kujiona wao viongozi na wabunge kilikuwa kizazi kiteule ambacho hakiwezi kulipa kodi. Kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi. Mtu mwenye uelewa na nafasi aliyo nayo hawezi kuja na upuuzi kama huo eti "Wabunge tume-sacrifice hivyo na wananchi wafanye hivyo". Hata hajui kuwa sisi wananchi tumekuwa tukilipa kodi tokea siku nyingi.
 
Kumbe wabunge walikuwa wanawakamua wengine wao kimya. Kumbe nchi hui ilikuwa na wenye meno.
 
Back
Top Bottom