Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Hawa wahandisi wa mradi wa JNHPP wanamdanganya sana huyu waziri January Makamba kwa sababu yeye mambo ya sayansi ni mashikolo mageni. Eti tani 26 ni uzito mkubwa sana unaohitaji a special immobile crane kuunyanyua!
Mhuuuuu! Kweli? Kwa nini hawa wahandisi wanamfanyia hivyo Makamba? Mbona tani 26 au zaidi ndizo tunazoziona zimebebwa na malori ya semi trailer manarabarani mwetu. Mbona hayo mamia ya makontena yanayoshushwa na kupandishwa kila siku kwenye meli katika bandari zetu yanazidi hizo tani 26?
Nini hasa tatizo? Kwa nini wasikodi moja ya cranes zilizoko kwenye bandari zetu ili bwawa la JNHPP lianze kujazwa maji katika msimu huu wa mvua kama ilivyokuwa imepangwa? Makamba usikubali kuchezewa na hao wahandisi. Wananchi hawatakuelewa. Hizo kazi ili ziendelee zinahitaji ukali na si diplomasia.
Tusipojaza maji bwawa hilo msimu huu wa mvua ina maana itabidi tusubiri hadi msimu wa mwaka 2023/24 kujaza bwawa hilo. Maana yake hadi 2025 hatutakuwa na umeme wa JNHPP ambao ungalishusha bei ya unit moja ya umeme kutoka sh 350/ hadi sh 30/ kama ilivyo kwenye nchi zilizoendelea kama China na Ulaya.
Viwanda vyetu vingaliweza kuzalisha bidhaa zenye bei inayoweza kushindana kwenye masoko ya kimataifa. Hili kama halitafanikiwa tutegemee umeme kupanda bei maradufu, kukatika mara kwa mara na mgawo wa umeme na maji kama ilivyokuwa enzi zile za Richmond. Hili litaufanya ushindi kwenye uchaguzi mkuu kuwa ngumu sana kwa chama chenu.