Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Biteko: Kama watu hawapati umeme na nishati, hata tukivaa suti hatuna maana

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727
NWM na Waziri wa Nishati DK Doto Biteko amewataka Wafanyakazi wa Tanesco kudhalilisha umeme na Nishati zingine unapatikana.

---
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kazi iliyo mbele yake ni kuhakikisha huduma ya nishati inawafikia wananchi wote na kwamba pamoja na kazi nzuri iliyofanyika ya kuimarisha sekta ya nishati, bado kuna nafasi ya kufanya ili nishati ya uhakika ipatikane.

“Kama watu hawapati umeme, kama watu hawapati nishati wanayoihitaji, hata tukivaa suti za namna gani tunakuwa hatuna maana na tutakuwa tunasemwa kila siku, kiu yangu ni kuona tunafanya kazi kwa viwango ili huduma ya nishati iwafikie wananchi wote,” alisema Dk Biteko.

Dk Biteko alisema hayo jana Jumatatu, Septemba 4, 2023 baada ya kupokewa rasmi na menejimenti na watumishi wa Wizara ya Nishati katika Ofisi za wizara hiyo zilizopo jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan kushika nyadhifa hizo.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza aliyekuwa Waziri wa Nishati, January Makamba (ambaye sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje) kwa juhudi alizofanya kuendeleza sekta hiyo na kuahidi utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati ili nchi kuwa na nishati ya uhakika.

Pia, Dk Biteko aliongozana na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ambaye naye ameteuliwa na kuapishwa kuchukua nafasi ya Stephen Byabato aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje akishughulikia masuala ya Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba aliwapongeza Dk Biteko na Judith kwa kuteuliwa kwao na kuwakaribisha viongozi hao katika Wizara ya Nishati na kueleza wafanyakazi watatoa ushirikiano kwa viongozi hao ili kuweza kutekeleza majukumu yao kazi kwa ufanisi mkubwa.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Mda ni Mwalimu mzuri Wacha tuendelee kula popcorn.Kwa Hali hii hakika hamna maana

View: https://twitter.com/MwananchiNews/status/1699021741018767366?t=aceIxaiN2_wCNaDuK1Jhgw&s=19
 
Back
Top Bottom