Mods plz, hawa members walijiunga kwa mizuka ya uchaguzi watatuharibia jukwaa muda si mrefu, hii lugha wanayotumia mbona kama wametumwa vile ili kijiwe hiki kionekane cha wahuni?
Halafu tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo sisi tilipojiunga angalau unachukua muda kusoma kanuni na taratibu za JF ambazo zinakataza lugha kama hizi, hawa wenzetu wao nafikiri wanakurupuka. Tafadhali jamani bado tunaipenda JF.
By the way hata mimi sim fagilii Makamba lakini siwezi kumtukana kihivyo kwakuwa na ni binadamu.