Makamba na Bei za Mitandao ya Simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba na Bei za Mitandao ya Simu

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Milindi, May 7, 2012.

 1. M

  Milindi JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,212
  Likes Received: 373
  Trophy Points: 180
  Makamba

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, January Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema moja ya mambo ya kufanya katika wizara hiyo ni kuitazama upya gharama za mitandao ya simu, mitandao kutofika maeneo ya vijijini pamoja na huduma hiyo kuwa bora zaidi.

  “Wizara hii inagusa maisha ya kila siku ya Mtanzania hivyo kuna ulazima wa kutizama gharama za mitandao ya simu ili iendane na maisha halisi ya mtanzania” alisema Makamba.

  Akizungumzia masuala ya sayansi, Makamba alisema kuwa kuna ulazima wa kutizama upya msingi wa elimu ya sayansi kuanzia shule ya msingi kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi, lengo likiwa ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaosoma somo hilo.

  Pia, aligusia mikakati iliyowekwa awali ya asilimia moja ya pato la taifa kuingizwa katika ufanyaji wa tafiti mbalimbali na kwamba umefikia wakati wa suala hilo kuanza kutekelezwa kikamilifu.

  “Tunatakiwa kuondoa urasimu wa matumizi ya teknolojia, hakuna haja ya watumishi wa Serikali na wananchi kupanga foleni kwa ajili ya kuchukua fomu, huu ni wakati wa fomu kujazwa katika mitandao tu,” alisema Makamba.

  Hata hivyo, Makamba alisema kuwa mambo mengi anayoyaona na kuyazungumza hata bungeni yameshaanza kufanyiwa kazi na wizara hiyo.

  Source:Mwananchi.


  Ushauri:Mh.Makamba kama unataka mitandao bei ishuke na kuenea vijijini ni kuiokoa TTCL Mobile ili ienee mpaka vijijini na bei itashuka.

  Nakutakia kila la kheri na tembelea TTCL na ulizia kwa nini TTCL Mobile haijaenea Tanzania.
   
 2. Parata

  Parata JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 3,119
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mmmh ni upepo tu utapita ccm wapuuuzi wote
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,736
  Trophy Points: 280
  Makamba ni waziri ama ni naibu/ mbona anapata sana coverage? waziri wake ni nani?
   
 4. mpingauonevu

  mpingauonevu JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 617
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Hata mimi nashangaa sana. Kwanza manaibu hawaingii kwenye vikao. Hawana say yoyote na wizara. Leo anaongea kama vile yeye ndiye mtopu na coverage yake ni siasa tupu! Leo campuni yao ya simu (Rostam & makamba family) vodaphone wameshusha bei zao nadhani dada yake mwamvita makamba amesaidia ili ionekane kaka yake ameanza kuchapa kazi!
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hivi conflict of interest ikoje kati ya January na Mwamvita kuwa katika sekta moja?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,736
  Trophy Points: 280
  wewe unauliza swali gani? mtu na dada yake unafikiri kuna interest gani hapo? kuna maswali mengine sio ya kuuliza
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,511
  Trophy Points: 280
  hakuna conflict yoyote of interest. Lady Makamba ni muajiriwa tuu vodocom sio owner na sio top managenent hivyo sio decision maker, role yake ni advisory tuu so do Mhe. Makamba yeye ni deputy tuu the powers lies with the minister!.

  Kitu anachoweza kufanya ni just to influence decisions ambazo dada yake hawezi ku benefit kwa sababu she is not the owner!.
   
 8. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu ile email aliyoombea pesa kwa ajili ya kampeni za kaka yake? Halafu usimpambe huyo sio Lady bana
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,423
  Likes Received: 19,736
  Trophy Points: 280
  mbona january ana maneno mengi sana au kuna watu wanampaisha ..hadi mimi nilifikiri kuwa ni waziri ama watu ndio wanampaisha na kwa nini?
   
 10. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,718
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  hivi pale mnaposema ladies and getlemen huwa mnamaanisha nini????

  i thought ladies ni plural na lady ni singular!!!!!!

  swali...kama Mwamvita si Lady basi ni nani? Gentleman au? au ndiyo nyie mmekariri maana moja tu ya neno???

  swali...na wale walimu wenu waliowafundisha asubuhi muwaamkie Goodmorning Sir!!! unasemaje hapo????
   
 11. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,718
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Makamba hana jipya wala hawezi kuwa na jipya...kashindwa babaake, babu yake, etc. anachoongea ni porojo za kusherehekea ulaji, kama hivyo waliahidi maisha bora lakini wapi...walikuta sukari Sh 700 kilo na sasa ni sh. 2200-2500.

  CCM haina dira wala muelekeo(Kolimba alisema back in 1995)....hawana dira katika maisha ya watu ya kila siku, hawawezi kuwa na dira katika vitu ambavyo wenyewe wanaviona ni anasa.

  walishindwa na kampuni ya umma TTCL wataweza hizi za mabepari akina Rostam...maweeee!!!!
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mdau umenena!
   
 13. W

  WILSON MWIJAGE JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 276
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndugu,

  Inawezekana kabisa
   
 14. rfjt

  rfjt Senior Member

  #14
  May 7, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Makamba! Natumai hata kupokea ripoti za shule hasa za sekondari kwa njia ya S.L.P utapotea polepole kadri teknolojia inavyozidi kupanuka...unasumbuka mpaka ofisi ya posta kufuata barua moja iliyofika tangu mwezi uliopita...!!! Gharama tu ya kufika posta ingeweza kununua bundle ya kufungua intaneti kusoma barua na kuijibu.

  Tunashukuru kutuma ada/pesa siku hizi si tatizo tena.

  Kila la kheri J Makamba. Tunataka Watazania wenye mtazamo mpya kama huo. From there we want to see things happening.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Magamba wote huwa wanaanza hivi hivi kwa maneno na mbwembwe nyingi sana! mmesahau jinsi Kikwete alivyoanza kibarua chake back in 2005? alikuwa na mbwembwe ambazo hata Obama hakuwa nazo.
  Alitembelea masoko mjinga akiwapa ahadi nyingi za maboresho, alikwenda mawizarani na mahospitalini, mbwembwe, mbwembwe mbwembwe tuuuu hamna lolote.
  ukiwa ccm huwezi kufikiri zaidi ya ccm wenyewe. Namuonea huruma makamba. Kakaa ikulu anaelewa wapi nchi hii inakwamia, na sasa kaingia mtego, amekwisha maana kaingizwa chini ya uvungu
   
 16. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,476
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  Angetuambia na muda wa kulitekeleza hilo, ghrama za mawasiliano ni kubwa mno ukilinganisha na mataifa mengine.
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  May 7, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  TOFAUTISHA SALAMU NA CHEO/NAFASI KATIKA JAMII ......LADY THATCHER NI CHEO/NAFASI KATIKA JAMII LAKINI GOODMORNING LADY NI SALAMU........JAMAA KAMWITA LADY MAKAMBA.

  The word lady is a polite term for a woman, specifically the female equivalent to, or spouse of, a lord or gentleman, and in many contexts a term for any adult woman. Once relating specifically to women of high social class or status, over the last 300 years it has spread to embrace all adult women, though in some contexts may still be used to evoke a concept of "lady-like" standards of behaviour
   
 18. Petiro

  Petiro JF-Expert Member

  #18
  May 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu gamba kweli anafikiria kwa masaburi anafikiri hizo BTS,running power na running cost zinatolewa bure na Nape.
  Hizo BTS zitaendeshwa na umeme upi huko vijijini? Miundo mbinu mibovu? Fanya kwanza utafiti ujue nini changamoto zao ndio uweze kucomments na siyo kusema hovyo
   
 19. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #19
  May 7, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As long as hizi biashara si za serikali ni za private na market ndio inadetermine price, i think the rest will be political initiatives.
   
 20. H

  Hkeen Member

  #20
  May 7, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ok! Tunataka maendeleo ya sayansi na teknohama, changamoto ni kwa hao nafasi zao za kazi zinachukuliwa na mashine, serikali inachukua hatuwa zipi za kuwafeed hao ambao ni jobles watarajiwa ikiwa wasasa imewashinda? Au ni jeshi na ualimu ndio inajivunia.
   
Loading...