KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,737
- 86
Makamba: Msinihukumu kwa mabaya, I love you
2007-11-06 08:33:34
Na Beatrice Bandawe, Dodoma
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, (pichani kulia) juzi alilazimika kuwaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kura kwa kutomhukumu kwa mabaya yake na kuwaambia: `Ilove you`.
Bw. Makamba ambaye mara baada ya kuwaambia wajumbe hao `I love you` (nawapenda), waliripuka kwa mayowe ya vicheko, alisema kuwa binadamu yuko mara tatu.
Alifafanua kwamba upande wa kwanza wa binadamu ni vile anavyojifahamu mwenyewe, anavyofahamika na wenzake na anavyofamika na Mungu.
Alisema kwa jinsi anavyojifahamu yeye, anafaa kuchaguliwa katika uchaguzi huo.
Bw. Makamba ambaye aligombea kundi la viti 20 la NEC Taifa, hata hivyo, alichaguliwa kwa ushindi mnono.
`Chonde chonde wajumbe nichagueni I Love you,` alisema kwa kuweka msisitizo.
Aliwataka wanachama hao kutomhukumu kwa mabaya yake kwani hata Mungu aliwasamehe waliomkosea.
`Nawaombeni mninusuru na chama chetu,` alisema na kuongeza kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu aliochaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, amepambana na kuwagaragaza wapinzani.
Alisema kama wajumbe watamuangusha, hata wapinzani watafurahi na kusema CCM wameangusha Katibu Mkuu wao.
Aidha, alisema vyombo vya habari pia vitapata ya kuandika na kuweka kwenye vichwa vya habari kwamba Makamba agaragazwa na wana-CCM wenzake.
Bw. Makamba ambaye alikuwa akitoa kauli hiyo wakati aliposimama kwenye jukwaa la kuombea kura, mara baada ya kumaliza kujinadi, Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, alimjibu kwa kumwambia: `We love you too,` na kusababisha ukumbi mzima kushangilia.
SOURCE: Nipashe