VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Katika kile kinachoonekana kama kuepuka kuepusha mgongano, mvurugano na mtifuano kwenye mwaka huu wa uchaguzi, wakuu chamani wameamua na kupanga kumalizana na Makamba, Kinana na Membe kimyakimya.
Makamba, Kinana na Membe walitajwa kama watu waliopaswa kuitwa na kwenda kujibu tuhuma zao za kimaadili kwenye Kamati ya Maadili ya CCM. Lakini, hadi sasa hakuna wito uliowafikia wahusika hao na tayari wakuu wa chama wameamua kusaka suluhu bila sururu.
Inaaminika na kukumbukwa kuwa Makamba, Kinana na Membe ni wanaCCM wenye ushawishi mkubwa chamani na kuwashughulikia kwa sasa, miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani ni kuukaribisha mgogoro na kasoro ndani ya CCM.
Watatu hao, kwa mujibu wa makada waandamizi chamani, wanatajwa kama watu muhimu kiushauri na kikampeni katika kuhakikisha kuwa CCM inaibuka na ushindi wa kishindo kuliko nyundo kwenye uchaguzi mkuu ujao ambao tayari uko kwenye kona kama ya Banana.
Naunga mkono Makamba, Kinana na Membe kuachwa kama walivyo. Else, kama wakongwe chamani tutawatetea na kubaki nao kichama!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwa sasa Tunduma, Tanzania)