Makamba Amvaa Ngeleja: Ataka Mikataba Ya Wachimba Uranium

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
January Usikate Tamaa. Wewe ni mpiganaji . Wewe ndo dawa ya mafisadi Wizara hiyo imeoza kwa ufisadi! Pigana hadi kieleweke

Patricia Kimelemeta
KAMATI ya Bunge ya Nishati na Madini, imeitaka Wizara ya Nishati na Madini, kuwasilisha mikataba ya kampuni za Mantra na Urinex, zinazojihusisha na uchimbaji wa madini ya Uraniam, ili kuliwezesha Bunge kujiridhisha juu uhalali wao katika kufanya shughuli hizo. Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, January Makamba, ambaye alisema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa madini yenyewe katika dunia ya sasa.Alisema kukaguliwa kwa mikabata hiyo, kutasaidia kubaini uhalali na uwezo wa kampuni hizo katika kufanya shughuli hizo.

"Kuna kampuni mbili za uchimbaji wa madini ya Uranium hapa nchini, lakini hadi sasa mikabata yake hatujaiona, kwa hiyo tumeitaka wizara kuwasilisha mikataba hiyo kwenye kikao kijacho cha Bunge ili tuweze kuikagua,"alisema Makamba.
Alisema Kampuni ya Urinex inachimba madini hayo katika maeneo ya Manyoni, mkoani Singida na Bahi huko Dodoma wakati Kampuni ya Mantra, inachimba Uranium katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Alisema Serikali kupitia kamati hiyo inapaswa kuhakikisha kuwa madini yanawanufaisha wananchi kuiwezesha nchi kujiingizia mapato. Alisema madini hayo yanahitajika sana duniani katika shughuli mbalimbali na kwamba kwa msingi huo kama lazima ijue mikabata yote inayohusu uchimbaji wa Uranium.Alisema kutowasilishwa kwa mikataba ya kampuni hizo, kumeifanya kama yake, kushindwa kujadili suala lolote kuhusu kampuni hizo.


 
hivi kitu ishaanza kuchimbwa hapa nchini? ni mapato kiasi gani tunategemea kuingiza as a nation? hivi vitu vinapaswa kuwa disseminated to the public freely na sio mpaka watu walazimishwe kutoa information
 
Kijana Makamba piga kazi ukitapata weka wazi tujue mbivu na mbichi,wamezidi hao kutuona wajinga.
 
yaani unaliambia fisadi lisikate tamaa'wewe ndio kweli wee''mwenzio anatafuta uwaziri wa ngeleja kuliko jambo lolote'anapenda ukubwa sana yule barstard
 
sasa mwenyekiti wa madini anafanya kazi yake eti anataka uwaziri.kwa hiyo mlitaka aaache tu wabongo bwana
 
..tuombe MUNGU tu kusitokee ajali ya aina yoyote ktk mradi huo.
 
Environment Impact Assessment ilifanyika?ripoti yake pia ni muhimu sana. nchi itanufaikaje? au biashara ndio ile ya kuchimba kwanza miaka mitano bila kulipa kodi?
 
Back
Top Bottom