Makamba amtaka Tambwe atubu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba amtaka Tambwe atubu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Makamba amtaka Tambwe atubu

  2009-03-26 12:32:29
  Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya

  Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amewataka Hizza Tambwe na Lucy Rutainurwa kutubu kutokana na kushiriki kusema uongo walipokuwa vyama vya upinzani ili wananchi waichukie CCM.

  Tambwe kabla ya kujiunga na CCM, alikuwa Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Sera Chama cha Wananchi (CUF) huku Rutainurwa alikuwa Mwenyekiti wa (TLP) Mkoa wa Dodoma ambapo wote walirejea CCM.

  Makamba ambaye yupo katika ziara mkoani Mbeya, akiwa ameambatana na Tambwe kama Kaimu Katibu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM makao makuu na Rutainurwa, aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Uyole.

  [COLOR="Red]``Tambwe na Lucy wakati wapo vyama vya upinzani walikuwa waongo sana, sijui watasema nini kwa Mungu, itabidi wakatubu kwa kushiriki kusema uongo,`` alisema Makamba na kumwita Tambwe jukwaani kuwaeleza wananchi waliokuwepo hapo sababu za kujitoa CUF na kujiunga na CCM.[/B][/COLOR]

  [COLOR="Blue"]Makamba alikiri kuwa Tambwe wakati akiwa CUF alikuwa anaisumbua sana CCM na kwamba aligombea ubunge Temeke mara tatu mfululizo.

  Pia bosi huyo wa CCM alisema hata Rutainurwa alikuwa anakisumbua mno chama chake wakati akiwa TLP na hata aliupogombea ubunge.


  Kwa upande wake, Tambwe alisema CCM kamwe haitaweza kung`oka madarakani labda miaka 150 ijayo kwa sababu chini ya serikali ya serikali yake, wananchi wanaishi kwa matumaini kutokana na kuleta maendeleo makubwa nchini.

  Tambwe alidai kuwa wapinzani wanapenda kutumia umaskini wa Watanzania kuwatia hasira.

  Naye Rutainurwa alidai kuwa vyama vya upinzani siku zote vinapenda kuwashawishi vijana wanaokaa vijiweni kwa sababu ni wapiga kelele wazuri lakini kimsingi havina dira wala mwelekeo
  [/color]
   
 2. C

  Chuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bubu wakati mwingine unabore....kukopy na kupaste vichwa cha habari...kuna thread kibao za tambwe...kuanzisha thread mpya kila wakati too much....please brother...chuja basi...!!!
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Wote waganga njaa tu, hakuna mwenye uchungu na nchi, all of these political figure are loosers who got opportunity to lay their dirty hands on national fortune, but yana mwisho bana, wapi Mabuta, Kamuzu Banda, P. Botha, Chiluba, Pinochet, Hittler, Tito nk. walikuwepo watasepa ila their offspring na vizazi vyao vitalipa tu
   
 4. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukisikia siasa za maji taka ndiyo hizi. Wewe Tambwe hiza na hicho kituko chenzako mlipokuwa vyama vya upinzani mlilishwa yamini kusema mliyokuwa mnasema? Si mlisema kwa kupenda wenyewe? Hawa jamaa naona wamechanganyikiwa inatakiwa wakapimwe ubongo haiwezekani mtu ukakana maneno yako.

  Anasema vyama vya upinzani vinatumia vinajan wa vijiweni kupiga kilele! We Rutta na Tambwe tofauti yenu na hao vijana wa vijiweni ni nini? Wale hawawezi kujidhalilisha kwa kuvua nguo labda kama wamevuta bangi au madawa. Lakini nyie maneno na matendo yenu ni kama kichaa anayeenda bila nguo...

  HAFADHALI HATA HUO UONGOZI HAWAKUUPATA MAANA WA UMASKINI MPAKA WA AKILI
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Na WaTanzania watabadilika lini kuzikataa siasa za matumaini ? Huyo Tambwe inaonyesha kuwa yeye anapenda kuishishwa kwa matumaini ? Yaani Wafuasi wa SUltani CCM wamewafanya watu kuwa na itikadi ya kuishi kwa matumaini ,japo hujapata mkate na maharagwe kwa siasa za Sultani CCM usiwe na wasi wasi utasonga siku ya pili ,watatujengea barabara na mazahanati kila baana kilomita tano ,mashule kibao na badala ya wanafunzi kuwa wanaotandikwa bakora ,walimu ndio watakuwa wakitandikwa bakora ,yaani hawa CCM wanajua kuupalilia mwisho wao ,sasa huyo Tamwe awaeleze sababu ya CCM kuangushwa Zanzibar nzima na kusababisha polisi kuiba masanduku ya kura na kukimbia nayo.
   
 6. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Usanii at its best! Makamba kamzidi hata mzee Jongo!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Sichuji chochote kama unaboreka tafuta thread nyingine. Kwa taarifa yako tu ni kwamba Invisible alisharuhusu habari za magazeti mbali mbali kuwekwa hapa, sijui wewe ulikuwa wapi!!!! Kwani umelazimishwa kusoma kila habari hapa ukumbini!!!? Wenye forum yao wametoa ruhusa wewe kulalamika kila kukicha hebu tafuta kingine cha kusema hili lilishamalizwa na invisible. Watu wengine bwana!!!! :(
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa wanadhalilishwa hadharani kwamba walikuwa ni waongo sana lakini wameamua kukaa kimya tu!!! Tena mtu mwenyewe anayewadhalilisha ni Makamba ambaye ameshoanekana mara chungu nzima akienda kuona pochi kwa mafisadi akina Manji na Rostam!!!!Duh!!! huu ni upumbavu na unafiki wa hali ya juu. Kweli siasa ni mchezo mchafu!!!!
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135


  Anachekesha huyu mzee. Watubu jambo ambalo ndio lililowafanya wanunuliwe na CCM?
  Kule Upinzani ilikuwa cha mtoto lakini sasa wamefika kwa baba lao na sasa ndio wanasema uongo kwani walipokuwa upinzani na kuyasema mabaya ya CCM walikuwa wakisema ukweli na ndio maana wakakaribishwa CCM kuwaziba mdomo.
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Yani kutumiwa kwa NJAA ni kitu kibaya sana, yani Tambwe anasema wapinzani wanatumia umasikini wa watanzania kuwatia hasira. Kweli kuna mtu anafurahi kuishi maisha ya umasikini, unahitaji kuambiwa na mtu ili uwe na hasira kwa watoto kukaa chini, wazazi kujifungulia katika mazingira mabaya mno, kuishi bila maji, hospitali hakuna huduma nzuri, wakulima kukopwa ama kulipwa kidogo mazao yao nk. Kweli Tambwe umechoka kiakili.

  Na huyu Rutainurwa anachekesha sana, eti vyama vya upinzani vinashawishi wakaa vijiweni. Unadhani CCM ingeweka mazingira mazuri hawa wa vijiweni si wangepungua ama kutokuwepo kabisa. Kweli hawa jamaa ni kama Kuku, wananyea wanapolala.
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 83,055
  Trophy Points: 280
  Mfumwa, hizi kauli za hawa mabaradhuli zinasikitisha sana. Wanakubali kudhalilisha mbele ya kadamnasi halafu wanapewa nafasi ya kuzungumza na kuishia kutoa kauli ambazo hazina kichwa wala miguu!!! Halafu wakitoka hapo wanajisifia kwamba CCM ni nambari one!!!! Kumbe kumejaa mahayawani ambao wanaweza kusema chochote na kukubali kudhalilisha ili wagange njaa zao!!!
   
 12. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Inachosha kuona watanzania bado tunakubali kupigiwa siasa za kijamaa na kikomunisti! Nakubaliana na Bubu hawa akina Tambwe ndo wanaonyesha kufilisika kimaadili na kiakili kwa kuwa wanatukanwa na kudhalilishwa hadharani alafu hawasemi kitu bali wanazidi kutukuza chama. Lakini zaidi ya ku-express outrage ningpenda kuwakumbusha akina Tambwe:
  - CCM ndo ilikuwa mstari wa mbele ikiwashawishi vijana wa vijiweni mwaka 2005, tena wanamtandao walikuwa wanagawa sh 5,000 au 10,000 waende 'kumlaki' mgombea wao na ndo vijana hao walioshangalia kwa nguvu zote aliposhinda kura za maoni nakumbuka kule Jangwani, JK alienda kuongea nao na ilikuwa vurugu tupu, wamachinga, na vijana wa vijiweni wakishangilia kwa nguvu zote. Cha ajabu leo tunamsikia katibu mkuu akiwadhihaki vijana haohao na kuwa-dismiss. Lakini mwakani CCM watakuwa vijiweni wakiwahonga vijana wetu!
  Suluhisho ni kuwabana CCM washindwe kabisa kuiba kutoka Benki Kuu na wakose pesa za kuendesha uchaguzi... ndipo tutakapoona CCM hawana lolote, bila pesa na nguvu za dola.
   
 13. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2009
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  "Kwa upande wake, Tambwe alisema CCM kamwe haitaweza kung`oka madarakani labda miaka 150 ijayo kwa sababu chini ya serikali ya serikali yake, wananchi wanaishi kwa matumaini kutokana na kuleta maendeleo makubwa nchini".

  Ukickia kuishiwa ndio huku, yaani mheshimiwa ktk chama anatuambia watanazania tutaendelea kuishi kwa matumaini zaidi ya karne moja na nusu ijayo, huyu mtu ndio anatangaza sera ya chama chao, matumaini yenyewe yako wapi? mbona hayaonekani? au ni matumaini ya kuzidi kufisidiwa kwa nchi, kunyonywa na kuzidi kuzama ktk bonde la umaskini?

  "Naye Rutainurwa alidai kuwa vyama vya upinzani siku zote vinapenda kuwashawishi vijana wanaokaa vijiweni kwa sababu ni wapiga kelele wazuri lakini kimsingi havina dira wala mwelekeo"

  Maneno hayo wangesema wapinzani wangeonekana wanakikashifu chama tawala, lakini yametoka kwa watawala yanaonekana ni sahihi!!!
  Wanaacha kuwaelimisha wananchi ni vipi chama chao kimehusika na kashfa kubwa kubwa kama za EPA, KAGODA na nyenginezo; wanazungumzia wapinzani kuwachukua vijana wa vijiweni. Ila wananshindwa kujua hao vijana ndio product ya ya chama kushika hatamu maana hakuna ajira za uhakika, hakuna elimu ya uhakika na wala hakuna mitaji ya uhakika kama wanataka kujiajiri!!!
   
 14. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nachukia sana sema kuwa CCM imeleta maendelea, hivi kwa kipimo gani CCM imeleta maendeleo au ndio sekondari za kata alizosema Malecera juzi? hivi wanajua kuwa kuna wazazi wanalala chini Temeke Hospital au temeke hawafai kuwa na Hospital nzuri? Hivi maendeleo yanaletwa kwa kutumia resources kiasi gani maana hapa kuna issue ya tija (Efficiency)

  Wanatumia sh. 100 wanaiba sh. 1000 halafu wanadai wameleta maendeleo, Miaka zaidi ya 40 ya uhuru bado kuna sehemu ambazo hawajui hata barabara ya rami ikoje halafu unasema CCM imeleta maendeleo.

  mwakani hakuna EPA tutaona kama mtashinda.
   
 15. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mmmmmh na wewe Bubu huna dogo!! msamehe basi mwenzio
   
 16. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hao sio wanasiasa ni wajasiliamali fulani wanaotafuta maisha. For no reason only fools can join CCM these years.
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mhhhh, kama walikuwa wanasema uongo walipkuwa huko, nitaaminije kuwa wanayoyasema sasa ni ukweli! Just wondering
   
Loading...