Makamba amka! Nusu ya nchi inaelekea kuwa jangwa

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,179
7,330
Tatizo
1. Tafiti zinaonyesha kati ya 55-65% ya archi ya Tanzania ipo hatarini kuwa jangwa miaka 20-30 ijayo. Ni tatizo ambalo lipo pia nchi nyingine za Africa

2. Namna pekee ya kunusuru mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho ni kwa kupanda miti

3. "Mahubiri" ya upandaji miti yamekuwa kama nyimbo zisizo na wasikilizaji wala wachezaji. Utekelezaji umekuwa sifuri.

4. Mwezi April mwaka 1999 raisi Mkapa alizindua programu ya upandaji miti iliyplenga kuandwa kwa miti milioni 10. Hata hivyo lengo la milioni kumi halikufikiwa hata kwa 20% na hata ile iliyopandwa zaidi ya 80% inasemekana ilijifia kwa kukosa matunzo. It was a failure to say so...

5. Tokea wakati huo hakujawa na plan zozote za maana za upandaji miti na hali ya mazingira inazidi kuwa mbaya

Suluhisho
1. Kwanza nisikitike kusema tangu apewe nafasi hiyo miezi takribani 6 iliyopita sijawahi kumuona waziri anayeshughulika na mazingira hata akipanda mche mmoja wa mti. Hii ni ishara mbaya juu ya uwepo wa azma yeyote ya serikali kuokoa mazingira

2. Kwa hiyo namshauri wazi mhusika Bwana J. Makamba "aamke" aanzishe program ya "kufa na kupona" ya upandaji miti. Natambua wizara yake inajishughulisha na masuala mengi ya mazingira lakini naomba suala la upandaji miti lipewe uzito wa kipekee

Ushauri

Najua zipo namna nyingi za kufanya program endelevu za upandaji miti. Naomba nipendekeze hii moja.
Shule zote za msingi na sekondari nchini zitakiwe kuwa sehemu ya program. Kila shule, chini ya usimamizi na ushauri na msaada wa halmashauri ianzishe kitalu cha miche ya miti shuleni. Waziri husika (makamba) awe ndiye mwezeshaji na mhamasishaji mkuu kwa kuandika hiyo program, kuigawa kwenye halmashauri zote na kutembelea kila halmashauri kuhakikisha program inatekelezeka.

Plan iwe kila shule ipande miche angalau 10,000 kwa mwaka na kila mwanafunzi ahusike moja kwa moja na upandaji na utunzaji wa angalau miche 100 kwa mwaka. Miche inayopandwa mashuleni igawiwe kwa wananchi wanaozinguka shule na hasa wazazi wa wanafunzi, na kuwe na uhamasishaji na usimamizi wa miti hiyo kupandwa na kutunzwa

Faida
1. Program ya kuhusisha shule itasaidia kutoa mafunzo na hamasa juu ya upandaji na utunzaji miti

2. Tanzania kuna jumla ya shule ziadi ya elfu kumi za msingi na sekondari (za serikali). Kama program hii ikifanikiwa kwa angalau 50% ya shule, ina maana miche 50,000,000 itapandwa kwa mwaka. Hii ina maana kama miche hiyo ikipona kwa ngalau 50% miche 25,000,000 itapandwa kwa mwaka, na kama hiyo ikifanikiwa kutunzwa na kukuzwa, ina maana miti milioni 12.5 itapandwa kwa mwaka.

3. Program hii ikifanyika kwa miaka 10 ina maana miti zaidi ya milioni 125 itakuwa imependwa.

Sustainability
1. Najua "kikwaz0" cha kwanza mtu atasema program ya namna hii inahitaji fedha nyingi na hazipo kwa sasa. Lakini hebu tujiulize fedha kiasi gani zitahitajika kuanzia hatua ipi ya mradi. Kwa mfano Programu itahusisha hatua zifuatazo
i. Kuandika program
ii. Kusambazwa program kwenye mashule
ii. Kuandikisha shule zinashoshiriki
iv. Shule kutenda eneo la kitalu
v. Kulimwa na kutengenezwa vitalu

Hadi hapa naweza kusoma ni 0 cost.

Kwa maana hiyo utaweza kuona kinachohitajika ni azma, nia, na uwajibikaji tu. Gharama ndogo ndogo kama stationeries na gahrama za mawasiliano na ufuatiliaji ni gharama za kawaida za ofiri wala hazihitaji bajeti maalumu.

Gharama za vifaa kama vifuko vya kupandia mbegu nina uhakika shule zinaweza kujipanga na zikapata hivyo vifaa ambavyo havizidi Tsh 20,000 wa shule moja.

Wanafunzi wanahamasishwa kuleta mbegu za miti mbalimbali kutoka kwenye mazingira yao na pale zitakapohitajika mbegu za kununua halmashauri zinaweza kusaidia kupitia ofisi za misitu na wakala wa miti wa taifa...

Nawasilisha
 
Mkuu nimefarijika sana na uzi wako. Nchi inaenda kubaya. Vijito vinakauka, miti hakuna, milima imebaki na mawe matupu.

Nakumbuka wakati JK anaingia madarakani kwa mara ya kwanza alitoa hotuba nzuri sana na aliongelea suala la mazingira na akatukumbusha kwamba tujiulize kama vile vijito vilivyokuwepo wakati tukiwa watoto kama bado vipo. Nikajikumbusha nikakuta hakuna hata kimoja. JK akasema VP atakuja na mkakati wa kutunza mazingira; VP akaja na mikakati lukuki: Wanajeshi wapande miti, mkaa marufuku hadi kwa kibali (mkaa ukapotea bei ikawa kubwa) na mengine mengi. Lakini baada ya muda hakuna kilichoendelea matokeo yake nchi inayoyoma kuwa jangwa.

Juzi kodi ya gesi imepanda nadhani sasa matokeo yake ni kuendelea kushambulia vimisitu vichache vilivyobaki ili kujipatia nishati ya mkaa.

Hakina Makamba anatakiwa aje ni mikakati ya kuirudisha nchi kwenye umbijani. Hii si siasa ni uhai wa nchi.
 
Mkuu umanikumbusha ile mikakati ya JK... itabidi nijaribu kufuatilia machapisho kama ilitekelezwa na ilishindwa wapi...

Kwa kweli suala la upandaji miti inabidi lipewe muamko mpya na nguvu ya kipekee...
 
Wazo zuri kwa kuongezea halmashauri ishirikiane na ofisi ya kijiji kuhakikisha inapatiwa ardhi ya kutosha na yenye rutuba kwa ajili ya upandaji miti hyo lakini pia,na eneo liwe karibu ya shule,nimependekeza ofisi ya kijiji ihusike kwa sababu ofisi nying zipo vijijini,kingne ni lazma tuhakikishe tunajitahada za makusudi za kulinda mapori na misitu yetu,shughuli kubwa zinazoharibu misitu ni uchomaji mikaa,kutengeneza mbao na ufugaji hasa ndugu zetu wasukuma,na kilimo chao cha kuhamahama,so cha kufanya 1 kuwahmiza kutokuwa na mifugo mingi watakayoshndwa kuihudumia 2.kuwatengea maeneo maalum ya ufugaji wa kisasa kubwa ambalo itakaa mifugo ya kutosha na kila kitu kipatikane wasilazimike kuhama eneo na mwisho shughuli za ukataji uvunaji misitu kwa ajili ya mbao na mkaa ziangaliwe upya,
 
Hicho cheo ni kama hakitaki vile?
Simuoni akishughulika kama alipokuwa katika wizara ya awamu iliyopita.
Naona humfahamu makamba, aliwahi kufanya nini lenye manufaa kwa nchi? yooote aliyo fanya yalikuwa na manufaa kwa chama chake, hata hio sheria ya makosa ya mitandao pamoja na kuwa na vipengele vyenye manufaa kwa umma inavyo pia vya kukifavour chama na selekali na kama vingekosekana, nina uhakika mswada huo usinge kanyaga bungeni. Makamba ni wa manufaa kwa ccm yake si kwa taifa! hivyo hawezi kununua wazo hili.
 
Tanzania ndio nchi pekee duniani ambako mtu anaamka asubuhi na mtaji wa baskeli na panga anaingia msituni anakata miti na kuchoma mkaa anarudi jioni na kuuza kujipatia mlo wake wa siku bila kupanda mti mwingine au kuulizwa kwa nini unaharibu maliasili ya watanzania wote. Huwezi kuachia maliasili ikateketezwa hovyo namna hii wakati wazungu walituletea miradi ya participatory forest management ikatupwa mara baada ya wazungu kuondoka na serikali kulala. Acha tuwe jangwa
 
Wazo zuri sana hili.

Na serikali inachotakiwa si kuwagawia tu wananchi miti wakapande, lakini kuwatumia watoto wa shule kupanda hii miti majumbani mwao.

Kama kila mtoto wa shule ya msingi na sekondari akilazimishwa kwa mwaka apande nyumbani kwao miti mitatu na kuitunza itakuwa rahisi sana kusambaza miti hii majumbani.

Miti iachwe kuuzwa pia.

Wananchi wako tayari kupanda miti, tatizo mamlaka zinauza miti bei ghari sana, idara za maliasili zimeigeuza hii kitu kuwa biashara.

Kinachonisikitisha ni kuwa idara za serikali zimegeuza hii kuwa biashara na zinatumia mwanya huu ufanya biashara.
 
Ni wazo zuri ila ingefaa pia ukajikita zaidi kwenye changamoto.
Kuna baadhi ya wilaya hapa Nchini wamenufaika sana na faida za upandaji miti.
Wilaya kama Sengerema, Mafinga, Njombe na Makete wamehamasika sana na upandaji wa miti na ndo imekuwa kama shughuri yao rasmi inayopa uhakika wa kuboresha maisha yao. Wengi wametajirika kupitia upandaji na uvunaji miti.
Kanda zote hizo hakuna muingiliano wa wafugaji waharibifu tofauti kabisa na mikoa mingine kama Morogoro ambapo wananchi wanashindwa kuhamasika na upandaji wa miti kutokana na ufugaji holela wa mifugo ambao kwa kiasi kikubwa umechangia sana kufifisha jitihada hizi.
Ni gharama kubwa sana kumudu utunzaji wa shamba la miti kwa mikoa iliyozagaa wafugaji holela hasa jamii za kimaasai na baribaig.
Kwa kipindi cha miaka3 niliyoishi Morogoro, nimeshuhudia uharibifu mkubwa sana wa mazingira na mashamba ya miti unaosababishwa na hawa wafugaji.
Wakulaumiwa ni Serikali kwa kukosa program endelevu kunusuru misitu na ufugaji holela.
 
hongera mleta uzi, kwa kweli mimi ni mkulima na ni mpenzi wa mazingira toka tumboni kwa mama yangu. Huku vijijini vijana wameachana na kilimo wanakazana na kukata mkaa, hakuna anayewaza hata kupanda kisamvu. Wenye jukumu la kutoa elimu ya mazingira wako maofisini wanachat kwenye facebook na mainstagram, wakitoa ripoti wakopy na kupaste ya miaka iliyopita!!! Sipati picha ndani ya miaka 10 nchi hii itakuwa kwenye hali gani. Naunga mkono asilimia 100 mawazo ya mleta hoja.
cc: January Makamba
 
Kwanza serikali ingetafuta chanzo mbadala wa kuni na mkaaa
Gesi ilitakiwa iuzee bei ndogo ili mkaa ukose thamani na watu wahamie kwenye gesi
Hapo miti itasalimika tofauti na hapo tutakuwa twapigia mbuzi gitaa
 
Kwanza serikali ingetafuta chanzo mbadala wa kuni na mkaaa
Gesi ilitakiwa iuzee bei ndogo ili mkaa ukose thamani na watu wahamie kwenye gesi
Hapo miti itasalimika tofauti na hapo tutakuwa twapigia mbuzi gitaa[/QUOTE
Mkuu yan mi nimeshangaa gesi kua juu bajeti mpya sijui wanalengo gani na sisi mi mkaa sihupendi kabisa lakin wanatulazimisha..nchi hii hatar
 
Wazo zuri sana hili.

Na serikali inachotakiwa si kuwagawia tu wananchi miti wakapande, lakini kuwatumia watoto wa shule kupanda hii miti majumbani mwao.

Kama kila mtoto wa shule ya msingi na sekondari akilazimishwa kwa mwaka apande nyumbani kwao miti mitatu na kuitunza itakuwa rahisi sana kusambaza miti hii majumbani.

Miti iachwe kuuzwa pia.

Wananchi wako tayari kupanda miti, tatizo mamlaka zinauza miti bei ghari sana, idara za maliasili zimeigeuza hii kitu kuwa biashara.

Kinachonisikitisha ni kuwa idara za serikali zimegeuza hii kuwa biashara na zinatumia mwanya huu ufanya biashara.
Kweli kabisa mkuu...

Na hii inaweza kuhamasishwa zaidi kwa mfano wakiweka mipango ya kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi na shule bora... ikawa kama mashindano hivi...
 
Tatizo
1. Tafiti zinaonyesha kati ya 55-65% ya archi ya Tanzania ipo hatarini kuwa jangwa miaka 20-30 ijayo. Ni tatizo ambalo lipo pia nchi nyingine za Africa

2. Namna pekee ya kunusuru mazingira kwa faida ya kizazi hiki na kijacho ni kwa kupanda miti

3. "Mahubiri" ya upandaji miti yamekuwa kama nyimbo zisizo na wasikilizaji wala wachezaji. Utekelezaji umekuwa sifuri.

4. Mwezi April mwaka 1999 raisi Mkapa alizindua programu ya upandaji miti iliyplenga kuandwa kwa miti milioni 10. Hata hivyo lengo la milioni kumi halikufikiwa hata kwa 20% na hata ile iliyopandwa zaidi ya 80% inasemekana ilijifia kwa kukosa matunzo. It was a failure to say so...

5. Tokea wakati huo hakujawa na plan zozote za maana za upandaji miti na hali ya mazingira inazidi kuwa mbaya

Suluhisho
1. Kwanza nisikitike kusema tangu apewe nafasi hiyo miezi takribani 6 iliyopita sijawahi kumuona waziri anayeshughulika na mazingira hata akipanda mche mmoja wa mti. Hii ni ishara mbaya juu ya uwepo wa azma yeyote ya serikali kuokoa mazingira

2. Kwa hiyo namshauri wazi mhusika Bwana J. Makamba "aamke" aanzishe program ya "kufa na kupona" ya upandaji miti. Natambua wizara yake inajishughulisha na masuala mengi ya mazingira lakini naomba suala la upandaji miti lipewe uzito wa kipekee

Ushauri

Najua zipo namna nyingi za kufanya program endelevu za upandaji miti. Naomba nipendekeze hii moja.
Shule zote za msingi na sekondari nchini zitakiwe kuwa sehemu ya program. Kila shule, chini ya usimamizi na ushauri na msaada wa halmashauri ianzishe kitalu cha miche ya miti shuleni. Waziri husika (makamba) awe ndiye mwezeshaji na mhamasishaji mkuu kwa kuandika hiyo program, kuigawa kwenye halmashauri zote na kutembelea kila halmashauri kuhakikisha program inatekelezeka.

Plan iwe kila shule ipande miche angalau 10,000 kwa mwaka na kila mwanafunzi ahusike moja kwa moja na upandaji na utunzaji wa angalau miche 100 kwa mwaka. Miche inayopandwa mashuleni igawiwe kwa wananchi wanaozinguka shule na hasa wazazi wa wanafunzi, na kuwe na uhamasishaji na usimamizi wa miti hiyo kupandwa na kutunzwa

Faida
1. Program ya kuhusisha shule itasaidia kutoa mafunzo na hamasa juu ya upandaji na utunzaji miti

2. Tanzania kuna jumla ya shule ziadi ya elfu kumi za msingi na sekondari (za serikali). Kama program hii ikifanikiwa kwa angalau 50% ya shule, ina maana miche 50,000,000 itapandwa kwa mwaka. Hii ina maana kama miche hiyo ikipona kwa ngalau 50% miche 25,000,000 itapandwa kwa mwaka, na kama hiyo ikifanikiwa kutunzwa na kukuzwa, ina maana miti milioni 12.5 itapandwa kwa mwaka.

3. Program hii ikifanyika kwa miaka 10 ina maana miti zaidi ya milioni 125 itakuwa imependwa.

Sustainability
1. Najua "kikwaz0" cha kwanza mtu atasema program ya namna hii inahitaji fedha nyingi na hazipo kwa sasa. Lakini hebu tujiulize fedha kiasi gani zitahitajika kuanzia hatua ipi ya mradi. Kwa mfano Programu itahusisha hatua zifuatazo
i. Kuandika program
ii. Kusambazwa program kwenye mashule
ii. Kuandikisha shule zinashoshiriki
iv. Shule kutenda eneo la kitalu
v. Kulimwa na kutengenezwa vitalu

Hadi hapa naweza kusoma ni 0 cost.

Kwa maana hiyo utaweza kuona kinachohitajika ni azma, nia, na uwajibikaji tu. Gharama ndogo ndogo kama stationeries na gahrama za mawasiliano na ufuatiliaji ni gharama za kawaida za ofiri wala hazihitaji bajeti maalumu.

Gharama za vifaa kama vifuko vya kupandia mbegu nina uhakika shule zinaweza kujipanga na zikapata hivyo vifaa ambavyo havizidi Tsh 20,000 wa shule moja.

Wanafunzi wanahamasishwa kuleta mbegu za miti mbalimbali kutoka kwenye mazingira yao na pale zitakapohitajika mbegu za kununua halmashauri zinaweza kusaidia kupitia ofisi za misitu na wakala wa miti wa taifa...

Nawasilisha

Mkuu kwa wapenda mazingira kama sisi,tumefarijika sana na makala yako

Ni ukweli ulio wazi,serikali ikiamua,hakuna gharama yoyote kubwa kwenye utekelezaji wa mpango huo wa upandaji miti.

Kama mtakumbuka Mzee makamba alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar,alilazimisha kila mtu apande miti nyumbani kwake,watu tunaopenda mazingira tuliitikia wito tukapanda miti,hata kama zoezi halikufanikiwa sana kutokana na viongozi wengi hutoa matamko kisiasa zaidi,lakini Leo hii Dar ina uafadhali wa miti na kupendezesha mji tofauti na miaka ya nyuma.

Katika kutekeleza zoezi hilo la upandaji miti,Serikali inaweza kuwatumia wafungwa wenye makosa mepesi ambao wapo mikoa yote.Pia kuna majeshi kama JKT,migambo hawa wakitumika vizuri zoezi lisingekuwa na gharama.

Na katika kufanya watu wote washiriki kwenye kampeni hiyo,inatakiwa viongozi wa dini washirikishwe kwa wao kuhamasisha waumini,mfano mzuri ni kanisa la KKT Kilimanjaro, askofu wao ametoa agizo,kila mtoto anayepokea kipaimara ni lazima apande miti 20,ambapo serikali haijahusika hata chembe.

Na sisi wenye uchungu na jambo hilo tuhamasike kuwa mfano kwa kupanda miti mahali tulipo.Mimi kwangu nilitengeneza bustani ya miti,ambapo hadi leo majirani zangu wanatumia kufanya vikao mbalimbali,hivyo tusiishie kuiambia serikali peke yake,bali tuonyeshe mfano.Ahsante naomba kuwasilisha!
 
Back
Top Bottom