Makamba akataa CCM kukutana na Chadema

Move ya CDM bado naiona ni nzuri tuu, Alichokifanya Mbowe ni kizuri sana maana mambo yakishindikana na ya kurudi kwenye nguvu ya Umma CDM haina lawama kwani imeshaomba mambo haya yajadiliwe mezani lakini wakapuuzwa hivyo wameyapelaka kwa wapiga kura walioibiwa ili wachukue hatua wenyewe.

Kuhusu kuwafukuza Bungeni wabunge wa CDM, kosa hilo CCM hata kama mara nyingi hawatumii akili kwenye maamuzi hawawezi kulifanya. Kumbukumbu ya Kumfungia Zitto kisha mashtaka yakapelekwa kwa wananchi bado wanayo. Maana kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, ndipo iliposhuhudiwa Mawaziri na viongozi wakizomewa hadharani,misafara yao ikitupiwa mawe hadi ule wa Rais na nguvu ya CDM ikipata kasi zaidi.

Mie nafikiri Mbowe na CDM wanajua CCM ilivyo na walifahamu jeuri ya CCM na kuwa tamko lao la kutaka kukaa meza moja LITAKATALIWA ,ila wamelitoa maksudi ile kukwepa lawama hapo baadae kuwa hawakutaka majadiliano na serikali.

Now CHADEMA, plan A succeded, move to plan B, mwagikeni uraiani muwaeleze wananchi jinsi walivyo ibiwa uhuru wao wa kuchagua viongozi, wizi ambao ni mbaya sana kuliko aliyevunja nyumba na kukuibia RADIO NA NGUO.
 
Nimegundua watu mnajadiri mada kwa kutumia hasira na ushabiki, you are not realistic and logical! huu ni mgogoro na mgogoro lazima uwe na stages can't you know that? with this conflict process kuna watu watakuja kukalishwa chini na kuulizwa kwa nini mmelifikisha taifa mahala hapa? kila mmoja atatakiwa kueleza jitihada zake zakutetea hayo yaliyolifikisha taifa katika maangamizi na huo utakuwa utetezi wake mbele ya mahakama ya kimataifa.

Hivyo msidhani CDM niwajinga wanatasira ya kuona mbali leo tunasema CDM lakini itafika siku ambapo Mbowe atasimama yeye kama yeye Dr.Slaa atasimama yeye kama yeye na kutoa utetezi wake makamba,chilgati,kikwete hivyo hivyo wata sema nafasizao kwa yaliyo tokea.We need to be proactive lazima kuwe na provission yakujinasua kwenye mtego ambao utakutia kitanzi wewe binafsi yatakapokuwa yametokea yakutokea na wewe ukiwa mhusika mkuu.

Apingaye maono yangu na aniambie kwanini hajaandika jina lake la ukweli hapa jamvini? kwanini unajiita Kishoka,arasululu,nyani,mfuatiliaji, Dar es salaam hivyo ndio majina uliyo batizwa na wazaziwako au ndugu zako au projections za kuogopa kuwa responsible kwa kaulizako hapa jamvini. Nadhani nimeeleweka
 
Mwanakijiji mimi naona hoja yako kwa pande mbili.

1. True advise to CCM

2. Au mtego

But

All in all ni mada yenye mashiko ya kujadiliwa.

Kwanza kabisa, madai ya Chadema according to katibu mkuu (aliyekuwa mgombea kiti cha urais wa muungano Dr. Slaa ni kupinga mchakato mzima wa NEC uliomweka madarakani Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.Huo ndio ulikuwa msingi wa hoja iliyowafanya wabunge wa Chadema kutoka nje ya Bunge kususia Hotuba ya Rais ya Ufunguzi wa Bunge.

Chadema na sisi sote twafahamu kuwa, kwa katiba hii tuliyonayo, tume ikishatangaza basi there is no recall.Matokeo cannot be challenged kwenye chombo chochote cha haki pamoja na kuwa ni uhaini.

Walichofanya Chadema ni jambo moja muhimu sana.Kutomtambua Kikwete kama Raisi aliyechaguliwa na Wana wa nchi wa JMT na wanamtambua kama raisi aliyewekwa madarakani na tume (by-defacto) na ujumbe huu umefikishwa kunakopaswa na ndicho kinachomfadhaisha Kikwete pamoja na CCM kuwa Raisi aliyeko madarakani si kwa ridhaa ya wananchi BALI ni kwa ridhaa ya tume.Huu ndio ulikuwa ujumbe very bold and was echoed kisawasawa.

Nini ambacho CCM wanataka?

CCM wanataka Chadema imtambue Kikwete kama raisi aliyechaguliwa na wananchi ili wapate legitimacy ndani na nje ya nchi.Hicho ndicho kinachokosekana na Chadema wamewanyima.

Ni nini Philosophy ya matendo ya wabunge wa Chadema?

Ni wazi...kiini cha matatizo haya yote ni KATIBA.For what it worth kama katiba yetu ingeruhusu a people centered democratic processes haya yote yasingetokea. Tunachokikosa ni ule msimamo thabiti kupita hisia zozote za kiitikadi wenye kutetea misingi ya demokrasia komavu na kujali sauti ya umma.

The demands here goes beyond what some pundits see as short term benefits such as vyeo na masurufu ambayo wabunge watayapata or whether to be thrown out of the parliament abusively( without justice) using popularity in the house improperly to serve the interest of the few.

I bet that DR. Slaa and Chadema are thinking beyond this limit and that is precisely what bothers CCM and other allies

Nini kimefanyika?

Ili kupata legitimacy ya kuanza mabailiko ya katiba, lazima uombe yule mwenye madaraka (government) kujadili mustakabali wa matatizo haya yote bila kujali itikadi yeyote na kuweka maslahi ya Taifa mbele ili wakikataa CHADEMA watakuwa na cha kuwaambia wananchi.

Nini kinafanyika sasahivi?

Nionavyo mimi CHADEMA wanajibu maswali ambayo wataulizwa hapo baadaye.

CHADEMA WATAENDA SUPREME COURT:KWA WANA WA NCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMBAKO WATAPATA VERDICT YENYE KUBEBA USHINDI WA KISHINDO AMBAO UTATEKELEZWA RASMI 2015 NA MAHAKAMA HIYO ILIYOKUBWA KULIKO MAHAKAMA ZOTE TANZANIA.

CCM hawaoni mbali.Pengine kosa ambalo watafanya ni kupitisha azimio la kuwaondoa wabunge wa CHADEMA BUNGENI.Kufanya hivyo utakuwa ni msumari wa mwisho katika JENEZA la CCM and we flip OVER a NEW CHAPTER.

Hilo azimio litawasha moto ambao hautazimika kamwe hadi 2015 na hapo ndio wamewapa CHADEMA fursa ya kujijenga zaidi wakati CCM wanajitetea kwa mashataka ambayo CHADEMA watayapeleka kwa supreme court ya WANA WA NCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

Mkuu asante kwa kuondoa huu mvurugano ktk kujadili hii hoja..maelezo yako yanatosheleza kufunga huu mjadala kilichobaki CDM utekelezaji:A S crown-1:
 
Mimi nadhani kuwa CDM wanaitegea CCM ili kujustify the next step ya kuleta public grievances zao public, kuwa wamekataa kuzungumza. Kama kawaida CCM ni short sited, na hasa Makamba ni hodari kutoa snap judgements.

MMK usikate tamaa. Siku zote mmoja wa huonyesha njia na hasa pale ambapo vita ni vikubwa, keep up your spirit dont dispair
 
SIKU moja baada ya Chadema kusema ipo tayari kuketi meza moja na serikali, chama tawala au taasisi nyingine yoyote kwa ajili ya mazungumzo, katibu wa CCM, Yusuf Makamba amesema chama hicho hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema juzi kuwa wako tayari kukaa meza moja na serikali au wadau hao ili kujadiliana nao kuhusu msimamo wao wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, madai ambayo yameimarisha hoja ya kuundwa kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Hata hivyo, Mbowe aliweka bayana kuwa mazungumzo hayo yasiwe ya kuweka mbele maslahi ya kisiasa na wala yasijikite kwenye kauli zinazotolewa na Makamba na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati na badala yake yaweke maslahi ya taifa mbele.

Lakini jana Makamba alisema chama chake hakina jambo lolote la kuzungumza na Chadema na kwamba sasa siasa zinahamia bungeni.


Makamba,ambaye huzungumza kwa mifano ya vichekesho na pia kutumia vitabu vitakatifu vya Biblia na Qorani, alianza kunukuu kifungu kitabu cha Methali 18:18 katika Biblia kinachosema: “Kura hukomesha mashindano; hukata maneno ya wakuu.

“Sisi wote tulikwenda kwenye uchaguzi, kura zikapigwa, aliyeshinda anajulikana na walioshindwa wanajulikana, sasa sisi tukutane na Chadema tuzungumze nini? Wao watafute watu wengine wa kuzungumza nao si CCM.”

Kwa mujibu wa Makamba, kwa sasa siasa zinahamia bungeni na kwamba endapo Chadema wanataka siasa za nje ya Bunge, wasubiri tena mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.

“Tutakutana bungeni kwenye kujadili sera, kwa sasa sisi tunaunda serikali,” alisema Makamba ambaye katika Bunge la Tisa alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais.

Naye mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kukuza demokrasia nchini inayoitwa Agenda Participation 2000, Moses Kulaba alipongeza uamuzi wa Chadema, lakini akaonyesha wasiwasi kama serikali itakuwa tayari kukaa na chama hicho.

“Ni jambo jema kwa Chadema kukubali maridhiano, lakini serikali itakuwa tayari kuzungumzia mambo haya,” alisema Kulaba.


Kulaba alisema mapambano yaliyoanzishwa na Chadema yanatakiwa yawe chachu ya kudai mabadiliko ya katiba pamoja na tume huru ya Uchaguzi baada ya hii iliyopo kulalamikiwa tangu uchaguzi unaoshirikisha vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1995.

“Kilio cha kudai hivi vitu kilianza tangu mwaka 2000, sasa inatakiwa Chadema iwe chachu ya mabadiliko hayo. Zanzibar wamefanya mabadiliko ya katiba; uchaguzi umeenda vizuri hakuna malalamiko kwanini ishindikane Tanzania Bara,” alihoji Kulaba.


“Tume ya Uchaguzi ni chombo muhimu sana, lakini pamoja na malalamiko ya miaka yote, kutoka mwaka 1995 mpaka leo, (Jaji Lewis) Makame amekuwa mwenyekiti wa tume hiyo,” alisema Kulaba.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ally, alisema bado Chadema haijaweka bayana madai yao ili wananchi waweze kuwaelewa. Bashiru alisema baada ya waangalizi wa uchaguzi kutoa ripoti zao kamili, itakuwa ni wakati muafaka wa kujua kilichotokea katika uchaguzi huo.
CHADEMA pokeeni kwa mikono miwili ya furaha ushauri wa makamba wa kuongea na watu wengine na si ccm hivyo nendeni kwa wananchi.njooni kwetu tutoe maoni yetu.makamba atajuta kwa kauli yake
 
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!
Heshima yako Mzee Mwanakijiji!
Do I need to say more?You're damn right!Na ndiyo maana Makamba amewaambia siasa sasa ni bungeni na sio kukaa nao meza moja.Wakitaka siasa za nje wasubiri uchaguzi.Kwa maana nyingine anawaeleza kama 46 dhidi ya 176 wataweza kupitisha mabadiliko yeyote pamoja na msimamo waliokwisha chukua ambao unaongeza uadui zaidi.
 
chadema ni watu makini, mbowe amesema wakae chini wajadiliane kwa maslahi ya nchi na si maslahi ya kisiasa. Makamba amekurupuka na kukataa majadiliano ya amani (kidemokrasia) hatua ya pili chadema watatufuata wananchi, hatua ya tatu tutachukua maamuzi. 4. tutauona unafiki wa nchi za magharibi maana hatua zote za amani zilishindikana

makamba subiri moto wake na tunaanza na familia zenu wahusika
 
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo.

Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.

Waombe msamaha kwa kosa gani? Hoja za makamba ni za mshabiki asiye na dhamira yo yote nzuri na taifa hili. Kwake yeye siasa ni ajira (Ndiyo maana anawakumbatia na kuamrishwa na mafisadi). Issues za kujadiliwa ni za kitaifa. Wasipojadiliana na serkali ya ccm au na CCM watashitakiwa kwa wananchi hata kama watatumia jeshi.

Chadema hawakuanza kuweka masharti ya majadiliano ni serikali ya ccm na ccm ndio wanachokoza majadiliano waone upepo unavumia wapi. Mapambano yanahitaji ukomavu ambao unatokana na uzoefu. CCM hawajifunzi na hawatajifunza kutokana na historia hata ya hapa nchini. Kwa hiyo kama mapambano ni bungeni ni vema, hoja zitajibiwa kwa hoja. Kweli wana wingi wa kupitisha jambo lo lote hata la kipuuzi lakini jamii italipokea kwa kuwahukumu.
 
CHADEMA pokeeni kwa mikono miwili ya furaha ushauri wa makamba wa kuongea na watu wengine na si ccm hivyo nendeni kwa wananchi.njooni kwetu tutoe maoni yetu.makamba atajuta kwa kauli yake

Makamba my foot. Akawashauri wenye mtindio wa ubongo. Huo ushauri alioutoa kwa CHADEMA hautapokelewa hata kwa kucha. Jibu la Makamba halingekuwa bora zaidi ya hilo. Kwa sasa hivi anaweweseka na Chadema subiri taarifa nyingine toka kwake utashangaa. Maanake atasema ya mtaani baada ya kitaifa. Yeye siasa kwake ni ajira ya kulinda ufisadi unaotafuna taifa. Kwenda kwa wananchi sawa lakini siyo kwa wenye maoni kama ya makamba. Hivi maandamo ya CCM kulaani Chadema kutoka nje wakati wa hotuba ya JK yameishia wapi?
 
Hapatakalika hapo bungeni hadi kieleweke........

Hata kama makamba hataki kufanya mazungumzo na chadema... Iko siku atawatafuta yeye mwenyewe.. Wakati wanapelekwa mahakamani kwa kufuja mali za ummaa.......
 
Makamba my foot. Akawashauri wenye mtindio wa ubongo. Huo ushauri alioutoa kwa CHADEMA hautapokelewa hata kwa kucha. Jibu la Makamba halingekuwa bora zaidi ya hilo. Kwa sasa hivi anaweweseka na Chadema subiri taarifa nyingine toka kwake utashangaa. Maanake atasema ya mtaani baada ya kitaifa. Yeye siasa kwake ni ajira ya kulinda ufisadi unaotafuna taifa. Kwenda kwa wananchi sawa lakini siyo kwa wenye maoni kama ya makamba. Hivi maandamo ya CCM kulaani Chadema kutoka nje wakati wa hotuba ya JK yameishia wapi?
Thubutu, yalitolewa tamko la kufutwa (na wao wenyewe) sio zaidi ya saa moja baada ya kutangazwa. Habari ni kuwa wale walioibiwa kura zao walikuwa wanasubiri huko mtaani ili wawa adhibu wale wanaoandamana kushangilia jinsi walivyo waibia. DSM isingekalika na CCM waliligundua hilo.
 
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo.

Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.

Kwenye green nakubaliana na wewe mkuu. lakini nafikiri both parties in the saga should trade a bit of their pride while CDM maintain its position on election process and the need for constitutional review.
 
Sasa hapa ndipo mtakubaliana na ambao tulishasema kwamba Chadema wamepoteza na wataendelea kupoteza chance muhimu sana. Kutoka nje iliwapa political gain kubwa sana, lakini kudefend argument yao imesababisha waonekane kituko. Na haya yote yanarudi pale pale, Mboe sio great leader period.

Wameshindwa kuarticulate kitu muhimu sana kuonyesha Watanzania nini umuhimu wa kutomtambua JK, sasa wanaonekana kama wahuni fulani. CCM hawawezi kukaa chini na Chadema, because wamesha smell blood.

MM umeongea point sana, ni wazi ccm watarudisha mmjadala bungeni wa kuwabana Chadema waombe ruhusa and i doubt kama watafurukuta.
 
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo.

Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.

Mkubwa umesahahau msemo mmoja unaosema hivi "Ukiona watu wote na kwa nyakati,na fikra na mitazamo inafanana,basi ujue kwamba fikra na mitazamo yao ni finyu".Kuparanganyika kwao kutawajenga zaidi.Wakati mwingine ni vzuri kuonyesha Hisia zako hata kama zitawaudhi wengine.Tofauti Ccm wanaminya fikra za wabunge wao!
 
Tunahitaji katiba mpya hata kwa maandamano ya nchi nzima. Hivi, tangu 1995 wimbo ni katiba mpya katiba mpya katiba mpya. Nadhani badala ya Operesheni Sangala, ianzishe 'Oparesheni Katiba Mpya'. Hili ni kwa maslahi ya taifa. Hakuna longolongo hapa!
 
Mwanakijiji mimi naona hoja yako kwa pande mbili.

2. Au mtego


Nini kimefanyika?

Ili kupata legitimacy ya kuanza mabadiliko ya KATIBA, lazima uombe yule mwenye madaraka (government) kujadili mustakabali wa matatizo haya yote bila kujali itikadi yeyote na kuweka maslahi ya Taifa mbele ili wakikataa CHADEMA watakuwa na cha kuwaambia wananchi.

Nini kinafanyika sasahivi?

Nionavyo mimi CHADEMA wanajibu maswali ambayo wataulizwa hapo baadaye.Pasipo shaka wamefikiria mbali kuliona hili to clear all doubts katika njia ya Ukombozi.CCM hilo hawalioni, na hawataliona, kwa sababu hawataki kuliona, na gharama yake itakuwa kubwa asilani.

Nini kitafanyika?


CHADEMA wataenda SUPREME COURT:KWA WANA WA NCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ambapo watapata VERDICT yente kubeba ushindi wa kishindo ambao utatekelezwa rasmi 2015 NA MAHAKAMA hiyo iliyo kubwa kuliko MAHAKAMA zote katika JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

CCM hawaoni mbali.Pengine kosa ambalo watafanya ni kupitisha azimio la kuwaondoa wabunge wa CHADEMA BUNGENI.Kufanya hivyo utakuwa ni msumari wa mwisho katika JENEZA la CCM and we flip OVER a NEW CHAPTER.


Mkuu

Huo ndiyo ukweli wenyewe. Mwanakijiji unasahau hata swala moja ambalo Slaa alishasema. Alisema kuwa watawaonyesha na marafiki wa Tanzania, nchi wahisani nini CCM imekifanya. Sasa linaweza kuja swali "....je, nyie Chadema mliomba mkae nao mlijadili hili swala au mnakurupuka tu kugoma na kuwashitaki...?" Hapo sasa ndiyo yanawekwa mezani maneno ya Katibu Mkuu wa CCM yaani Makamba akisema "wao hawatakaa nao katakata. Kwa maana nyingine, wanataka katiba na utaratibu huu wa Uchaguzi unaowapa wao mwanya wa kuiba, uendelee milele na milele kwa jina la NEC.

CCM kwa kukataa kwao, wanazidi kujimwagia mafuta na mara Slaa/Chadema akija na riport ya Uchaguzi na kuipeleka kwa Wananchi na Nchi wadhamini, basi watakuwa na wakati mgumu sana. Wakifika nje, wataulizwa maswali magumu sana na nina imani wengi wataanza kuogopa kwenda na hata wakienda, basi watajificha na si kutanua na kujionyesha kama zamani.
 
Makamba can go to hell pamoja na Mkwere wake,wapiganaji wa chadema hawataomba msamaha na hawatafukuzwa bungeni kwa kutumia haki yao ya msingi.Mkwere ni raisi na atabaki kuwa raisi lakini jinsi gani kawa raisi ndio wapiganaji hawakubaliani.
 
Heshima mkuu, mada nzuri, ila hapa vp? wawaombe huruma wabunge wa CCM..? Aisee mkuu umenichoma moyo, CDM hawawezi kurudi nyuma CCM wakikataa maongezi shauri yao we have given them a chance at least, kitakachofuata ni kujinadi kwa wananchi, hadi kieleweke mkuu, tupo weeeeeeeeeeeeeengi we need change, makamba, chili ni bomu, hawajui hata leo ni lini, these are old folks, mkuu usikate tamaa, tupo pamoja kanyaga twende, keep ur spirit high

hata wakikataa kukaa na cdm, wananchi tutapigania katiba mpya hata kama ni uhai wangu, kwa manufaa ya ndugu zangu na watoto wao nipo radhi kuingia msituni. tunaoelewa siasa za tz ni kwamba ccm haitakubali kirahisi kwani watakapofanya hivyo ndipo chama kitakufa rasmi kwani kitapoteza nguvu za dola kilichokuwa kinategemea miaka mingi hadi sasa
 
Back
Top Bottom