Makamba akataa CCM kukutana na Chadema

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
0
SIKU moja baada ya Chadema kusema ipo tayari kuketi meza moja na serikali, chama tawala au taasisi nyingine yoyote kwa ajili ya mazungumzo, katibu wa CCM, Yusuf Makamba amesema chama hicho hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema juzi kuwa wako tayari kukaa meza moja na serikali au wadau hao ili kujadiliana nao kuhusu msimamo wao wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, madai ambayo yameimarisha hoja ya kuundwa kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Hata hivyo, Mbowe aliweka bayana kuwa mazungumzo hayo yasiwe ya kuweka mbele maslahi ya kisiasa na wala yasijikite kwenye kauli zinazotolewa na Makamba na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati na badala yake yaweke maslahi ya taifa mbele.

Lakini jana Makamba alisema chama chake hakina jambo lolote la kuzungumza na Chadema na kwamba sasa siasa zinahamia bungeni.

Makamba,ambaye huzungumza kwa mifano ya vichekesho na pia kutumia vitabu vitakatifu vya Biblia na Qorani, alianza kunukuu kifungu kitabu cha Methali 18:18 katika Biblia kinachosema: "Kura hukomesha mashindano; hukata maneno ya wakuu.

"Sisi wote tulikwenda kwenye uchaguzi, kura zikapigwa, aliyeshinda anajulikana na walioshindwa wanajulikana, sasa sisi tukutane na Chadema tuzungumze nini? Wao watafute watu wengine wa kuzungumza nao si CCM."

Kwa mujibu wa Makamba, kwa sasa siasa zinahamia bungeni na kwamba endapo Chadema wanataka siasa za nje ya Bunge, wasubiri tena mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.

"Tutakutana bungeni kwenye kujadili sera, kwa sasa sisi tunaunda serikali," alisema Makamba ambaye katika Bunge la Tisa alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais.

Naye mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kukuza demokrasia nchini inayoitwa Agenda Participation 2000, Moses Kulaba alipongeza uamuzi wa Chadema, lakini akaonyesha wasiwasi kama serikali itakuwa tayari kukaa na chama hicho.

"Ni jambo jema kwa Chadema kukubali maridhiano, lakini serikali itakuwa tayari kuzungumzia mambo haya," alisema Kulaba.

Kulaba alisema mapambano yaliyoanzishwa na Chadema yanatakiwa yawe chachu ya kudai mabadiliko ya katiba pamoja na tume huru ya Uchaguzi baada ya hii iliyopo kulalamikiwa tangu uchaguzi unaoshirikisha vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1995.

"Kilio cha kudai hivi vitu kilianza tangu mwaka 2000, sasa inatakiwa Chadema iwe chachu ya mabadiliko hayo. Zanzibar wamefanya mabadiliko ya katiba; uchaguzi umeenda vizuri hakuna malalamiko kwanini ishindikane Tanzania Bara," alihoji Kulaba.

"Tume ya Uchaguzi ni chombo muhimu sana, lakini pamoja na malalamiko ya miaka yote, kutoka mwaka 1995 mpaka leo, (Jaji Lewis) Makame amekuwa mwenyekiti wa tume hiyo," alisema Kulaba.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ally, alisema bado Chadema haijaweka bayana madai yao ili wananchi waweze kuwaelewa. Bashiru alisema baada ya waangalizi wa uchaguzi kutoa ripoti zao kamili, itakuwa ni wakati muafaka wa kujua kilichotokea katika uchaguzi huo.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,979
2,000
CHADEMA wakomae na kudai marekebisho ya KATIBA, kwa kuendelea kutokutambua matokeo ya urais.
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,531
2,000
Rais huyu hatambuliki hata iweje..Mwizi wa kura why CHADEMA mnataka kukaa na wezi meza moja....
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo.

Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.
 
Wameiba Kura

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
390

Heshima mkuu, mada nzuri, ila hapa vp? wawaombe huruma wabunge wa CCM..? Aisee mkuu umenichoma moyo, CDM hawawezi kurudi nyuma CCM wakikataa maongezi shauri yao we have given them a chance at least, kitakachofuata ni kujinadi kwa wananchi, hadi kieleweke mkuu, tupo weeeeeeeeeeeeeengi we need change, makamba, chili ni bomu, hawajui hata leo ni lini, these are old folks, mkuu usikate tamaa, tupo pamoja kanyaga twende, keep ur spirit high
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
10,692
2,000
Nimeitumikia CCM kwa uadilifu sana wakati wa ujana wangu wote tangu tunaianzisha mwaka 1977 hadi mwaka 1989 ilipogeuka kuwa jeuri dhidi ya watu na kutufungia chuo chetu cha UDSM ndipo nilipotupilia mbali kadi ya CCM na kujiunga na NCCR ambayo baadaye ikajajulikana kama NCCR-Mageuzi. Ninashangaa sana kuwa tangu niondoke CCM imegeuka kuwa genge la wahuni na wezi wa haki za wananchi likiongzwa na viazi kama Makamba na Kikwete. Kwao wao sera ni kumwaga pesa nyingi sana wakati wa kampeini, kununua vizawadi vya kipumbavu kwa wapiga kura, na kuahidi kuleta Mwezi duniani. Maisha ya watanzania wa kawaida na future ya nchi hii siyo jambo la muhimu kwao. Sijamwelewa Msekwa aliyekuwa Katibu mtendaji wa kwanza CCM na mwandishi wa katiba CCM anaishi vipi kwenye kundi la namna hii.
 
Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Mar 18, 2010
593
0
.................. Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ally, alisema bado Chadema haijaweka bayana madai yao ili wananchi waweze kuwaelewa. Bashiru alisema baada ya waangalizi wa uchaguzi kutoa ripoti zao kamili, itakuwa ni wakati muafaka wa kujua kilichotokea katika uchaguzi huo.

huyu mhadhiri wa UDSM na bado hajaelewa madai ya chadema ni nini! hali ikoje kwa wanachi wa kawaida? ni kweli huyu jamaa hajaelewa madai ya chadema au kuna kamchezo anachezeshwa hapo? watch out. hii ni politiki per se!
 
Mtu Mmoja

JF-Expert Member
Mar 18, 2010
593
0
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo. Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.

chadema ni wa kuhurumiwa sana, kwanza wameishagawanyika na hivyo hawawezi tena kupigana vita hii, muda si mrefu itabaki vita ya mbowe na slaa tu, pale wengine wote wakishaingizwa kwenye payrol ya waheshimiwa
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
Heshima mkuu, mada nzuri, ila hapa vp? wawaombe huruma wabunge wa CCM..? Aisee mkuu umenichoma moyo, CDM hawawezi kurudi nyuma CCM wakikataa maongezi shauri yao we have given them a chance at least, kitakachofuata ni kujinadi kwa wananchi, hadi kieleweke mkuu, tupo weeeeeeeeeeeeeengi we need change, makamba, chili ni bomu, hawajui hata leo ni lini, these are old folks, mkuu usikate tamaa, tupo pamoja kanyaga twende, keep ur spirit high

Nimesema hivyo ili nieleweke vizuri; kama Mwenyekiti na Katibu wake hawajui walitoka Bungeni kwa ajili gani huku Naibu na Kaimu nao wakiwa na upande wao nani awape umakini wa kuwasikiliza. Wakienda kwa wananchi watawaambia nini? Aidha waombe radhi kwa taifa kwa kuwafanya watu waamini walitoka kwa sababu walikuwa hawatambui jinsi Tume ilivyotangaza ushindi wa Rais na kutoka hapo ushindi wa Kikwete mwenyewe. Nadhani wanashindwa kujenga hoja yenye mantiki ambayo ni more balanced. Inashangaza wanashindwa kuarticulate a logical position na sasa wanachanganyana wenyewe.
 
Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
0
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo. Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.
Nafikiri MKJJ hujawaelewa Chadema hapa wanataka nini unaweza kuona kama weakness lakini is a planned mission.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,819
0
ccm haiwezi kukaa na chadema kwa sababu ccm ina upper hand kwenye situation hii. Kukaa nao pamoja kutamaanisha vilio vya chadema vina mantiki wakati Chadema yenyewe haijui inataka nini au ina msimamo gani.

Slaa kasema jengine, Mbowe jengine, Zitto jengine na kujionyesha kama chama hakina maono ya aina moja.

Kwa nini ccm izungumze na chama kisichojielewa?

Hapa ni kwenda bungeni na kutoa miswada huku wakiwa lobby wabunge wa upinzani na ccm kuwaunga mkono or else hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya katiba
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
Gaijin, katika position ya weakness waliyo nayo Chadema sasa watakachofanyiwa ni Hoja itatolewa na mbunge wa CCM kutaka Chadema waombe msamaha ama sivyo wafukuzwe Bungeni.. guess what will happen?
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,819
0
Gaijin, katika position ya weakness waliyo nayo Chadema sasa watakachofanyiwa ni Hoja itatolewa na mbunge wa CCM kutaka Chadema waombe msamaha ama sivyo wafukuzwe Bungeni.. guess what will happen?

kwa propaganda machine za ccm zilivyomakini kuharibu image ya vyama pinzani hilo linaweza kutokea, lakini kwani katiba inasemaje? mtu anaweza kufukuzwa Bungeni kwa kuondoka rais akihutubia?
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,663
2,000
Mimi nilisema kuwa Makamba kama katibu mkuu wa CCM yuko effective sana watu wakanibishia......
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,512
2,000
Wabunge wa CHADEMA sio WAMOJA. Baadhi, hasa wale waliochaguliwa Majimboni wanadhani ni jitihada zao binafsi zimewafikisha pale. Hawauoni MCHANGO wa Dr Slaa wala CHAMA chao. Mtu kama Zitto anadhani anakubalika yeye kama yeye tena sio KIGOMA tu bali TANZANIA nzima. Ni vigumu kuwa na maamuzi ya PAMOJA, msimamo wa pamoja na AGENDA ya pamoja kwa lolote katika hali kama hii. Isingekuwa tatizo la KATIBA yetu ya JMT, Zitto na wengine kama yeye walifaa zaidi kuwa Independent Candidates. Hili litawafanya akina JK na manyang'au wengine wa CCM wawagawe na kuwatumia watakavyo.
Makamba ana haki ya kutamba hivo anavyotaka.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,045
2,000
kwa propaganda machine za ccm zilivyomakini kuharibu image ya vyama pinzani hilo linaweza kutokea, lakini kwani katiba inasemaje? mtu anaweza kufukuzwa Bungeni kwa kuondoka rais akihutubia?

haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
26,038
2,000
Mimi sioni mantiki yoyote kwa Chadema kukaa na CCM , ili iweje? CCM na NEC ndiyo wameengiza nchi kwenye mtafaruku kwa kuchakachua kura, sasa utazungumzaje na mhalifu? Kwa vile sheria hairuhusu kwenda mahakamani, njia pekee ni kupeleka mashitaka kwa wananchi ambao kura zao ndiyo zimechakachuliwa na hii mijambazi, na kwa kuanzia Chadema waweke hadharani takwimu sahihi za kura zilizopigwa, vinginevyo tutakuwa tunapotezeana muda kujadili wizi huo wa kura bila kuwa na takwimu, Chadema wakishindwa kufanya hilo bora watulie kwani wanavyozidi kulalama wanatutia uchungu sisi ambao hatuna majukwaa ya kusemea.
 
Gaijin

JF-Expert Member
Aug 21, 2007
11,819
0
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!

Kama kuna fursa kama hii sitarajii kuona Makamba anaacha kuitumia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom