Makamanda wapo pamoja kunani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamanda wapo pamoja kunani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Mar 4, 2012.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Nimesikia kwa mbali bahati bukuku akitumbuiza ndani ya kanisa la kkkt usharika wa Kiboriloni na nilipokwenda kuchungulia kwa ndani namuona kamanda mh Ndesa(MB), Owenya(MB), Lucy(MB) na comrade Mandara. Ndio najiuliza jimbo la Arumeru mashariki limefika hadi huku? Ama ni usharika wao mahala wanapoabudu kwa pamoja? Naomba Chadema mtoe ufafanuzi kwa uwepo wa hawa makamanda pamoja tafadhali.
  .
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Duh..!
  Madam uliwaona wahusika ulishindwa nini kuwauliza ili wakupe majibu mujarabu?
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Siasa mpaka kanisani...congrats CDM, kweli siasa mnaiweza!
   
 4. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  .
  Wamekaa siti za mbele karibu na madhabahu. Namna ya kuwafikia kwa sasa kuwauliza sii rahisi. Labda niahirishe sarafi yangu ili baadae nipate kuwauliza.
  .
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,011
  Trophy Points: 280
  Basi nimeishafahamu ni kwa nini makamanda wamejikusanya hapa katika usharika wa Kiboriloni. Kuna kwaya ya wokovu ndio wanaozindua mkanda wao wa kwaya. Kwa hiyo walikuwa wamealikwa kama wageni rasmi. Ila sijui hii imekaaje wana Jamvi? Mheshimiwa Ndesa-pesa alikuwa akidadavua kuhusu pesa ya mfuko wa CDF na ni kiasi gani zimeingia na zimekwenda wapi na kufanya nini. Lucy(mb) nae alichukua mike na kufafanua kwamba wao kama wabunge wa viti maalumu mfuko huo hauwahusu na mkiwaona wanatoa michango yao katika shughuli za kimaendeleo ni kutoka katika mishahara yao. Saafi sana, ila nilichotaka tusaidiane ni kutaka kujua, je kanisa ama msikiti ni jukwaa sahihi la kutolea michanganuo ya kisiasa?
  .
  Ukanda wa kaskazini mwa Tanzania linapokuja suala la mambo ya maendeleo hawana utani kabisa. Wanashikana wote kama siafu kuhakikisha gurudumu linasonga mbele. Nilipodadisi madhumuni ya kwaya ya wokovu kuitisha harambee kwa kuchangisha, nimeelezwa kuwa kanisa lina kituo kinachowalea watu walemavu na wengi wao ni wale wenye mtindio wa ubongo. Hivyo walikuwa wanatafuta pesa kwa ajili ya mahitaji ya watu waliopo kituoni. Katika harambee hiyo iliyoongozwa na mh, Ndesa-pesa zimepatikana zaidi ya Tsh. 30Millioni, Ndesamburo mwenyewe akichangia Sh. 8 milioni, mke wake 5 milioni kwa kuinunua saa ya Ndesa. Mh Lucy 1. Milioni na mh G. Owenya laki tano.
  .
   
Loading...