Makamanda wa CHADEMA ndani ya Songea mda huu

skendo

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
212
101
Makamanda wapo ndani ya Songea wakitoa elimu juu ya katiba mpya na uraia,kikao kitaanza mda wowote toka sasa.nitaendelea kuwa julisha yanayo jili watu ni wengitu hapa ukumbini. nikipata chance nitarusha picha
 
Viongozi watakua wameingia mda c mrefu nitawajurisha watakao kuwepo ila kwa sasa MC katoa dk5 watu wakanunue pen na karatasi kwajili ya kumbukumbu ya yale yatakayo kua yakifundishwa.
 
safi sana CDM,elimu kwanza na hatimae kupitia hio elimu watu watakuwa tayari kwa ukombozi wa taifa letu!!! Big up chadema.
 
Good work...mmoja wao kati ya hao viongozi nadhani atakuwepo mdada wangu Regia..well done!!
 
Yupo Regia Mtema na katibu wa Cdm jimbo la kawe Mfinange.mkutano umeanza na sasa mfinange alikua anasoma barua toka kwa katibu mkuu wa chadema ambayo inaelekeza kila mwnanchi,kila kata na maeneo yote ujumbe wa barua iyo ufike
 
R.mtema amenza mada.
1.kama chama wameona bora waanze kutoa elimu kwa mikoa yote ili watu wajue kwa nini cdm wanapinga mchakato mzima huu wa katiba
2.anafundisha nini maana ya katiba
Kwasasa amesitisha kdogo kuna zoezi la kugawa karatasi ili kila mtu awe anaandika yale yanaojili da!wakuu jamaa wamedhamilia
 
R.mtema
1.katiba ndio sheria mama nakupitia katiba tunapata mihimili yote ya dola.mahakama,bunge
2.ukiwa na katiba mbovu kimsingi utakua na bunge bovu,mahakama mbovu
3.historia ya kudai katiba ilianza toka zamani ila serikali imekua ikiweka viraka badala ya kutengeneza mpya
4.anazungumzia pia mapendekezo ya tume ya nyalali
5.serikali inaogopa sana kuhusu katiba maana wanajua ikilekebishwa itawatoa madarakani
 
1. Cdm wanataka wananchi wapewe haki kumiliki ardhi
2.katiba mpya ili serikali itoe huduma bora kwa wananchi.mfn vyuoni,mahospitalini
 
Hongera chadema kwa kuanza kutekeleza mara moja maazimio ya kuelimisha umma.Chama makini kinatakiwa kufanyia kazi maazimio kwa vitendo kama mnavyofanya,Dalili njema hizi
 
R.mtema
1.cdm wanapinga Rais kuchagua tume nzima ya mchakato huu
2.wanapendekeza nafasi izo zigombewe kulingana na vigezo vitakavyo wekwa
3.wananchi hawajashirikishwa ipasavyo
4.cdm wanapinga bunge maalumu la katiba namna ya linavyopaswa kuwa
5.zanzibar wako km milioni 1 sisi tupo km milioni arobaini iweje tuwe na uwakilishi sawa katika bunge la katiba
6.ukipiga hesabu za uwakilishi huo ccm itatoa asilimia 52 ukijumlisha na asilimia za mke Cuf tayali katiba itakua ni ya ccm na Cuf
 
Duh, Kamanda Regia ameipasua hivyo CUF laivu? Au umeongeza wewe kwa msisitizo?:lol:
 
Back
Top Bottom