RC MAKALLA AWATAKA WANANCHI KULIPA FEDHA KUEPUKA UTEKELEZAJI WA HUKUMU YA MAHAKAMA ARDHI KIWANDA CHA WAZO.
- Asema
serikali haitoendelea kuwatetea Watakaokaidi kulipa Na hukumu ya mahakama Kuu itatekelezwa.
- Awahakikishia
Usalama wote waliolipa.
- Awataka
Wavamizi wapya kuondoka.
- Awatahadharisha
wanaopotoshwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
Mhe. Amos Makalla amesema Serikali haitojihusisha kwa namna yoyote kuwasaidia
Wakazi wa Chasimba, Cha Tembo na Cha Chui waliovamia eneo la Kiwanda Cha Wazo
Watakaokaidi kulipa fidia kwa mujibu wa makubaliano waliyowekeana na badala yake
waliolipa watapata uhalali wa kuishi kwenye eneo hilo na
waliokaidi kulipa Wataondolewa kwa mujibu wa Sheria.
RC Makalla ametoa msimamo wakati
Mkutano wa hadha na wavamizi hao ambapo
kwa Mujibu Wa sheria Kiwanda cha Wazo
kilishinda kesi na kupatiwa
amri ya kuwaondoa wavamizi wote lakini Kutokana na
wingi wa Wavamizi hao na uendelezaji wa Ardhi walioufanya
Serikali ilitumia busara kukutanisha
Pande zote mbili na kufikia muafaka kulipa fidia ya
Tsh 6,419 kwa kila Square meter moja lakini
baadhi wamelipa na wengine kukaidi.
Kutokana na hilo
RC Makalla amefika kwenye eneo hilo kwa lengo la
kuwakumbusha kutekeleza wajibu wa kulipa kwa mujibu wa makubaliano ili
kujihakikishia kubaki kwenye eneo hilo kihalali.
Aidha
RC Makalla amesema mpaka Sasa zaidi ya
wananchi 1,500 wamefanya miamala ya
malipo lakini wengine wamekaidi ambapo ametoa wito kwa Wananchi hao
kujiepusha na wanasiasa wanaotoa
kauli za kisiasa kuhamasisha wasilipe kwakuwa
muda ukiotolewa ukimalizika wataondolewa.
Hata hivyo
RC Makalla amewaelekeza
Wavamizi Wapya kuanza kuondoka kwenye eneo hilo hao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa Nguvu.
Pamoja na hayo
RC Makalla amepokea
kero mbalimbali za Wananchi wa eneo hilo ikiwemo
ukosefu wa Shule ya Msingi ya kata ya Wazo ambapo ametoa Siku 10 kupatiwa
taarifa ya eneo lililoteuliwa kwa Ujenzi Kama linakidhi vigezo na Kama litaoneka kukidhia
ameahidi kusimama kidete kuhakikisha shule inajengwa na
Wanafunzi wanapata elimu Bora.