Makalla: Serikali haitojihusisha kwa namna yoyote kuwasaidia Wananchi waliovamia eneo la Kiwanda cha Wazo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
1,116
2,000
RC MAKALLA AWATAKA WANANCHI KULIPA FEDHA KUEPUKA UTEKELEZAJI WA HUKUMU YA MAHAKAMA ARDHI KIWANDA CHA WAZO.

- Asema serikali haitoendelea kuwatetea Watakaokaidi kulipa Na hukumu ya mahakama Kuu itatekelezwa.

- Awahakikishia Usalama wote waliolipa.

- Awataka Wavamizi wapya kuondoka.

- Awatahadharisha wanaopotoshwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Serikali haitojihusisha kwa namna yoyote kuwasaidia Wakazi wa Chasimba, Cha Tembo na Cha Chui waliovamia eneo la Kiwanda Cha Wazo Watakaokaidi kulipa fidia kwa mujibu wa makubaliano waliyowekeana na badala yake waliolipa watapata uhalali wa kuishi kwenye eneo hilo na waliokaidi kulipa Wataondolewa kwa mujibu wa Sheria.

RC Makalla ametoa msimamo wakati Mkutano wa hadha na wavamizi hao ambapo kwa Mujibu Wa sheria Kiwanda cha Wazo kilishinda kesi na kupatiwa amri ya kuwaondoa wavamizi wote lakini Kutokana na wingi wa Wavamizi hao na uendelezaji wa Ardhi walioufanya Serikali ilitumia busara kukutanisha Pande zote mbili na kufikia muafaka kulipa fidia ya Tsh 6,419 kwa kila Square meter moja lakini baadhi wamelipa na wengine kukaidi.

Kutokana na hilo RC Makalla amefika kwenye eneo hilo kwa lengo la kuwakumbusha kutekeleza wajibu wa kulipa kwa mujibu wa makubaliano ili kujihakikishia kubaki kwenye eneo hilo kihalali.

Aidha RC Makalla amesema mpaka Sasa zaidi ya wananchi 1,500 wamefanya miamala ya malipo lakini wengine wamekaidi ambapo ametoa wito kwa Wananchi hao kujiepusha na wanasiasa wanaotoa kauli za kisiasa kuhamasisha wasilipe kwakuwa muda ukiotolewa ukimalizika wataondolewa.

Hata hivyo RC Makalla amewaelekeza Wavamizi Wapya kuanza kuondoka kwenye eneo hilo hao wenyewe kabla ya kuondolewa kwa Nguvu.

Pamoja na hayo RC Makalla amepokea kero mbalimbali za Wananchi wa eneo hilo ikiwemo ukosefu wa Shule ya Msingi ya kata ya Wazo ambapo ametoa Siku 10 kupatiwa taarifa ya eneo lililoteuliwa kwa Ujenzi Kama linakidhi vigezo na Kama litaoneka kukidhia ameahidi kusimama kidete kuhakikisha shule inajengwa na Wanafunzi wanapata elimu Bora.

 

Plan Paris

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,950
2,000
Magufuli alikuwa sahihi kumtumbua huyu bwana, kuna wakati Magufuli nilikuwa namuona mtu anayekurupuka kuwafukuza watu kazi.

Mfano huyu Makalla na mwenzake Ndugulile walifukuzwa kazi tukajua wameonewa.

Baada ya kurudishwa madarakani huyu makalla kawa bomoa bomoa, ndugulile akageuka mpandisha bei ya mabando,

Bado yule kipenzi cha wengi naye atatuletea mgao wa umeme sababu alowaweka ni rafiki zake hawezi kuwakemea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom