Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,305
- 9,734
Ndugu zangu Watanzania,
Nimefurahishwa na Habari niliyoisoma katika Gazeti la Mwananchi,likielezea utaratibu ambao mkuu wa mkoa wa Mwanza mh Amos Makalla amekuja nao na kuuzindua katika kuwafikia wananchi wenye kero na changamoto mbalimbali kwa jina la Ongea Live na mkuu wa Mkoa. Ambapo katika wazo hilo ni kuwa mh mkuu wa mkoa Anatoka ofisini na kwenda kuzungumza na wananchi kwa kuwasikiliza kero zao wilayani huko kutoka ngazi ya mkoa na kuzitatua kwa kutoa majibu. huku akiwataka wakuu wake wa wilaya kufika hadi ngazi ya kata.
Kwa utaratibu huu ni kuwa mkuu wa mkoa kwa kushirikiana na wakuu wake wa wilaya wanakwenda kuwafikia wananchi wenye kero mbalimbali hadi ngazi za mitaa,hali ambayo itapunguza na kuondoa changamoto nakero sugu za wananchi ambao wamekuwa wakihangaika na kuhangaishwa na baadhi ya watumishi wa umma ambao wanakuwa siyo wasikivu kwa wananchi,maana hapa ni lazima RC ama DC atoe maelekezo ya utekelezaji wa chochote atakachokibaini.
Utaratibu huu unakwenda kupunguza hata mabango yanayojitokeza wakati wa ziara za viongozi wetu wakuu yaani Rais ,makamu wa Rais pamoja na Waziri Mkuu. Kwa kuwa kero nyingi za wananchi zitakuwa zinamalizwa na ma RC na DC na zile zilizo inje ya uwezo wao watakuwa wanatafuta namna yakuwasiliana na ngazi za juu ikiwepo wizara ili kupata ufumbuzi.
Utaratibu huu ukifanywa na wakuu wa mikoa na wilaya nchi nzima kwa hakika italeta matumaini makubwa sana na kupunguza kero mbalimbali za wananchi. itaondoa adha na machungu ya watanzania kuporwa haki zao,kuonewa,kutosikilizwa na baadhi ya watumishi na kukosa mahali pa kukimbilia, Italeta Tabasamu kwa wajane,yatima na wazee wanaokuwa wameonewa au kunyanyaswa na wenye nguvu na itawasaidia wanyonge kupata haki zao.
Rai yangu na ushauri wangu kwa mh Amos Makalla na wengine pia Ni kuwa katika utaratibu huu mzuri ahakikishe kuwa anafuatilia utekelezaji wa maagizo anayokuwa ameyatoa pindi anapopokea kero ya mwananchi, kuhakikisha kuwa kama mwananchi anatakiwa kupata haki yake na akatoa maagizo ya kushughulikia kero hiyo ,basi awe na utaratibu wa kuhakikisha kuwa anapewa mrejesho wa kimaandishi na kinyaraka juu ya utekelezaji wa maagizo yake. Ili wananchi wapate haki. Kwa kuwa kuna baadhi ya watumishi anaweza akapewa maagizo ya utekelezaji halafu akafanya upuuziaji wa maelekezo ,hivyo ni vyema kwa mkuu wa mkoa na wilaya kuagiza kupewa mrejesho wa kimaandishi wa namna maelekezo na maagizo yake yalivyo tekelezwa.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge.
Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.