Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,754
- 2,859
Chama cha Mapinduzi CCM kimesema hakuna chama chochote ambacho kina mamlaka ya kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu na siyo matakwa ya chama hicho kufanya uchaguzi bali wanafuata kanuni na sheria za katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka uchaguzi mkuu kufanyika mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ambaye yupo ziara ya kikazi mkoani Morogoro na kuwataka wananchi wajiandae kwa uchaguzi mkuu.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga ametoa rai kwa wananachi wa mkoa wa huo kujiepusha na vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi mkuu .