Makali ya umeme, chanzo cha milipuko ya makombora Gonga la Mboto

Msandawe Halisi

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
647
350
Habari za kiintelejesia nilizo zipata juu ya chanzo cha milipuko ya makombora ni umeme. Kwa kawaida eneo hilo la maghala ya jeshi, alitakiwa kuzimwa viyoyozi kabisa.


Cha kustajabisha, inaonekana makambi ya jeshi yetu ayana masomo ya safety au awazingatii.



Umeme ni janga la taifa kuliko hata Ukimwi. Uzalishaji umepungua, ajira za watu zimepungua. Miaka 50 ya inchi huru. Umeme bado aujapata mwarubaini. Mikataba mibovu.



Tunaitaji mabadiliko, tunaitaji wachapa kazi wenye kujali maslai ya Taifa na wanaichi mbele. Napenda siku moja kuwa na jivunia utanzania wangu.



Kwa taharifa yako tu, wanajeshi kibao wamepoteza uhai. Habari zao ni siri kubwa kama mikataba ya Ufisadi.
 
Hapa kuna ukweli "fulani" - Does the END justify the MEANS? or they are INSEPARABLE?
 
Mbagala tulijifunza nini, nikiangalia tu mandhari ya kambi, na uhakika hata na maghala yalivyokaa. Kiwango duni sana.Ripoti ya tume ni siri, haya hayatarudia tena na sasa yamerudia tuwaeleweje. Hapa naona kuna mipango kabambe juu ya hili, ipo siku litafichika. Tuwe wafuatiliji wa mambo ya nchi yetu na uozo wa viongozi wetu, tutafakari na tuchukue hatua, na moja lingepiga ikulu mwitiko wao ungekuwaje?. POLENI SANA WAHANGA
 
Au Tanzania imekuwa dampo la silaha chakavu. Wachina wapo kwenye kambi zetu, nawasiwasi.
 
Dont run for that cheap conclusion.

Mie sikubaliani kwamba tatizo ni umeme maana kama hayo maghala yanajulikana kwamba lazima kuwe na viyoyozi kupoza joto kwa nini hakuna majenereta kwa ajili ya imejensi??
Umeme ungekuwepo wangesema hitilafu ya umeme.

Gharama ya majenereta inalingana na hasara (mali na watu) iliyopatikana? Jenereta la dola $50,000 linagharimu mabilioni sasa in terms of fidia ya maisha na mali, pamoja na hasara inayoambatana na ammunition iliyoteketea.
Mbona kuna jenereta kuhahkikisha kuna umeme muda wote kwa Mkuu wa majeshi??

Kwa nini usifikirie kwamba kuna kundi la watu wanauza zana za kivita kwa waasi nchi jirani then wanalipua stock kidogo iliyobaki kufuta ushahidi??.
Kama ni makombora yaliyopitwa na wakati kwa nini serikali haija-contract wataalam wa kuyateketeza kama walivyofanya kwa kampuni ya Ujerumani kuteketeza masalia ya kemikali zenye sumu kali??

Watanzania tunakubali kirahisi sana kupewa majibu mepesi kwa maswali magumu.
 
Kwa taharifa yako tu, wanajeshi kibao wamepoteza uhai. Habari zao ni siri kubwa kama mikataba ya Ufisadi.
hakika
 
Back
Top Bottom