News Alert: Soko la Vetenari lililoko maeneo ya TAZARA linateketea kwa moto, Chanzo Hitilafu ya umeme

konda msafi

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,631
8,050
Muda huu soko lililopo mbele ya Daraja la TAZARA au Mfugale upande wa kushoto kama unatokea Buguruni linateketea kwa moto.

Jina la soko silikumbuki vizuri, sijui linaitwa Vetinari. Chanzo cha habari ni mimi mwenyewe. Nimepita muda huu nimekuta soko linateketea.

Zima moto na gari lao wapo ila naona wanakodoa macho tu.

====


Screenshot_20220530-074137.png


Soko la Vetenari lililopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam linawaka moto.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Zimamoto mkoa wa kizimamoto Temeke Mrakibu Msaidizi Michael Bachubira amesema Hadi sasa Jeshi linaendelea kuuzima moto huo na kudhibiti usisambae maeneo mengine na kwamba wanaendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.

Hii ni mara ya nne kwa masoko jijini Dar kuungua kwa mwaka huu ambapo mwezi Februari soko la Mbagala likiungua, na Soko la Karume kuungua mara mbili, mwezi Januari na Aprili

====

RC MAKALLA: HITILAFU YA UMEME CHANZO CHA KUUNGUA SOKO LA VETERINARY.

- Asema kazi ya kurejebisha Miundombinu iliyoungua itafanyika usiku na mchana.

- Awahakikishia Wafanyabiashara hakuna atakaehamishwa.

- Asisitiza Masoko kuwa na Fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO.

- Aonya tabia ya Mamalishe kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema chanzo Cha Moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ilitokana na Hitilafu ya umeme.

RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko Hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453.

Aidha RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha Miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na Biashara Kama awali ambapo ameahidi hakuna mfanyabiashara atakaeondolewa.

Hata hivyo RC Makalla ametoa pole kwa Wafanyabiashara walioathiriwa na Moto huo na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali yao inaendelea kutatua changamoto hiyo.

Kutokana na matukio ya Moto kujirudia Mara kwa Mara, RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO,Halmashauri kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye Kila soko, Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva huku akisisitiza Masoko kuwa na Ulinzi.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
14,306
12,403
Wafanyabiashara hasa wengi jambo la kukatia bima shughuli zao wanalionaga kama upuuzi fulani hapa UK bima hukatwa kwanza na ndiyo licence hutolewa.

N. B, BIMA ILIVYO YA LAZIMA KWENYE MAGARI NA KWENYE BIASHARA UWEPO ULAZIMA HUO.
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
5,235
8,545
Soko la Vetenari lilioko maeneo ya Tazara linaungua moto mida hii.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Temeke amethibitisha kutokea kwa tukio la moto katika Soko ilo.
20220530_071440.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
28,333
55,277
Ila inachosha kila siku tunashauri, tunatoa mawazo ya jinsi ya kupambana na hili swala lakini ni kama hawana habari.
 

Ndalilo

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
2,589
5,361
Mwalimu alisema, "tuhuma tu inatosha kumtoa mtu kwenye nafasi yake", limewaka la kwanza, likawaka la pili, likajirudia tena, moto ukavuka mipaka, ukawaka mkoani, leo umewaka tena!

Kama wanahisi ni hujuma, nini kimefanyika? Ripoti ni za kweli, zilifanyiwa kazi? Kinyume chake, tutasikia tena Sameer katoa pesa kujenga soko, kisha ndo Machinga Complex effect kazini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

8 Reactions
Reply
Top Bottom