Katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la Mwananchi la leo,kuna habari isemayo "Makaidi ajitolea kunusuru ndoa ya Zitto,CHADEMA". Kwenye habari hiyo inayoandikwa katika kurasa za 1 na 4, Mwenyekiti huyo mwenza wa UKAWA na NLD Emmanuel Makaidi amekaririwa akidai kuwa Zitto alimuomba kumpatanisha na Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe. Makaidi amedai kuwa sasa yu tayari kuanza kazi aliyoombwa na Zitto kwakuwa Mbowe anaingilika na ni mtu makini,safi na muungwana.
Lakini,Zitto alipoulizwa kuhuu hilo alikana na kusema kuwa kama kuna haja ya kufanya hivyo atakaa na Mbowe na kuyamaliza. Pia Zitto amesema kuwa asilazimiswe kuingia UKAWA kwa njia ya CHADEMA tu kwakuwa aweza kuingia UKAWA kupitia CUF,NCCR-Mageuzi au ACT-Tanzania. Alisema "Huyu mzee ni mtu ninayemheshimu sana na juhudi zake ni nzuri,lakini sijawahi kuzungumza naye kuhusu kupatanishwa na chama changu,sisi wenyewe tuna uwezo kukaa wawili na kuyamaliza,jitihada zake kwasasa hazijahitajika"
Baada ya kukana kumuomba Makaidi, Makaidi amesema " amekana huyu Bwana,haa! Tulikutana pale kantini Bungeni,aweza kukutajia namashhidiwaliokuwapo,laini mimi nilikuwa nafuatilia jinsi ykumuingia huyoBwana mkubwa wa CHADEMA na sasa naona inawezekana."
Lengo ni zuri. Lakini mkweli ni nani?
=======================