Makahaba Wagonganisha Ma RPC Dar

Makahaba Wagonganisha Ma RPC Dar

Kwa taarifa yako, ukahaba ni kosa kishria.

Tanzania Penal Code
CHAPTER XV
Ofences Agaist Morality.
146. Any woman who knowningly lives wholly or part of the woman earning of prostitution or who is proved to have, for the purpose of gain, exercised, control, direct or, influence other over the move for engaging in prostitute in such a manner as to show she is aiding, abetting or compelling her prostitution, with any person, is guilt of misdemeanour.


Crytal Clear, Kenyela is right
 
Mkuu asante kwa kutuletea hii sheria. Now the problem is, how do you prove beyond doubt that these ladies were actually exercising prostitution before the court of law? Na je sheria inasemaje kuhusu wateja wa hao wadada? Ili kitendo cha prostitution kikamilike, lazima awepo mwanamke na mwanamme. Je wanaume wanaowanunua hao wadada wao wanakosa au hapana?

Tiba

Hata wateja wa ukahaba ni wavunjifu wa sheruia.
tanzania Penal Code
Chapter XV
Offences Against Morality
145. 1.A any male person -
(a) who knowningly lives wholy or part of earnings on prostitution; or
(b) in any public place persistently solicits or importunes for immoral purposes is guilt of misdemeanour. In the case of the second or subsequent conviction under this section the court may, in addition to any term of imprisonment awarded, sentence the offender to corprol punishment.
(2) Where a male person is proved to live with or to be habitually in the company of prostitute, or is proved to exercised, control, direction or influence over the movement of a prostitute in such manner as to show that he is aiding, abetting or compelling prostitution with any other, or generally, he shall unless satisfy the court contrary be deemed to be knowningly living on prostitution.
 
nimesoma maoni ya watu wengi na nimegundua watu wanachanganya mambo mawili;

- moja ni kama kitendo cha ukahaba ni kosa kisheria na mahakamani atashitakiwa kwa kosa gani?
- pili ushahidi wa mtu kufanya ukahaba ni utata.

kwa hoja ya kwanzai ukweli ni kuwa, ukahaba ni kosa la jinai kwa sheria ya kanuni ya adhabu ambayo baadhi yetu wametuwekea kifungu husika hapa hivyo sitapenda kukinukuu tena. jamabo jingine ni kuwa, sababu kosa tajwa ni jinai hivyo mtuhumiwa atafunguliwa shitaka la kufanya ukahaba.

kwa hoja ya pili kuthibitisha ya kuwa unayemkamata anafanya ukahaba mathalani kumkuta mwanamke amesimama nusu uchi barabarani usiku bila hata ya mwanaume kuwepo? katika hili ni vizuri tukaelewa kuwa polisi wanatakiwa kufanya uchunguzi katika moja ya majukumu yao mengi hivyo ni wajibu wa polisi kuhakikisha katika uchunguzi anaofanya ushahidi wa kutenda kosa unapatikana. kwa sababu hii mwenye jukumu la kouna ushaidi dhidi ya kosa itakuwa ni mahakama na sio polisi.

mtu anaweza kuuliza sasa kwanini umkamate mtu bila ya kuwa na ushaidi? jibu ni kuwa polisi wamepewa malaka ya kumkamata mtu yeyote amabaye anamuhisi kutenda kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jina ya mwaka 1985 na marekebisho yake. kifungu kifuatacho kinahusika moja kwa moja

" 10.-(l) If from the information received or in any other way a police​
officer has reason to suspect the commission of an offence or to appre- hend a breach of the peace, he shall, where necessary, proceed in person to the spot to investigate the facts and circumstances of the case and to take such measures as may be necessary for the discovery and arrest of the offe.nder where the offence is one for which he may arrest without warrant.
 
All in all, kiondo hakupaswa kumkosoa mwenzie vile mbele ya media/jamii, hata kama sheria imekaaje. Lengo lake hasa ni lipi? Kujenga kubomoa, au ndio anawamotivate makahaba kwenda kufungua charge? Na bado ukahaba sio jambo la kubarikiwa, au wana mabiff yao akaona ndio mahali pa kumshusha level mwenzie? Akifanya jambo yeye na mwenzie nae akaja na stail hiyo atafurahi? Alikuwa na njia nyingi tu za kufikisha taarifa bila kuutangazia umma, kama alikuwa na nia njema lakini, otherwise na yeye kachemka.
 
Kwa mujibu wa sheria za makosa ya jinai za Tanzania ni hivi:

Tanzania Penal Code
Chapter XV
Offences Agaist Morality
147. If it is appeal to the magistrate by information on power of oath that there is reason to suspect any house or part of a serch house is used by a woman for the puposes of prostitution, and that any person residing in or frequenting the house is knowningly living wholly or in part of the earnings are of the prostitute, or is exercising, control, direction of influence over the movement of the prostitute, the magistrate may issue a warrant authorising any poloce officer to enter and search the house and to arrest such person.


Hii ndio Great thinking, badala ya utashi. Keep up kutufunza kuwa tunahitaji elimu ya jambo kabla ya kutowa maoni yetu.
 
ukweli ni kuwa kENYELA KACHEMKA SANA TUUU!

Kweli wewe ni Quick Reply. Wakati mwingine uwe unajua maudhui ya jambo linalojadiliwa. Kenyela hajakosea. Kama hakuna sheria ya kuzuia ukahaba, basi Kiondo aonyeshe sheria inayoruhusu!! Haipo. Ukabaha umezuiwa kwenye sheria ya uzururaji. Mwelezeni Kiondo aisome hiyo sheria. Ukahaba ni biashara kongwe kabisa duniani. Kwa nchi kama yetu ni lazima ikemewe hapa na pale, vinginevyo kila kona tutashuhudia watu wakifunuana ving'amuzi hadharani!! Hongera Kenyela.
 
Hii ndio Great thinking, badala ya utashi. Keep up kutufunza kuwa tunahitaji elimu ya jambo kabla ya kutowa maoni yetu.


Nashauri sheria hii iingie pale Mrina Annex, Arusha. Pale ukahaba ni kama kiumbe hai na hewa ya oksijeni. Vikitengana, hakuna uhai.
 
Kamanda wa Temeke anafaidi nini na biashara ya uchangudoa? kwanini anaingilia mambo ambayo siyo yake maana Kinondoni is not Temeke? Anataka amrithi Kamanda Kova? I wonder!!
 
Kwa mujibu wa sheria za makosa ya jinai za Tanzania ni hivi:

Tanzania Penal Code
Chapter XV
Offences Agaist Morality

Offenses against morality? Never knew morality could be legislated!
 
Hawa dada zetu walikuwepo tokea enzi na enzi, watakuwepo mpaka mwisho wa dunia, itumike tu hekima lakini kama ni magereza hilo sio suluhisho kabisa, kwani wateja wao ni akina nani ili wakamatwe wao peke yao!
 
Kwa mujibu wa sheria za makosa ya jinai za Tanzania ni hivi:

Tanzania Penal Code
Chapter XV
Offences Agaist Morality
147. If it is appeal to the magistrate by information on power of oath that there is reason to suspect any house or part of a serch house is used by a woman for the puposes of prostitution, and that any person residing in or frequenting the house is knowningly living wholly or in part of the earnings are of the prostitute, or is exercising, control, direction of influence over the movement of the prostitute, the magistrate may issue a warrant authorising any poloce officer to enter and search the house and to arrest such person.

Kama kweli hii sheria ipo basi guest house na hotel zilizonyingi hapa Tanzania zingefungwa kwani hutumika kwa ukahaba tu. SWALI LANGU. Hao wanaowanunua mbana hamuwakamati? au wao hawatendi makosa. Tuna n jia ndefu kuelekea kutokomeza mfumo dume.

Watu wote mnaona hawa wakina dada wamekosea sana lakini wanaoenda kuwatafuta hao akina dada wakiwemo waheshimiwa sana hamuoni kama wana kosa.

hata kama wanakamatwa kwa uzururaji kwani kuzurura ni usiku tu? mchana je, huwezi zurura
 
Kenyela anafanya mambo kwa sifa akitarajia labda neema ya U-IGP inaweza kumwangukia ila kwa suala la ukahaba ni gumu mno kulithibitisha kisheria. Mathalani Kenyela na kundi lake la ITV wali kwenda Mwananyamala kufanya msako wa makahaba. Pale kwenye vile vyumba walikamata baadhi ya wapangaji wa kike wakiwa peke yao kwenye vyumba. Sasa mahakamani uta thubitisha vipi kuwa wale ni makahaba? Na utawashitaki kwa kosa gani na kwa kipengele kipi cha sheria kilicho vunjwa?

Opersehsni kama hizo zilishafanywa huko nyuma sio kigezo cha kusema kuwa serikali/polisi walikuwa sahihi. Rejea kesi ya kumshitaki Mrema na sungusungu yake. Kila mtu alitii kulinda sungusungu pale jamaa mmoja wa Magomeni (kam sijakosea) alikataa kulinda Mrema aka amrisha akamatwe na kuwekwa lupango. Mahakamni jamaa alimweka Marando kama wakili na mahakama ikatamka jeshi la sungusungu liko kinyume cha sheria hivyo jamaa hakuvunja sheria yoyote

Kiondo yuko sahihi nyakati zimebadilika.Kama tuko serious kupinga ukahaba sheria itungwe , wabunge wengi wanaponea huko (Rejea ripoti ya mama Terry).
unaua mzee wa usafi
 
MAKAMANDA wawili wa polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyela wa Mkoa wa Kinondoni na Kamanda wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, wamekwaruzana na kurushiana maneno yasiyofaa kuhusu namna ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.

Kutofautiana huko kumeibuka baada ya wiki iliyopita, Kamanda Kenyela kufanya operesheni ya kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba, maarufu kama machangudoa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Baada ya Kamanda Kenyela kuendesha operesheni hiyo, Kamanda Kiondo wa Temeke, alinukuliwa na vyombo vya habari jana, akikosoa zoezi hilo na kusema hakuna sheria nchini inayozuia mwanamke kujiuza.
Katika maelezo yake, Kamanda Kiondo alisema, operesheni hiyo ilifanywa kwa kukurupuka na kwamba kamanda huyo hajasomea elimu ya jamii juu ya madanguro.

Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, kama Kamanda Kenyela angekuwa anaielewa vizuri elimu hiyo, kamwe asingedhubutu kuwakamata wanawake hao bali angewapatia elimu na ushauri dhidi ya maradhi wanayoweza kuambukizwa.
Pamoja na hayo, alihoji kuna umuhimu gani wa kuwakamata machangudoa wakati hakuna sheria inayomtaka awafikishe mahakamani badala yake anayetakiwa kushitakiwa ni mtu anayetoa nyumba ili itumike kama danguro.

Naye, Kamanda Kenyela alipozungumza na MTANZANIA jana juu ya kauli za kejeli zilizotolewa na mwenzake huyo, alisema amestushwa na taarifa ya Kamanda Kiondo kwa kuwa amemdhalilisha kupitia vyombo vya habari. “Yaani mwandishi sipati picha kama Kamanda Kiondo ambaye hana miezi sita kwenye nafasi hiyo tangu ateuliwe, anaweza kunidhalilisha juu ya utendaji wangu wa kazi, kwanza inakuwaje azungumzie mambo ya Kinondoni wakati mimi nipo? “Kama alijua nimekosea, alipaswa kunipigia simu kwanza tushauriane kabla ya kusema kwenye vyombo vya habari au angenisema kwa wakubwa wetu ambao wangeniita na kunishauri ili nisitishe operesheni hiyo, kama kweli ninakwenda kinyume.

“Amenidhalilisha sana na unajua ni vigumu kwa kamanda kama yule kutoka kwenye himaya yake na kuzungumzia himaya ya kamanda mwingine wakati mhusika yupo. “Kibaya zaidi anasema eti mimi sina elimu ya jamii juu ya madanguro, lakini binafsi siwezi kuona vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani au usumbufu kwa raia wengine, halafu nikakaa kimya, sitaacha kuchukua hatua.

“Ninachoweza kumwambia Kamanda Kiondo ni kwamba, sina ugomvi naye na pia sitaki malumbano naye, kazi ya kudhibiti uhalifu haihitaji mpango mmoja lazima tutumie njia mbadala kuhakikisha tunatimiza majukumu yetu ya kulinda raia na mali zao, nafikiri suala hilo linazungumzika tuache litapata suluhisho,” alisema Kamanda Kenyela akionyesha kukerwa na kauli za Kamanda Kiondo.


Source: Mtanzania, 14th Jan 2013


My Opinion:
Kamanda Kenyela yupo sahihi, sheria ipo inayokataza vitendo vya ukahaba - http://www.un.org/Depts/los/LEGISLATIONANDTREATIES/PDFFILES/TZA_penal_code.pdf

Hivi Dar es salaam kuna mikoa mingapi? Ilala pia ni mkoa? ni lini Kinondoni au Temeke imekuwa mikoa?
 
Safi sana waache wakabane wenyewe ili wapunguze kuwaua raia wasio na hatia. Lakini huyu Kenyela badala ya kudhibiti majambazi anawasumbua wadada wanaojitafutia ajira baada ya serikali kushindwa kuwaajiri? Angalia Vyuo vikuu wanafunzi wa kike wanajiuza wapate ada kwa kuwa bodi ya mikopo haiwapi fedha kwa wakati au haiwapi kabisa. Kwanza Dada poa hao wana wateja wengi tu wakubwa na hawana tatizo labda wachache wanaojihusisha na wizi. Haya Kenyela umewakamata hao wote utawaajiri wewe au unataka wafanye nini? Mbona wanaokeketa wanatafutiwa kazi nyingine sembuse hao wanaotumia miili yao bila kumdhuru Mtu?
 
Back
Top Bottom