Makahaba Wagonganisha Ma RPC Dar

Makahaba Wagonganisha Ma RPC Dar

Engelbert Kiondo, bila shaka umesoma sheria na katika sheria imeainisha kazi halali na kazi isiyo halali. Tunaposema kazi halali inayompa mtu kipato ukahaba si kazi halali japo unampa mtu kipato lakini si kazi halali, Afande kazi hii wanawake hawa wanaifanya si kwa lengo la ora kwa Kila Mtanzania" tuliyoahidiwa lakini nadhani hata muasisi wa "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" hawezi kuungana na wewe kuhusu hili. Tusiendelee kulea maovu kiasi hiki. Nyie Polisi mmekuwa mkiwaua raia je hili liko kwenye katiba? Najua utasema Polisi huwa wanajihami, je raia wakijihami mbona mnasema haiko katika katiba. Samahani ingekuwa Ndugu yako wa karibu kabisa katika zoezi lenu la kuwaondoa machangudoa ukakutana na ndugu yako wa damu ungemwambia dada endelea katiba inakuruhusu.

Una maana gani unaposema zoezi hilo la Kenyela haliko kwenye katiba kwa hiyo ni hahali kuendelea kufanyika???. Ningekuwa IGP ningekuvua vyeo vyako, maana wenzio wanakemea maovu wewe unahubiri maovu.

yaaaankwa wino mwekundu kabisaaaa,,,,yumekuelewa
 
mambo mengi hapa kwetu tunabambikiwa. utasikia marufuku kuandamana kesho wakati katiba inaruhusu wanakupotezea muda tu mahakamani haya mapolisi bure kabisa
 
Kenyela anafanya mambo kwa sifa akitarajia labda neema ya U-IGP inaweza kumwangukia ila kwa suala la ukahaba ni gumu mno kulithibitisha kisheria. Mathalani Kenyela na kundi lake la ITV wali kwenda Mwananyamala kufanya msako wa makahaba. Pale kwenye vile vyumba walikamata baadhi ya wapangaji wa kike wakiwa peke yao kwenye vyumba. Sasa mahakamani uta thubitisha vipi kuwa wale ni makahaba? Na utawashitaki kwa kosa gani na kwa kipengele kipi cha sheria kilicho vunjwa?

Opersehsni kama hizo zilishafanywa huko nyuma sio kigezo cha kusema kuwa serikali/polisi walikuwa sahihi. Rejea kesi ya kumshitaki Mrema na sungusungu yake. Kila mtu alitii kulinda sungusungu pale jamaa mmoja wa Magomeni (kam sijakosea) alikataa kulinda Mrema aka amrisha akamatwe na kuwekwa lupango. Mahakamni jamaa alimweka Marando kama wakili na mahakama ikatamka jeshi la sungusungu liko kinyume cha sheria hivyo jamaa hakuvunja sheria yoyote

Kiondo yuko sahihi nyakati zimebadilika.Kama tuko serious kupinga ukahaba sheria itungwe , wabunge wengi wanaponea huko (Rejea ripoti ya mama Terry).
 
hata kama Kenyela amekosea,Kiondo hakutakiwa kuliongelea jambo hilo kwa jamii.


Alichofanya Kamanda Kiondo ni completely unethical. Mosi, yeye ni Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Temeke inakuaje aje kuongelea Mkoa wa mwenzie Kenyela i.e Kinondoni? Hana jurisdiction na Kinondoni. Yaani ni sawa na Kamanda Kova wa kanda maalum D'salaam aongelee mambo ya mkoa wa Tabora, hii italeta chaos within the force.

Mbili, hivi inakuwaje watu mpo ndani ya taasisi moja tena jeshi ambalo linajulikana kabisa moja kati ya kanuni zake kuu ni nidhamu si tu baina ya maofisa bali pia taratibu za kimfumo ajitokeze ofisa mmoja kumpinga mwenzie kwenye media? Katokea wapi huyu kamanda Kiondo? Kwa hili amepotoka vibaya, nitashangaa sana kama taratibu za kinidhamu zitampitia kando.
 
Kiondo anaweza kua sahihi
ila kumkosoa mwenzake kwenye vyombo vya habar inaweza kua tatizo
msishangae akarud makao makuu kupanga mafail,inaweza kua sheria hakuna
ila machangu hukamatwa kuanzia enzi haijaanza leo na ndio humo suspect
wa madawa ya kulevya na ujambazi hupatikana police lazima awe skeptic
kitu ambacho askar wetu wanajsahau.

Hivi mkuu unafikiri wauza madawa ya kulevya hawafaamiki polisi?? Hawajulikani?? au unafikiri majambazi hawajulikani?? Polisi wanawajua A-Z.
Kuwakamata hao makahaba ni kuwaonea tu, je unamshitaki kwa kosa gani? Yeye alikuwa anauza K yake...
Nachokiona hapa huyu kenyela amekosa kazi ya kufanya, tena ni mpuuzii kabisa... wakina riz wanauza poda wanawaacha tu, nyambaf lake...
 
hata kama Kenyela amekosea,Kiondo hakutakiwa kuliongelea jambo hilo kwa jamii.

naam, "code of conduct" za utumshi/watumishi zimekiukwa. hivi jeshi la polisi halina vikao vya kiutendaji?. nimegundua kwa nini Wilaya ya Temeke inamadada/kaka poa wengi na halaiki kubwa ya watumiaji wa madawa ya kulevya.
 
Dah!makamanda wanakosoana live kwenye media?siku hizi hakuna maadili jeshini
 
Kwa taarifa yako, ukahaba ni kosa kishria.

Tanzania Penal Code
CHAPTER XV
Ofences Agaist Morality.
146. Any woman who knowningly lives wholly or part of the woman earning of prostitution or who is proved to have, for the purpose of gain, exercised, control, direct or, influence other over the move for engaging in prostitute in such a manner as to show she is aiding, abetting or compelling her prostitution, with any person, is guilt of misdemeanour.

Mkuu asante kwa kutuletea hii sheria. Now the problem is, how do you prove beyond doubt that these ladies were actually exercising prostitution before the court of law? Na je sheria inasemaje kuhusu wateja wa hao wadada? Ili kitendo cha prostitution kikamilike, lazima awepo mwanamke na mwanamme. Je wanaume wanaowanunua hao wadada wao wanakosa au hapana?

Tiba
 
Sababu zako ni zipi?
Tujuze

Hakuna sheria inayoruhusu kahaba kukamatwa, labda kama ingekuwa ni mtoto chini ya miaka 18 lakini kwa mijitu iliyoamua yenyewe na inazaidi ya 18yrs kuwakamata nikuwakosea haki. likini siku nyingine mkuu uwe unasoma yoote yameelezwa kwenye 1 post!
 
Cheap popularity,kwa wote.Hakuna jipya.Tunatafuta ujiko kupitia kwenye migongo ya watu.Tuache hizo
 
Wamekukosea nini au unachuki binafsi.fikiria vizuri-wewe umeshiriki kutunga sheria za nchi hii wabaya wako wanacho fanya ni kutekeleza/kusimamia hizo sheria mlizo zitunga.
 
Huyu Kiondo mgonjwa wa akili katiba hairuhusu kabisa uchangudoa.Anakurupuka kuongea na vyombo vya habari wakati hana ufahamu wowote.Mbavu kabisa
 
sauti ya waziri wa mambo ya ndani kuhusu swala hili ni ipi? Tusijifanye tunao utamaduni wetu kumbe tuna-act tu! Waacheni raia wawe huru, elimradi wasivunje sheria ya Inchi.
 
ukweli ni kuwa kENYELA KACHEMKA SANA TUUU!


Tatizo kamanda Kiondo amekurupuka, mm niwakumbushe Penal Code Cap. 16 inaeleza bayana kuwa haya ni makosa ya jinai
1. mwanamke kufanya ukahaba au
2. mtu yeyote kumiliki danguro na kulitumia kwa ajili ya kujipatia kipato
3. kuwauza wasichana kwa ajili ya kujipatia kipato
4. mwanaume kujiuza kama mwanamke au kufanya ushoga
5. kufanya ulawiti
6. kufanya mapenzi ya jinsia moja
7. kufanya mapenzi na wanyama/ndege
8.kuwauza binadamu -

kwahiyo anachokifanya kamanda Kenyela kipo sahihi kisheria, wasiojua ndio wanaweza kumpinga.

Hata kama ingetokea ikawa vitendo hivyo ni halali, basi bado vingekuwa haramu kwa sheria zingine za usumbufu wa jamii yaani public nuisance, hivi wadau unajisikiaje unapotoka ofisini umechelewa halafu unapita usiku barabarani unakuta wanawake watu wazima wanatembea uchi au wengine wakiona gari wanainua juu nguo zao na kubakiza kufuli peke yake ambalo nalo ni kiuzi kimekatisha kuficha tu, je hilo si machukizo kwa jamii, wakati mwingine unapita na watoto/wazee n.k. kwa bahati mbaya barabara zetu zina option chache za kupita

haya kazi kwenu
 
Hivi umemkamata mtu barabarani utakuwa na ushahidi kweli anafanya ukahaba? Ila biashara ya ukahaba siyo!
 
ukweli ni kuwa kENYELA KACHEMKA SANA TUUU!
To your opinion, unadhani Kenyela alikurupuka tu kwenda kukamata au alijulishwa na wananchi wa maeneo yale kwamba wanapata kero kutokana na uwepo wa hayo madanguro?

Sheria inawezekana haisemi kitu chochote kuhusu madanguro na makahaba, lakini sheria inampa haki mtu ya kutokubughudhiwa na mwingine. Ulaya hata ukifungulia redio kwa sauti kubwa, majirani wakapiga simu polisi kwamba unawasumbua, unakamatwa na kushitakiwa kwa kuwasababishia usumbufu wenzako.

kwa hiyo hata hao makahaba kufanya biashara hiyo karibu na makazi ya watu na kuwaharibia watu wengine utulivu wao, ni kosa kisheria.
 
Back
Top Bottom