Makahaba Wagonganisha Ma RPC Dar

Makahaba Wagonganisha Ma RPC Dar

Goodrich

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2012
Posts
2,091
Reaction score
1,179
MAKAMANDA wawili wa polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Charles Kenyela wa Mkoa wa Kinondoni na Kamanda wa Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, wamekwaruzana na kurushiana maneno yasiyofaa kuhusu namna ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi.

Kutofautiana huko kumeibuka baada ya wiki iliyopita, Kamanda Kenyela kufanya operesheni ya kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba, maarufu kama machangudoa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Baada ya Kamanda Kenyela kuendesha operesheni hiyo, Kamanda Kiondo wa Temeke, alinukuliwa na vyombo vya habari jana, akikosoa zoezi hilo na kusema hakuna sheria nchini inayozuia mwanamke kujiuza.
Katika maelezo yake, Kamanda Kiondo alisema, operesheni hiyo ilifanywa kwa kukurupuka na kwamba kamanda huyo hajasomea elimu ya jamii juu ya madanguro.

Kwa mujibu wa Kamanda Kiondo, kama Kamanda Kenyela angekuwa anaielewa vizuri elimu hiyo, kamwe asingedhubutu kuwakamata wanawake hao bali angewapatia elimu na ushauri dhidi ya maradhi wanayoweza kuambukizwa.
Pamoja na hayo, alihoji kuna umuhimu gani wa kuwakamata machangudoa wakati hakuna sheria inayomtaka awafikishe mahakamani badala yake anayetakiwa kushitakiwa ni mtu anayetoa nyumba ili itumike kama danguro.

Naye, Kamanda Kenyela alipozungumza na MTANZANIA jana juu ya kauli za kejeli zilizotolewa na mwenzake huyo, alisema amestushwa na taarifa ya Kamanda Kiondo kwa kuwa amemdhalilisha kupitia vyombo vya habari. “Yaani mwandishi sipati picha kama Kamanda Kiondo ambaye hana miezi sita kwenye nafasi hiyo tangu ateuliwe, anaweza kunidhalilisha juu ya utendaji wangu wa kazi, kwanza inakuwaje azungumzie mambo ya Kinondoni wakati mimi nipo? “Kama alijua nimekosea, alipaswa kunipigia simu kwanza tushauriane kabla ya kusema kwenye vyombo vya habari au angenisema kwa wakubwa wetu ambao wangeniita na kunishauri ili nisitishe operesheni hiyo, kama kweli ninakwenda kinyume.

“Amenidhalilisha sana na unajua ni vigumu kwa kamanda kama yule kutoka kwenye himaya yake na kuzungumzia himaya ya kamanda mwingine wakati mhusika yupo. “Kibaya zaidi anasema eti mimi sina elimu ya jamii juu ya madanguro, lakini binafsi siwezi kuona vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani au usumbufu kwa raia wengine, halafu nikakaa kimya, sitaacha kuchukua hatua.

“Ninachoweza kumwambia Kamanda Kiondo ni kwamba, sina ugomvi naye na pia sitaki malumbano naye, kazi ya kudhibiti uhalifu haihitaji mpango mmoja lazima tutumie njia mbadala kuhakikisha tunatimiza majukumu yetu ya kulinda raia na mali zao, nafikiri suala hilo linazungumzika tuache litapata suluhisho,” alisema Kamanda Kenyela akionyesha kukerwa na kauli za Kamanda Kiondo.


Source: Mtanzania, 14th Jan 2013


My Opinion:
Kamanda Kenyela yupo sahihi, sheria ipo inayokataza vitendo vya ukahaba - http://www.un.org/Depts/los/LEGISLATIONANDTREATIES/PDFFILES/TZA_penal_code.pdf
 
ukweli ni kuwa kENYELA KACHEMKA SANA TUUU!
 
Engelbert Kiondo, bila shaka umesoma sheria na katika sheria imeainisha kazi halali na kazi isiyo halali.

Tunaposema kazi halali inayompa mtu kipato ukahaba si kazi halali japo unampa mtu kipato lakini si kazi halali, Afande kazi hii wanawake hawa wanaifanya si kwa lengo la kupanua ajira zenu millioni moja la hasha ni shida ndiyo hayo "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania" tuliyoahidiwa lakini nadhani hata muasisi wa "Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya" hawezi kuungana na wewe kuhusu hili. Tusiendelee kulea maovu kiasi hiki. Nyie Polisi mmekuwa mkiwaua raia je hili liko kwenye katiba? Najua utasema Polisi huwa wanajihami, je raia wakijihami mbona mnasema haiko katika katiba. Samahani ingekuwa Ndugu yako wa karibu kabisa katika zoezi lenu la kuwaondoa machangudoa ukakutana na ndugu yako wa damu ungemwambia dada endelea katiba inakuruhusu.

Una maana gani unaposema zoezi hilo la Kenyela haliko kwenye katiba kwa hiyo ni hahali kuendelea kufanyika???. Ningekuwa IGP ningekuvua vyeo vyako, maana wenzio wanakemea maovu wewe unahubiri maovu.
 
tuseme tu ukweli Kamanda Kiondo yuko sahihi vinginevyo Bunge litunge sheria itakayodhibiti vitendo vya ukahaba! mathalani makahaba wanakamatwa, wanafikishwa mahakamani na kushitakiwa kwa kosa la uzururaji. hao makahaba wakikataa kwamba hawakuwa wakizurura ila walikuwa wanapita njia tu then wakakamatwa. kwamba hawajui wamekosa nini maana hakuna sheria hapa TZ inayozuia mtu asitembee wakati wowote usiku. hapo hawajashinda kesi? makahaba wanaohukumiwa huwa hawajui kujitetea mahakamani!
 
Sijui kama kuna mwanaume ambae hajalala na changudoa kwa kujua au bila kujua.Kinachowatofautisha ni mazingira ya kazi tu. Kama kuna mwanmke anayetoa bure kwa wanaume sijui atakuwa wa wapi. Kitendo cha kupokea hela kila anapofanya hiyo kitu kitaitwaje? Na huyo kamanda ameshindwa kupambana na wezi anaelekza nguvu kwa vyangudoa? Atuambie priority ni nini. Kama huwezi kumshtaki mtu kwa kosa alilofanya basi hakufanya kosa Au sio polisi?
 
Kiondo anaweza kua sahihi ila kumkosoa mwenzake kwenye vyombo vya habar inaweza kua tatizo msishangae akarud makao makuu kupanga mafail,inaweza kua sheria hakuna ila machangu hukamatwa kuanzia enzi haijaanza leo na ndio humo suspect wa madawa ya kulevya na ujambazi hupatikana police lazima awe skeptic kitu ambacho askar wetu wanajsahau.
 
Kamanda wa Kinondoni kachemka. Bora aseme makahaba wamevunja sheria gani ya nchi hadi awakamate.
 
Madada poa/ changu doa na kaka poa wanatimiza ahadi ya ajira milioni moja! Kitu muhimu ilikuwa ni kuwapa elimu ya afya na kujilinda na magonjwa za zinaa. Badala ya kuwashughulikia wanaohujumu uchumi wa nchi kupita kiasi, wezi, matapeli na mafisadi au kuzifunga casino, wao wanashughulika na dagaa!
 
Waache WAPIKANE wenyewe kwa wenyewe! wakiiva TUTAOMBA ELIMU YAO ITAZAMWE UPYA!
 
Kamanda wa Kinondoni kachemka. Bora aseme makahaba wamevunja sheria gani ya nchi hadi awakamate.

Kwa taarifa yako, ukahaba ni kosa kishria.

Tanzania Penal Code
CHAPTER XV
Ofences Agaist Morality.
146. Any woman who knowningly lives wholly or part of the woman earning of prostitution or who is proved to have, for the purpose of gain, exercised, control, direct or, influence other over the move for engaging in prostitute in such a manner as to show she is aiding, abetting or compelling her prostitution, with any person, is guilt of misdemeanour.
 
Kiondo anaweza kua sahihi ila kumkosoa mwenzake kwenye vyombo vya habar inaweza kua tatizo msishangae akarud makao makuu kupanga mafail,inaweza kua sheria hakuna ila machangu hukamatwa kuanzia enzi haijaanza leo na ndio humo suspect wa madawa ya kulevya na ujambazi hupatikana police lazima awe skeptic kitu ambacho askar wetu wanajsahau.

Kwa mujibu wa sheria za makosa ya jinai za Tanzania ni hivi:

Tanzania Penal Code
Chapter XV
Offences Agaist Morality
147. If it is appeal to the magistrate by information on power of oath that there is reason to suspect any house or part of a serch house is used by a woman for the puposes of prostitution, and that any person residing in or frequenting the house is knowningly living wholly or in part of the earnings are of the prostitute, or is exercising, control, direction of influence over the movement of the prostitute, the magistrate may issue a warrant authorising any poloce officer to enter and search the house and to arrest such person.
 
kuna mambo mengi ya kweli yanayovuruga amani ya raia kama machinjo na ujambazi. Polisi wanabaki kusumbua raia wasio na hatia na vitisho.
 
Kamanda Kiondo kachemka anamdharau mwenzake kwa kusema amesomea mambo hayo South Afrika lakini inaelekea alikuwa anakariri kwani hajui sheria za South afrika na Tanzania zinasemaje juu ya ukahaba na tamaduni wakati wenzetu south mpaka ushoga umeruhusiwa sisi kisheria hatujaruhusiwa kamanda Kenyela angepaswa kupongeza kwa kusimamia na kulinda maadili ya kitanzania sio huyo aliyepoteza bure kodi za watanzania kwani pamoja na kuhitaji elimu toka kwa wenzetu walioendelea lakini inapaswa tuwe makini na mafundisho yao yanayoenda kinyume na tamaduni zetu ndiomaana leo hii bado tunatawaliwa pamoja na kuwa tuna uhuru wa zaidi ya miaka 50
 
Back
Top Bottom