Agricultural Reseacher
Member
- Jun 7, 2022
- 14
- 23
-Gharama za kuzalisha mkonge kwa ekari moja
-Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa I
-Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa II
-Kipindi cha marejesho (Payback period)
View attachment 2257362
View attachment 2257363
Kilimo-Biashara
-Kilimo biashara ni nini?
Kilimo-Biashara ni neno moja linalo unganishwa na maneno mawili neno KILIMO na neno BIASHARA.
Ni shughuli ya kilimo inayo husisha matumizi bora ya elimu ya ujasiriamali katika kujipatia faida.
-Nguzo kuu 4 za kilimo biashara ni:
•Wazo sahihi
•Maarifa na uzoefu (Kilimo chenye tija kinahitaji maarifa na taarifa sahihi)
•Rasilimali (Ardhi, mtaji wa fedha nk)
•Juhudi ya kazi.
Gharama za kuzalisha mkonge ekari moja Kwa Mkulima Mdogo
- Uandaaji wa shamba:
Ø Kukata miti na kung’oa visiki ni sh. 100,000.00
Ø Kukusanya na kusafisha eneo ni sh. 50,000.00
Ø Kulima kwa trekta (Ploughing) ni sh. 60,000.00
Ø Kulainisha udongo (Harrowing) sh. 50,000.00
q Kupima shamba kwa ajili ya kupanda miche:
Ø Kukata mambo za kuweka vipimo vya shamba (Layout) sh. 10,000.00
Ø Kamba ya mkonge kilo 4 sh. 20,000.00
Ø Gharama ya kulipa wafanyakazi 2 sh. 30,000.00
Utunzaji wa shamba miaka mitatu ya kwanza
Ø Palizi kwa miaka 3 @250,000 sh.750.000.00
-Jumla ya gharama zote kabla ya kuvuna majani ya kwanza ni sh. 1,444,000.00
Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa I
-Kwa kawaida mavuno ya kwanza hupatikina kidogo (tani 0.4)
-Gharama ya usindikaji wa tani 1 ni sh. 400,000.00
- Jumla ya gharama za uzalishaji tangu kuanza kwa mradi ni sh. 1,444,000.00
- Gharama za uvunaji kwa ekari sh.100,000.00
-Wastani wa bei ya singa za mkonge ni sh. 3.5 milioni kwa tani 1
- Mauzo ya singa yataingiza sh. 1,400,000.00
-Faida baada ya kuondoa gharama za uwekezaji na uendeshaji kwa ekari ni sh. (544,000.00)
Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa II
-Mwaka 2 mavuno huongezeka kidogo (tani 0.8)
-Faida baada ya kuondoa gharama za uwekezaji na uendeshaji kwa ekari ni sh. 1,294,000.00
- Jumla ya gharama za uzalishaji uthibiti wa magugu shambani ni sh. 250,000.00
- Gharama za uvunaji kwa ekari sh.100,000.00
- Gharama ya usindikaji wa tani 1 ni sh. 400,000.00
- Wastani wa bei ya singa za mkonge ni sh. 3.5 milioni kwa tani 1
- Mauzo ya singa yataingiza sh. 2,800,000.00
Kipindi cha marejesho (Payback period)
-Mradi unatazamiwa kurejesha gharama zote za uwekezaji na kuanza kuingiza faida katika mwaka wa 2 wa ukataji majani (mwaka wa 4 tangu shamba kuanzishwa).
- Mkonge aina ya H.11648 huzeeka inapofikisha miaka 12-15, hivyo mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa kuwa gharama pekee atakazolipia ni utunzaji, ukataji na usindikaji.
Agricultural ReseacherSamahani Researcher, sijaona sehemu umereflect bei ya mbegu/miche. Je, bei ya miche ya kisasa iliyo tayari kupandwa shambani inauzwa sh. ngapi kwa mche au sh. ngapi kwa hekari (ulisema hekari moja inaingia miche 3500 - 5000 kutgemea na style unayopanda (mraba mmoja/miwili)?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]ila jamii forum kuna vichaaaTupe na ile hesabu ya Matikiti mkuu na Ile ya mayai ya kwale.
Tunataka kuwa matajiri Sasa
Kivipi Mkuu? Si unauza then unanunua kinachoingia tumboni?Sitokuja kulima zao lisilohusiana na tumbo la mwanadamu mimi.
1. Hujaweka bei ya Shamba
2. Bei ya miche/mbegu
3. Gharama za Palizi zinaonekana kuwa kubwa kuliko thamani ya ardhi ?????
Kima wanakula mkonge?Asante sana kwa uzi na mchanganuo, japo kuna baadhi ya vitu havijawekwa au gharama si halisia.
1. Gharama ya ardhi roughly kuanzia 200k, inategemea na wilaya/eneo
2. Gharama za kufyeka, kuchoma na kusafisha shamba na kung’oa visiki kwa eneo nilipo inaweza kufika hata 400k
3. Gharama ya kupima, kuchora, kamba, mambo na mtaalam nazo ziko juu kidogo
4. Wataalam wanashauri kuweka lime na mbolea kutokana na matokeo ya kipimo cha udongo. Kiasili hii hatufanyi hivyo unaweza ignore.
5. Gharama za mbegu: Mlingano mche mmoja 150 hivyo andaa km 300k kwa hekali.
6. Kupakia n kusafirisha na kushusha mbegu itategemea umbali
7. Gharama za kupanda huwa ni 250k kwa hectare hivyo heka ni km 100k. Hii ni kwa wilaya ya Muheza, Tanga.
8. Gharama za kumaintain shamba inaweza isifike hasa ukilima mseto na mazao ya muda mfupi km mahindi, alizet nk. Japo ukipata ugonjwa inaweza kufika au kuzidi. Km itashambuliwa na wanyama km kima, nyani au nguruwe pori ni tatizo jingine pia.
Soko: range ni hiyo kati ya 3-4k kwa kilo
Hayo ni machache kutokana na uzoefu wangu mdogo.
Narudisha mic kwako researcher
Ndio maana yake yaani unazeeka after 12.yrs baada ya kuupandaUkipanda mara ya kwanza ni mpaka baada ya miaka 12 ndo unapanda tena au Mimi sijaelewa Agricultural Reseacher
Mbegu mbona hujaweka?-Gharama za kuzalisha mkonge kwa ekari moja
-Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa I
-Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa II
-Kipindi cha marejesho (Payback period)
View attachment 2257362
View attachment 2257363
Kilimo-Biashara
-Kilimo biashara ni nini?
Kilimo-Biashara ni neno moja linalo unganishwa na maneno mawili neno KILIMO na neno BIASHARA.
Ni shughuli ya kilimo inayo husisha matumizi bora ya elimu ya ujasiriamali katika kujipatia faida.
-Nguzo kuu 4 za kilimo biashara ni:
•Wazo sahihi
•Maarifa na uzoefu (Kilimo chenye tija kinahitaji maarifa na taarifa sahihi)
•Rasilimali (Ardhi, mtaji wa fedha nk)
•Juhudi ya kazi.
Gharama za kuzalisha mkonge ekari moja Kwa Mkulima Mdogo
- Uandaaji wa shamba:
Ø Kukata miti na kung’oa visiki ni sh. 100,000.00
Ø Kukusanya na kusafisha eneo ni sh. 50,000.00
Ø Kulima kwa trekta (Ploughing) ni sh. 60,000.00
Ø Kulainisha udongo (Harrowing) sh. 50,000.00
q Kupima shamba kwa ajili ya kupanda miche:
Ø Kukata mambo za kuweka vipimo vya shamba (Layout) sh. 10,000.00
Ø Kamba ya mkonge kilo 4 sh. 20,000.00
Ø Gharama ya kulipa wafanyakazi 2 sh. 30,000.00
Utunzaji wa shamba miaka mitatu ya kwanza
Ø Palizi kwa miaka 3 @250,000 sh.750.000.00
-Jumla ya gharama zote kabla ya kuvuna majani ya kwanza ni sh. 1,444,000.00
Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa I
-Kwa kawaida mavuno ya kwanza hupatikina kidogo (tani 0.4)
-Gharama ya usindikaji wa tani 1 ni sh. 400,000.00
- Jumla ya gharama za uzalishaji tangu kuanza kwa mradi ni sh. 1,444,000.00
- Gharama za uvunaji kwa ekari sh.100,000.00
-Wastani wa bei ya singa za mkonge ni sh. 3.5 milioni kwa tani 1
- Mauzo ya singa yataingiza sh. 1,400,000.00
-Faida baada ya kuondoa gharama za uwekezaji na uendeshaji kwa ekari ni sh. (544,000.00)
Tathmini ya mapato kwa mavuno ya mwaka wa II
-Mwaka 2 mavuno huongezeka kidogo (tani 0.8)
-Faida baada ya kuondoa gharama za uwekezaji na uendeshaji kwa ekari ni sh. 1,294,000.00
- Jumla ya gharama za uzalishaji uthibiti wa magugu shambani ni sh. 250,000.00
- Gharama za uvunaji kwa ekari sh.100,000.00
- Gharama ya usindikaji wa tani 1 ni sh. 400,000.00
- Wastani wa bei ya singa za mkonge ni sh. 3.5 milioni kwa tani 1
- Mauzo ya singa yataingiza sh. 2,800,000.00
Kipindi cha marejesho (Payback period)
-Mradi unatazamiwa kurejesha gharama zote za uwekezaji na kuanza kuingiza faida katika mwaka wa 2 wa ukataji majani (mwaka wa 4 tangu shamba kuanzishwa).
- Mkonge aina ya H.11648 huzeeka inapofikisha miaka 12-15, hivyo mkulima ataendelea kupata faida kubwa kwa kuwa gharama pekee atakazolipia ni utunzaji, ukataji na usindikaji.
Nadhani ni wastani! Inategemea na aina ya mbegu uliyopanda. Km ni maotea unaweza kuishia hata miaka 8 na wanasema ukipanda mbegu bora zinaweza kwenda mpk miaka 15Ukipanda mara ya kwanza ni mpaka baada ya miaka 12 ndo unapanda tena au Mimi sijaelewa Agricultural Reseacher
Kima, Nyani wote wanaharibu mkonge kwa kuvunja kile kiini cha mkonge na kukifyonza. Hawa mara nyingi wanaonea mkonge uliochini ya miaka 2.Kima wanakula mkonge?