Makada CCM, CUF, NCCR wafungua kesi ya kikatiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makada CCM, CUF, NCCR wafungua kesi ya kikatiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 7, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Makada CCM, CUF, NCCR wafungua kesi ya kikatiba
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 06 January 2012 20:00
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  [​IMG]Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila

  Waandishi Wetu
  WANANCHI wa Jimbo la Kigoma Kusini wamefungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam wakiiomba iamuru kusitishwa kwa matumizi ya Ibara ya 71 (1) (f) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano juu ya mbunge aliyefukuzwa uanachama katika chama chake.

  Pia wapiga kura hao wameiomba Mahakama iliamuru Bunge litunge sheria inayoruhusu mbunge aliyefukuzwa uanachama katika chama chake atambuliwe kuwa mbunge huru au aruhusiwe kuhama na ubunge wake kwenda chama chochote atakachotaka.

  Kesi hiyo imefunguliwa siku chache tangu Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila avuliwe uanachama wa NCCR-Mageuzi, hatua ambayo kikatiba inamvua ubunge wake. Kafulia alivuliwa uanachama Novemba 20, mwaka jana. Hata hivyo, amefungua kesi kupinga hatua hiyo.

  Kadhalika, siku tatu zilizopita, Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), lilimvua uanachama wa chama hicho Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed hatua ambayo inamfanya apoteze nafasi yake ya ubunge.

  Jana, CUF waliwasilisha barua katika Ofisi ya Spika wa Bunge, kumwarifu kuhusu uamuzi wa kumvua uanachama Hamad, huku mbunge huyo akisema uamuzi wa huo ni batili kwani ulikiuka amri ya mahakama iliyokuwa ikizuia kufanyika kwa kikao chake.

  Kesi ya Kikatiba
  Wapiga kura watatu wa Kigoma Kusini ndiyo waliofungua kesi hiyo ya kikatiba na kila mmoja anatoka katika chama tofauti cha siasa. Mmoja ni mwanaCCM, mwingine CUF na wa tatu anatoka NCCR Mageuzi. Walifungua kesi hiyo kwa niaba ya wananchi wengine wa jimbo hilo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo ya Kikatiba Namba 1 ya mwaka 2012 ni Juma Shaban Nzengula ambaye ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1980, mwenye kadi ya uanachama namba Aa 581252 ya Februari 5, 2003. Nzengula pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mkoa wa Kigoma akitokea katika Kata ya Nguruka.

  Mlalamikaji wa pili ni Patrick Haruna Rubilo, mwanachama wa NCCR-Mageuzi mwenye kadi ya uanachama namba 045845 ya 2000, pia akiwa Mjumbe wa Kata ya Itebula na Mwenyekiti wa Kijiji cha Bweru.

  Mlalamikaji wa tatu ni Fanuel Misigalo Bihole, mwanachama wa CUF mwenye kadi ya uanachama namba 1145401 ya Agosti 17, 2004 ambaye pia ni Katibu wa Wazazi wa Kata ya Mtegowanoti.

  Kwa mujibu wa hati ya madai waliyoiwasilisha mahakamani hapo, walalamikaji hao kupitia Kampuni ya Uwakili ya Mpoki & Associates, Ibara hiyo inakiuka haki za msingi zinazoelezwa katika Ibara ya 21 ya Katiba.

  Ibara hiyo inatoa uhuru wa kushiriki katika shughuli za umma kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa mujibu wa sheria.
  Pia wanadai kuwa Ibara hiyo inakiuka Ibara ya 201 (1) ya Katiba inayotoa uhuru kwa wananchi kushiriki na kutoa maoni kwa uwazi, na kwamba pia inakiuka Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Binadamu ambao Tanzania imeuridhia na kuusaini.

  “Matokeo ya Ibara hiyo ni kwamba kuna uwezekano kwamba mbunge wetu tuliyemchagua kwa kura nyingi anaweza kupoteza ubunge wake kwa matakwa ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya NCCR- Mageuzi ambao ni chini ya 30.”

  Kauli za wadai
  Wakizungumza baada ya kufungua kesi hiyo, walalamikaji hao walisema licha ya kwamba wanatoka vyama tofauti vya siasa uamuzi wao umejengwa katika msingi wa matukio ya kufukuzwa kwa Kafulila na Hamad Rashid.

  “Mimi ni mwanachama wa CCM na nilikuwa na mgombea wangu, lakini baada kuchaguliwa mbunge anakuwa ni mbunge wa umma. Kafulila alichaguliwa na wananchi 23,162,” alisema Nzengula.

  Kwa upande wake Rubilo alisema mbunge anafunga mkataba na wananchi na kwamba huwa wanatoa ahadi nyingi katika kutekeleza mkataba huo kama vile kusomesha watoto na shughuli nyingine za maendeleo... “Sasa anapovuliwa uanachama na kupoteza ubunge hizo shughuli zitakwama...” alisema Rubilo na kuungwa mkono na Bihole.

  Walalamikaji hao walitoa wito kwa watu wengine akiwamo Hamad Rashid wawaunge mkono katika kesi hiyo. Walisema ingawa wao ni wakazi wa Kigoma, wameamua kufungua kesi hiyo Mahakama Kuu Dar es Salaam kwa kuwa hoja yao si ya kijimbo, bali ni ya kitaifa na kwamba itawanufaisha Watanzania wote.

  CUF kwa Spika
  CUF kimewasilisha barua ya kumvua uanachama mbunge wa Wawi, Hamad Rashid katika Ofisi za Bunge. Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Julius Mtatiro alisema barua hiyo ilipelekwa jana katika Ofisi za Bunge Dar es Salaam na kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

  Katika hatua nyingine, Ofisi ya Bunge imesema haijapokea barua ya amri ya Mahakama Kuu kuzuia uamuzi wa NCCR-Mageuzi kumvua uanachama Kafulila.

  Kaimu Katibu wa Bunge, Eliakim Mrema alisema ofisi yake haijapata barua yoyote kutoka mahakamani inayofafanua amri hiyo... “Hakuna barua kama hiyo hapa ofisini kwetu… labda uiulize mahakama kama imeshatoa hiyo barua.”

  Hata hivyo, Kafulila akizungumza kwa simu akiwa Kigoma alisema: “Msajili wa Vyama vya Siasa (John Tendwa) alieleza kuwa barua ya Mahakama inaweza kupelekwa katika Ofisi za Bunge na chama chenyewe (NCCR) au mimi (Kafulila) na ndivyo nilivyofanya.”

  Alisema kazi ya mahakama ni kutoa amri baina ya chama na mwanachama na si kupeleka barua katika Ofisi ya Bunge.”

  Katibu Mkuu wa NCCR, Samwel Ruhuza alisema hawawezi kupeleka barua hiyo katika Ofisi za Bunge kwa kuwa amri hiyo haikukitaka kibatilishe uamuzi wake dhidi ya Kafulila... “Mahakama imesema kama chama, tusijadili wala kutoa uamuzi wa jambo lolote linalomhusu Kafulila… haikusema kama haitambui uamuzi ya chama.”

  Katika hatua nyingine Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Johnson Rweikiza amesema maslahi ndicho chanzo cha vyama vya upinzani kufukuzana uanachama.“Haya yanaonyesha dhahiri namna viongozi walivyo na uchu wa madaraka na si kuwajibika kwa ajili ya jamii,” alisema Rweikiza

  Habari hii imeandikwa na James Magai, Fidelis Butahe na Geofrey Nyang’oro
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  for the first time in my entire life I am beginning to see light at the end of this cryptic tunnel.........mgombea binafsi kuja hata kabla ya katiba babaishi kupitishwa.........
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Unafanya mchezo na posho ya 200000 per day.......
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  ilikuwa lazima wafungue hiyo kesi
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  ubunge usihusishwe na vyama, hata kama akivuliwa uanachama, aendelee kuwa mwanachama. hii itadhibiti pia vyama fukuzafukuza
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwa nini wana hangaika kihivyo waache tuingie kwenye uchaguzi . Watu anasema ni ghara kubwa sana kwani hizo hela zinafanya kazi gani ? kwa njia ya uchaguzi hata wanyonge nao wataambuli japo kidogo tu hata kama ni kanga, kofia , t-shirt etc watajistiri mwili kuliko kuwaachia kabisa pesa yote wanakula wachache tu
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Safi sana. Wacha tu mahakama ikatoe tafsiri ya kisheria manake watu wananyimwa haki na watu wachache. Mbunge anakuwa amechaguliwa na watu zaidi ya elfu ishirini lakini kanakuja kajigenge ka watu wachache kanamfuta kazi na kuwakosesha hao wote uwakilishi!
   
 8. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,337
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  'kwa nini wana hangaika kihivyo waache tuingie kwenye uchaguzi . Watu anasema ni ghara kubwa sana kwani hizo hela zinafanya kazi gani ? kwa njia ya uchaguzi hata wanyonge nao wataambuli japo kidogo tu hata kama ni kanga, kofia , t-shirt etc watajistiri mwili kuliko kuwaachia kabisa pesa yote wanakula wachache tu'

  Hili ni suala la kitaifa so kuchangia kijinga kama hapo ni uzembe wa kutumia ubongo. Mahakama ilishatoa hukumu tangu 1994-5 na kukubali kuwa ni haki kuwa na mgombea binafsi. Ila sasa serikali ndio ilizorotesha na kushawishi mahakama kuwa passive na ukweli huo. Safari hii tunaomba busara na nguvu ya kisheria itumike na haki ipatikane. Kafulila atakuwa mbunge wa kwanza binafsi. What a precedent.
   
 9. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi kwelikweli
   
 10. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ngoja niende msalani kwanza ntarudi kuchangia!!
   
Loading...