Makaburini: Ni sehemu iliyojaa upweke na ukiwa

Makaburini: Ni sehemu iliyojaa upweke na ukiwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,659
Reaction score
870,343
Wote tumeshawahi kufika makaburini kuzika ndugu, jamaa na marafiki na hata tusiowajua! Ni sehemu ambayo mara huwa busy na watu wengi wakipishana lakini mara baada ya mazishi watu hutawanyika na kuliacha kaburi peke yake, upweke na ukiwa huanzia hapo. Unarudi nyumbani peke yako ukimwacha mpendwa wako kule chini ya shimo na kilo nyingi za udongo juu yake.

Sasa upweke na ukiwa huo huongezeka zaidi usiku unapoingia na hasa kama umeamua kwenda kulala makaburini kwa sababu yoyote ile.

Mwaka 2005 jamaa yetu mwenye ulemavu wa ngozi (albino) alifariki hapa Dar na mazishi yalikuwa Msata, tukaenda huko, basi baada ya mazishi ikabidi wapatikane watu watatu au zaidi; hata kwa malipo kwa ajili ya kulilinda lile kaburi kwa siku mbili tatu, ili lisije kufukuliwa na wenye kuhitaji viungo vya albino.

Kwanza ilikuwa shida kupata watu lakini mimi nikajitolea, bahati nzuri kuna vijana wengine wawili wa pale pale Msata nao wakajitolea kwa sharti la kununuliwa bangi na gongo, wakakubaliwa.

Basi ilipofika sita usiku tukajivuta mpaka eneo la tukio ni pale msata barabarani kuna msitu una makaburi mengi sasa la jamaa yetu lilikuwa nyuma ndani kabisa kuna kiza kinene kuko kimya kabisa na kunatisha.
Jamaa na mibangi yao na gongo lao mi na tochi yangu na simu yangu ya mchina (wakati huo ndio zilikuwa hot kweli) tukatafuta mti mkubwa si mbali na kaburi tukaweka makazi pale.

Wale vijana wakala bangi sana lakini stimu zikawa hazipandi, wakanywa na gongo lakini wapi, kumbe walikuwa wanaogopa mno ile hali ya kukaa peke yetu kule makaburini, tena kizani.

Nikasema subiri nikatoka chemba nikaenda kutegesha alarm saa nane usiku ikifika ilie halafu nikaweka mlio wa paka sauti ya juu, nikaficha simu yangu kwenye koti. Nikarudi nikaaza kuwapigisha stori lakini za kutisha tupu! Hakika walitia huruma kwa hofu.

Nane kamili usiku tukasikia nyaaauuu pale tulipo! Wale vijana kila mmoja aliruka na kushika njia yake! Sijawahi kucheka kama siku ile! Mmoja alienda kuzirai barabara kuu mwingine akikutwa Kituo cha Polisi Msata chini ya kaunta na bangi zake mfukoni.

Makaburini kusikie hivi hivi!!!
 
Hahahaaa Ungeua, kuna siku nlijishaua nina mistress yangu nikaenda makaburini, Wallahi sikumaliza hata dakika 5, nlifagia kaburi huku natetemeka fasta nikasepaa. kunatisha kule.
 
Back
Top Bottom