Makabila ya Tanzania ni mengi lakini yanayoonekana wazi ni mawili au matatu

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
13,287
18,013
Tanzania ina makabila zaidi ya 120 lakini yanayoonekana wazi ni mawili au matatu hadi manne tu ambayo yanaonekana wazi hawajaacha utambulisho wao, nao ni wamasai, wasukuma, wabarbeigi na wahazarbe. Hawa utawona wakiwa na mavazi yao hata wakienda mjini utawajua tu hawafichi utambuliko wao, wanaongea mpaka lugha yao hadharani bila aibu.

Makabila mengine huwezi kuwatambua utaishia kukisia tu ni kabila gani. Wengine utasikia lafudhi tu na kukisia ni kabila gani na utakosea. Makabila mengi yamevurugika na kuacha tamaduni zao za utambulisho ni waswahili watupu
 
A Man without his culture, Origin & History is like a Tree without its roots" it will fall down suddenly

By Marcus Garvey

Makabila mengi hayana tena utambulisho wao wala cha kujivunia...wamemezwa na utamaduni wa kizungu na kiarabu
 
Ukipanda vyombo vya usafiri mmasai, msukuma, mbarbeigi utamjua haraka kwa mavazi na lufudhi/lugha yake. Hawa wengine si rahisi kuwatambua. Treni nzima ya mabehewa ya kwenda bara wanaongea lugha yao bila aibu. Makabila mengine hawajioneshi, wanataka waonekane ni waswahili tu, ukimuongelesha kilugha yake anajifanya hajui lugha yake ya asili anakujibu kwa kiswahili, anaona aibu ataonekana ni mshamba wa kijijini
 
Sasa inakuaje kabila moja tu kati ya makabila 120 lenyewe lionekane ndiyo brand ya utalii Tanzani? Pale KIA kabila hilo ndio hupekea watalii, watalii huondoka na picha wakijua hao ndio watanzani tu. Wachoraji wa picha za utalii nao huchora kabila hilo tu, wakiwa na nyumba zao za asili, wakiwa na ng'ombe zao. Vipi makabila mengine nayo hayawezi kuwa brand ya utalii Tanzania?
 
Kuna abiria mmoja aliyejaliwa kuwa mnne kiasi cha kujaa siti mbili peke yake kwenye daladala jijini dar, abiria wenzake toka mikoani walimsema kwa kabila yake kuwa ni mnene mno akawasikia na kuwajibu vibaya. Wale abiria wenzake hawakujua kuwa huyo ni kabila lao na lugha ya asili yao anaijua. Watu wa mikoani wakija dar hawataki kujulikana asili zao wanataka waonekane ni waswahili tu, wakitetwa wanasikia na kujibu vibaya kwa lugha yao hiyohiyo
 
Kwani ukiwa mnene inabidi ujibandike usoni kabila lako?
 
Mi huwa namwambia tu mtu mi kabila fulani, halafu wala sifeel kuwa mimi ni wa hilo kabila, maana sina nikijuacho hata sijawahifika huko kwenye huo mkoa.
Hata wanasalimianaje sijui

Hata wanangu sijui nitawaambia nini kuhusu kabila
 
nao ni wamasai
Umenikumbusha kuna Mzungu aliingia na Morani lodge moja, mmasai yule mrefu mweusi km mpingo alikua amevaa rubega na mkononi ana fimbo na kichwani kasokota rasta, walipoingia lodge Mzungu akambadirisha mmasai kwanza rasta kamfumua pili zile rubega kamvua akamveka suruali na t-shirt nahisi zilikua za kwake walipotoka ungeweza kumgundua huyu ni mmasai kwa vitu vitatu moja ana kovu la kuunguzwa na betrii kwenye paji la uso na mashavuni, mbili katoboa masikio yote mawili yananing'inia na tatu ana mwanya kwenye uvungu wa meno ya chini

Mavazi sio utambulisho
 
Tanzania ina makabila zaidi ya 120 lakini yanayoonekana wazi ni mawili au matatu hadi manne tu ambayo yanaonekana wazi hawajaacha utambulisho wao, nao ni wamasai, wasukuma, wabarbeigi na wahazarbe. Hawa utawona wakiwa na mavazi yao hata wakienda mjini utawajua tu hawafichi utambuliko wao, wanaongea mpaka lugha yao hadharani bila aibu.

Makabila mengine huwezi kuwatambua utaishia kukisia tu ni kabila gani. Wengine utasikia lafudhi tu na kukisia ni kabila gani na utakosea. Makabila mengi yamevurugika na kuacha tamaduni zao za utambulisho ni waswahili watupu
kila mtu angedumisha kabila nchi isingetawalika
Nenda ethiopia ndo utaeleweka

Kujenga nchi inabidi muue ukabila muhimiza uinchi
 
Sasa inakuaje kabila moja tu kati ya makabila 120 lenyewe lionekane ndiyo brand ya utalii Tanzani? Pale KIA kabila hilo ndio hupekea watalii, watalii huondoka na picha wakijua hao ndio watanzani tu. Wachoraji wa picha za utalii nao huchora kabila hilo tu, wakiwa na nyumba zao za asili, wakiwa na ng'ombe zao. Vipi makabila mengine nayo hayawezi kuwa brand ya utalii Tanzania?
Mpaka rais anawaonea wivu, anawatawanya na kuwatoa katika makazi yao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom