Majuto ni Mjukuu

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Yule hayati mzee wa butiama aliwaona walivyokuwa na uchu siku nyingii....
akamwambia mamvi we ni mwizi kaa kando,leo mkasahau mkamkaribisha ndani,kawakomba! nani alaumiwe?
Kumcheki Mkwere akamwambia we bado una mambo ya Boys II men yaani baado kabisa,mkasahau mkadhani amekua...leo amerudi jukwaani kuonyesha usanii wake,sijui yule babu akiamka atawaelewa kweli?
mdharau mwiba...
 
Halafu bado wanataka kumlipa za Dowans, huku wanaojua hali ya mambo wanadai eti wajanja wametuzidi.
Hakuna kulipa hela za Dowans kuonyesha kuonyesha na sisi tumewashtukia.
 
Hiyo ni kweli mkuu ila Watz huwa hatusikia la mkuu ila sasa yametukuta. Akifufuka leo mzee wa Butiama atarudi kaburini mara moja
 
Hiyo ni kweli mkuu ila Watz huwa hatusikia la mkuu ila sasa yametukuta. Akifufuka leo mzee wa Butiama atarudi kaburini mara moja

tunaongozwa na genge la wahuni..hamna utawala wa sheria kila mtu anasema lake
 
ingawaje gundu bado lipo kwa mzee John kabaki kuchonga mabarabara na akitaka kuyatumia wanamkataza.
 
Point Taken.

Nafikiri kwa mfumo wa uzalishaji wa wanasiasa katika Tz bado majuto yako mbele. Hao wawili ni sehemu ndogo sana ya kundi kubwa la wasiofaa wala kustahili ambao kwa sasa wanatawala Tz. Kwa mfano; hivi Mwl Nyerere angesema nini juu ya RA/Karamagi/Ngeleja/Mgonja/Balali?

Ni kama vile hiki kizazi cha mafisadi kiatokomee kije kingine au kiwekwe kando kwa nguvu ya umma na kisheria (Katiba Mpya), ndipo majuto yatapungua.
 
Halafu bado wanataka kumlipa za Dowans, huku wanaojua hali ya mambo wanadai eti wajanja wametuzidi.
Hakuna kulipa hela za Dowans kuonyesha kuonyesha na sisi tumewashtukia.

Suala la dowans ni la kimkataba na limetolewa maamuzi ya kimahakama, wewe hujui lolote ni bora unyamaze tu kwani hapa tunaongelea mambo ya TZ hatuko kenya hapa mkuu
 
Suala la dowans ni la kimkataba na limetolewa maamuzi ya kimahakama, wewe hujui lolote ni bora unyamaze tu kwani hapa tunaongelea mambo ya TZ hatuko kenya hapa mkuu

Hukumu nyingi zimewahi kukosewa kwa kutafsiri sheria vibaya au kwa msukumo wa kimaslahi wa mlalamikaji.
na hii ni mojawapo mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom