Majuto ni mjukuu, Kikwete ulikuwa na nafasi kutupatia Katiba Mpya

macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
10,148
Points
2,000
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
10,148 2,000
Ipo siku utaguswa utaelewa wenzio wanalalamikia nini juu ya huu utawala.
Kama ni kuguswa nilishaguswa kitambo kwenye tawala zilizopita. Hivyo nikiguswa ni mwendelezo tu ''kuishi dunia ya tatu'' na siyo eti ni kwa sababu ya Magufuli. Wakati wa Kikwete nilishawahi kukamatwa uzururaji na nikatoa fedha ili niachiwe japo mimi siyo mzururaji. Niliwahi kufokewa na polisi bila sababu. Huwa nafarijika ninapoona angalau Magufuli ana- take action anapoona mambo kama hayo.
 
dega

dega

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Messages
1,958
Points
2,000
dega

dega

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2012
1,958 2,000
Kumbuka Nduli idd Amin mla nyama za watu aliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki

Magufuli kachaguliwa na Watanzania kwa mamilion ya kura

Muache kuropoka ropoka
Nyama ya nani aliila wacha kuwa kasuku fanya utafiti!!
 
Ndebile

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Messages
4,561
Points
2,000
Ndebile

Ndebile

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2011
4,561 2,000
nakumbuka ile siku Kikwete na genge lake waliposigina "Maoni ya Watanzania maarufu kama katiba ya Mzee Warioba" Karma is bit**ch! acha imtafune!
 
T

TruthLover

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Messages
671
Points
500
T

TruthLover

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2019
671 500
Hofu yangu ni baada ya magufuli in case kaja ambaye ni kinyume chake.Ni muhimu kama taifa tuwe na taasisi imara siyo 'mtu imara'.
Say it again and again. Tanzania ya sasa ni tofauti kabisa. Nidhamu imerudi maofisini. Angalau watumishi wa serikali wanaonyesha kujali. Wengi ya watu wanaopiga kelele ni baadhi ya wanasiasa na wafanya biashara. Hawa (wa upinzani na CCM) walikuwa wamezoea kuishi kwa kutumbua kodi zetu. Wafanyabishara nao baadhi walikuwa ndiyo wakwepa kodi wakubwa. Na baadhi ya wafanya kazi wa serikalini walikuwa na malipo mengi fake. Go Magufuli.
 
Ndebile

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Messages
4,561
Points
2,000
Ndebile

Ndebile

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2011
4,561 2,000
Kabisa, JK na kundi la wanaccm wenzake ndio walichezea mchakato wa katiba mpya akidhani, cheo cha urais ni kwa ajili ya kuwahujumu wapinzani tu. Leo anajifanya ana busara baada ya kila siku kuwa anatajwa kwa mafumbo kwamba ni mmoja ya marais walioingiza nchi kwenye mikataba ya wizi. JK akae atulie maana alipewa penalti akapaiza, sahii kabaniwa chini ndio anajifanya kutaka viongozi wasijikweze. Yeye ashawishi wenzake 2020 wampige jiwe chini na katiba ya rasimu ya Warioba ndio ishike hatamu.
Nakutumia ka vocha kidogo huko PM ni halotel, kama hutumii mtandao huo mgawie hata jirani yako! MAlipo ni hapa hapa duniani nadhani JK acha dawa imuingie na bado sana! R.I.P Sengondo Mvungi (1952 – 12 November 2013)
 
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Messages
935
Points
500
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2017
935 500
Ni kawaida

Power corrupts but absolute power corrupt absolutely. Viongozi wa Afrika wana absolute power hivyo hulewa madaraka na kuchanganyikiwa wanapokua madarakani. na viongozi wote wa Afrika hupata busara na hekima punde wanapoondoka madarakani. Wote

Afrika nzima serikali hazina sheria zenye nguvu wala taasisisi zenye nguvu bali kuna watu wenye nguvu waliolewa madaraka na suala hili ni kama kesi ya kuku na yai nani alianza kwanza. Mtu mwenye nguvu akileta katiba, sheria na taasisi zenye nguvu zitampunguzia nguvu zake yeye na chama chake na kuwaangusha. Again kuku na yai nani wakwanza alikua nani
Kuku na yai bado unajiuliza nini kilianza? Muwe munasoma vitabu kama Biblia ili kupata maarifa. Mungu hakuumba yai aliumba kuku. Therefore, kuku ndo wa kwanza kuwepo duniani. Period.
 
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Messages
935
Points
500
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2017
935 500
Say it again and again. Tanzania ya sasa ni tofauti kabisa. Nidhamu imerudi maofisini. Angalau watumishi wa serikali wanaonyesha kujali. Wengi ya watu wanaopiga kelele ni baadhi ya wanasiasa na wafanya biashara. Hawa (wa upinzani na CCM) walikuwa wamezoea kuishi kwa kutumbua kodi zetu. Wafanyabishara nao baadhi walikuwa ndiyo wakwepa kodi wakubwa. Na baadhi ya wafanya kazi wa serikalini walikuwa na malipo mengi fake. Go Magufuli.
Kwahiyo kwa sasahivi hakuna maisha ya kuigiza ni kuishi maisha halisi yakwako kabisa?
 
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Messages
1,365
Points
2,000
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2016
1,365 2,000
Ni kawaida

Power corrupts but absolute power corrupt absolutely. Viongozi wa Afrika wana absolute power hivyo hulewa madaraka na kuchanganyikiwa wanapokua madarakani. na viongozi wote wa Afrika hupata busara na hekima punde wanapoondoka madarakani. Wote

Afrika nzima serikali hazina sheria zenye nguvu wala taasisisi zenye nguvu bali kuna watu wenye nguvu waliolewa madaraka na suala hili ni kama kesi ya kuku na yai nani alianza kwanza. Mtu mwenye nguvu akileta katiba, sheria na taasisi zenye nguvu zitampunguzia nguvu zake yeye na chama chake na kuwaangusha. Again kuku na yai nani wakwanza alikua nani
Very think able-bodied.
Kikwete anajiona leo ana huruma. Wakati alikuwa kama magu tu, pengine zaidi
 
sheiza

sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Messages
4,308
Points
2,000
sheiza

sheiza

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2010
4,308 2,000
Kwa vile nchi ilifikia pabaya, unaamini ni sahihi kuwaonea watu, au hata kuwakomoa watu ambao kwa sababu zako tu huwapendi.

Rais alitamka, 'katika utawala wangu, tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote. Unaelewa utekelezaji wa kauli hiyo ulivyoleta madhira kwa baadhi ya watu, siyo kwa sababu wana makosa, bali kwa vile tu wanasadikika kuwa ni matajiri?
Umesahau wakati wa jk pia maskini alikuwa anaweza kufanywa kitu chochote na tajiri? Watu walivunjiwa nyumba na kuporwa maeneo kisha unaambiwa nenda popote. Jioni waporaji wanakunywa chai na jk.
 
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Messages
935
Points
500
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2017
935 500
Unachosema nakuunga mkono 100%, hii nchi ilifika mahali utadhani nchi haikua na Rais, watumishi hewa, ufisadi nk na tuliomba Mungu tupate rais mkali, na asiye safiri, Mungu ametujibu, cha msingi tumpe ushirikiano amalize miaka yake 10, kwa sasa wale wanaopiga kelele haita saidia, Magu ana mapungufu kama binadamu yoyote ila juhudi zake kila mtu anaziona, na sitegemei Magu atapendwa na kila mtu, huyu Nyerere watu wanaompamba leo hii alikua na maadui wengi kuliko unavyodanganywa na hapa ndipo ninajiuliza unafiki wa watanzania
Kwa huku Africa hasa Tz mtu mzuri ni yule aliemaliza muda wake wa utawala. Akiwa madarakani wengi tunatazama mapungufu yake na kubeza.
 
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Messages
935
Points
500
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2017
935 500
Mwalimu Nyerere baada ya kutoka madarakani alitamka kuwa Katiba ya Nchi yetu ni vema ikabadilishwa maana katiba hiyo inamfanya Rais awe dikteta. Ni katiba inayompa Rais madaraka makubwa kupindukia juu ya nchi na wananchi wake. Na akasema kuwa kama siku moja ikatokea mkampata Rais asiye na hekima, Taifa litapata shida sana.

Lakini jambo la kujiuliza, Mwalimu hakuona tatizo hilo la katiba alipokuwa madarakani bali tu pale alipoondoka madarakani? Na kama aliiona katiba yetu ni mbaya, kwa nini hakuongoza mchakato wa kuipata katiba mpya yenye kutoa madaraka makubwa kwa umma badala ya mtu mmoja tu Rais, ambaye ni binadamu kama walivyo wengine?

Kikwete, kwa msukumo wa vyama vya upinzani aliamua kuanzisha mchakato wa kuipata katiba mpya lakini ni kama hakuwa amedhamiria. Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana. Na hoja kubwa ilikuwa ni madaraka ya Rais kuwa yamekuwa makubwa mno kupindukia. Lakini pia wakuu wa mikoa na wilaya, hawakuwa na majukumu ya msingi. Na hawa ilielezwa kuwa kuwepo kwao ni matokeo ya utawala wa kikoloni ambapo walitumika kama vibaraka wa gavana. Kwa sasa hawana kazi, na nafasi zao ikapendekezwa na wengi, ziondolewe.

Hata baada ya mchakato wa kupata katiba mpya kuanza, mambo mengi yaliyopendekezwa na wananchi yaliondolewa kiasi cha kulifanya zoezi la kupata katiba mpya kukosa maana na hamasa.

Jana tumemsikia Kikwete akilalamikia watawala kujiona ni watu zaidi kuliko Raia wengine. Wanajimbafaimwambafai. Ukiyasikiliza kwa umakini maneno ya Kikwete, Butiku, Membe, Nape, January, Kinana na Makamba mzee, bila shaka wanajutia kwa kushindwa kuhakikisha kuna kuwepo na katiba nzuri inayoweza kudhibiti madaraka ya Rais na wasaidizi wake katika mambo ambayo ni kinyume na katiba na matarajio ya wananchi walio wengi hasa kwenye haki za msingi za Raia. Hawa hawakuiona haja hiyo walipokuwepo madarakani kwa sababu madaraka hayo ya kupindukia yaliwapa wao nguvu kubwa pale ambapo wangetaka kuyatumia hata kama hawakuyatumia. Sasa amepatikana wa kuyatumia, na hakuna wa kumfanya kitu maana katiba inampa madaraka ya kifalme.

Yalitokea pia Zambia. Kaunda alishauriwa na wapinzania wake, wapate katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais, hakutaka. Mungu si Athumani. Kaunda akaupoteza Urais. Chiluba akawa Rais. Chiluba akayatumia madaraka ya Rais kwa kadiri ya katiba ya Zambia, akamweka chini ya ulinzi Kaunda. Ashukuru busara za Mwalimu, aliyemwombea kwa Chiluba. Akaachiliwa.

Leo, Magufuli anafurahia sana madaraka anayopewa na katiba. Anayatumia kwa kadiri atakavyo. Hakuna wa kumgusa. Na ametamka kuwa katiba mpya kwake siyo kipaumbele, na kweli siyo kipaumbele maana iliyopo inampa nguvu za kifalme. Lakini asichokijua kuna siku watakuwepo wengine ambao nao watayapata mamlaka ya kifalme. Kwa madaraka hayo ya kikatiba, watamfanya nini yeye, sidhani anaona haja ya kulifikiria hilo maana mamlaka hupofusha.

Mwalimu ulijutia kwa kutokuwaletea katiba ya wananchi Watanzania. Kikwete anajisikitikia kwa kugeuza maoni ya wananchi na kuchelewesha upatikanaji katiba mpya. Magufuli naye atajutia?

Siku za nyuma, kwa marais waliofuatia, pamoja na uwepo wa katiba mbaya, hakuna aliyefikiria kutumia madaraka ya Urais kumsumbua Mwalimu kwa sababu tu Mwalimu alitumia zaidi hekima yake kuliko nguvu za katiba, wakati wa utawala wake. Hakuna aliyemsumbua Mwinyi, Mkapa wala Kikwete maana hawa wote hawakutaka kuzifurahia haki za kikatiba zinazomfanya Rais wetu kuwa mfalme.

Rais Magufuli anazifurahia na kuzitumia hasa haki za kikatiba zinazomfanya yeye na wasaidizi wake kuwa wafame. Je, ajaye atafurahia kama yeye? Na je, atafanya nini kwa yale yatakayothibitika kuwa utawala wa sasa haukuwatendea haki baadhi ya raia? Maana ni ukweli uliothabiti kuna watu wametengenezewa kesi za uhujumu uchumi kwa chuki. Kuna watu wametengenezewa kesi za utakatishaji fedha kwa chuki. Kuna watu wametekwa na kupotezwa. Kuna watu wamekubali kunyang'anywa mali zao halali ili tu wazirudie familia zao. Lakini pia kuna maamuzi yaliyotakiwa kufanywa kitaasisi yanafanywa na mtu mmoja au kikundi cha watu kinyume cha sheria.

Kama Mh. Rais ni muumini mzuri wa dini, atafakari mfano wa mtumishi aliyeambiwa atafukuzwa kazi, naye akaamua kuwaendea wote waliokuwa wakidaiwa, akaamua kuwapunguzia madai yao ili atakapoondolewa kazini awe na kundi kubwa la marafiki.

Mungu awajalie viongozi wetu hekima ili wawatendee watu wote haki bila ya kujali vyama vyao, dini zao, makabila yao, maeneo yao na jinsia zao maana ndivyo walivyoapa.
Mku weka namba ya simu nikupe voucha. Kweli umejipinda sana hapo mezani na computer yako ukatoa wazo zuri.
 
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Messages
1,365
Points
2,000
Lihakanga

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2016
1,365 2,000
Magu ni wazi huwa hatumii muda wake kuwaza ya kesho baada ya yeye kuondoka madarakani.
Unawaza kwa nyayo. Kikwete aliyewaza kustaafu ameleta maendeleo gani?

Ni lini tutakuwa wakweli? Kikwete mpole mno, Magufuli dikteta, Mkapa kauza nchi, Mchonga meno nchi imemshinda, Mwinyi kauza nchi.

Aje mungu basi aongoze nchi.
 
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Messages
935
Points
500
K

Kikiwo

JF-Expert Member
Joined Nov 30, 2017
935 500
Unawaza kwa nyayo. Kikwete aliyewaza kustaafu ameleta maendeleo gani?

Ni lini tutakuwa wakweli? Kikwete mpole mno, Magufuli dikteta, Mkapa kauza nchi, Mchonga meno nchi imemshinda, Mwinyi kauza nchi.

Aje mungu basi aongoze nchi.
Hata yeye akibahatika kupata tutalalamika vilevile hawezi kuturidhizisha wote watu Million 55 Tz
 
G

gabatha

Senior Member
Joined
Apr 6, 2012
Messages
122
Points
195
G

gabatha

Senior Member
Joined Apr 6, 2012
122 195
Jk ni mnafiki sana, alikuwa wapi asibadilushe katiba kuondoa huo UMungu mtu serikalini. Akae kimya tu
 
M

mputa

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2012
Messages
924
Points
1,000
M

mputa

JF-Expert Member
Joined Jun 11, 2012
924 1,000
Kwa huku Africa hasa Tz mtu mzuri ni yule aliemaliza muda wake wa utawala. Akiwa madarakani wengi tunatazama mapungufu yake na kubeza.
HUU NI UKWELI 1000%
 
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
3,850
Points
2,000
C

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
3,850 2,000
Rais hapangwi na mtu Rais huletwa na Mungu

Kwa nchi ilivyofikia 2015 Magufuli ndio alikuwa best choice

Tofauti na hapo nchi ingekuwa failed state kwa sasa

2015 Nchi ilikuwa shimoni,kongole kwa Magufuli kwa kuirejesha nchi pahala pake
Utakuwa unaumwa Mungu alete utekaji, uuaji, upotezaji watu, ufukara, umaskini wa kutupa, unanyasaji, ukiukaji wa haki za binadamu, Ukabila, ukanda, uvyama, ubambikiaji kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
 
Nyabutoro

Nyabutoro

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Messages
771
Points
1,000
Nyabutoro

Nyabutoro

JF-Expert Member
Joined Apr 8, 2017
771 1,000
Rais hapangwi na mtu Rais huletwa na Mungu

Kwa nchi ilivyofikia 2015 Magufuli ndio alikuwa best choice

Tofauti na hapo nchi ingekuwa failed state kwa sasa

2015 Nchi ilikuwa shimoni,kongole kwa Magufuli kwa kuirejesha nchi pahala pake
Mafirauni huletwa na shetani
 
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
11,587
Points
2,000
Odhiambo cairo

Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
11,587 2,000
Mwalimu Nyerere baada ya kutoka madarakani alitamka kuwa Katiba ya Nchi yetu ni vema ikabadilishwa maana katiba hiyo inamfanya Rais awe dikteta. Ni katiba inayompa Rais madaraka makubwa kupindukia juu ya nchi na wananchi wake. Na akasema kuwa kama siku moja ikatokea mkampata Rais asiye na hekima, Taifa litapata shida sana.

Lakini jambo la kujiuliza, Mwalimu hakuona tatizo hilo la katiba alipokuwa madarakani bali tu pale alipoondoka madarakani? Na kama aliiona katiba yetu ni mbaya, kwa nini hakuongoza mchakato wa kuipata katiba mpya yenye kutoa madaraka makubwa kwa umma badala ya mtu mmoja tu Rais, ambaye ni binadamu kama walivyo wengine?

Kikwete, kwa msukumo wa vyama vya upinzani aliamua kuanzisha mchakato wa kuipata katiba mpya lakini ni kama hakuwa amedhamiria. Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana. Na hoja kubwa ilikuwa ni madaraka ya Rais kuwa yamekuwa makubwa mno kupindukia. Lakini pia wakuu wa mikoa na wilaya, hawakuwa na majukumu ya msingi. Na hawa ilielezwa kuwa kuwepo kwao ni matokeo ya utawala wa kikoloni ambapo walitumika kama vibaraka wa gavana. Kwa sasa hawana kazi, na nafasi zao ikapendekezwa na wengi, ziondolewe.

Hata baada ya mchakato wa kupata katiba mpya kuanza, mambo mengi yaliyopendekezwa na wananchi yaliondolewa kiasi cha kulifanya zoezi la kupata katiba mpya kukosa maana na hamasa.

Jana tumemsikia Kikwete akilalamikia watawala kujiona ni watu zaidi kuliko Raia wengine. Wanajimbafaimwambafai. Ukiyasikiliza kwa umakini maneno ya Kikwete, Butiku, Membe, Nape, January, Kinana na Makamba mzee, bila shaka wanajutia kwa kushindwa kuhakikisha kuna kuwepo na katiba nzuri inayoweza kudhibiti madaraka ya Rais na wasaidizi wake katika mambo ambayo ni kinyume na katiba na matarajio ya wananchi walio wengi hasa kwenye haki za msingi za Raia. Hawa hawakuiona haja hiyo walipokuwepo madarakani kwa sababu madaraka hayo ya kupindukia yaliwapa wao nguvu kubwa pale ambapo wangetaka kuyatumia hata kama hawakuyatumia. Sasa amepatikana wa kuyatumia, na hakuna wa kumfanya kitu maana katiba inampa madaraka ya kifalme.

Yalitokea pia Zambia. Kaunda alishauriwa na wapinzania wake, wapate katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais, hakutaka. Mungu si Athumani. Kaunda akaupoteza Urais. Chiluba akawa Rais. Chiluba akayatumia madaraka ya Rais kwa kadiri ya katiba ya Zambia, akamweka chini ya ulinzi Kaunda. Ashukuru busara za Mwalimu, aliyemwombea kwa Chiluba. Akaachiliwa.

Leo, Magufuli anafurahia sana madaraka anayopewa na katiba. Anayatumia kwa kadiri atakavyo. Hakuna wa kumgusa. Na ametamka kuwa katiba mpya kwake siyo kipaumbele, na kweli siyo kipaumbele maana iliyopo inampa nguvu za kifalme. Lakini asichokijua kuna siku watakuwepo wengine ambao nao watayapata mamlaka ya kifalme. Kwa madaraka hayo ya kikatiba, watamfanya nini yeye, sidhani anaona haja ya kulifikiria hilo maana mamlaka hupofusha.

Mwalimu ulijutia kwa kutokuwaletea katiba ya wananchi Watanzania. Kikwete anajisikitikia kwa kugeuza maoni ya wananchi na kuchelewesha upatikanaji katiba mpya. Magufuli naye atajutia?

Siku za nyuma, kwa marais waliofuatia, pamoja na uwepo wa katiba mbaya, hakuna aliyefikiria kutumia madaraka ya Urais kumsumbua Mwalimu kwa sababu tu Mwalimu alitumia zaidi hekima yake kuliko nguvu za katiba, wakati wa utawala wake. Hakuna aliyemsumbua Mwinyi, Mkapa wala Kikwete maana hawa wote hawakutaka kuzifurahia haki za kikatiba zinazomfanya Rais wetu kuwa mfalme.

Rais Magufuli anazifurahia na kuzitumia hasa haki za kikatiba zinazomfanya yeye na wasaidizi wake kuwa wafame. Je, ajaye atafurahia kama yeye? Na je, atafanya nini kwa yale yatakayothibitika kuwa utawala wa sasa haukuwatendea haki baadhi ya raia? Maana ni ukweli uliothabiti kuna watu wametengenezewa kesi za uhujumu uchumi kwa chuki. Kuna watu wametengenezewa kesi za utakatishaji fedha kwa chuki. Kuna watu wametekwa na kupotezwa. Kuna watu wamekubali kunyang'anywa mali zao halali ili tu wazirudie familia zao. Lakini pia kuna maamuzi yaliyotakiwa kufanywa kitaasisi yanafanywa na mtu mmoja au kikundi cha watu kinyume cha sheria.

Kama Mh. Rais ni muumini mzuri wa dini, atafakari mfano wa mtumishi aliyeambiwa atafukuzwa kazi, naye akaamua kuwaendea wote waliokuwa wakidaiwa, akaamua kuwapunguzia madai yao ili atakapoondolewa kazini awe na kundi kubwa la marafiki.

Mungu awajalie viongozi wetu hekima ili wawatendee watu wote haki bila ya kujali vyama vyao, dini zao, makabila yao, maeneo yao na jinsia zao maana ndivyo walivyoapa.
Ni kweli tena ukweli mchungu. Kikwete alifanya unafki kuvunjilia mbali katiba ya wananchi. Na yote hii ilikuwa ni kulinda machafu haya tunayoambiwa sasa juu ya uongozi wake. Lakini pia kuilinda chama chake ili isitenganishwe na dola. Ili kuilinda kikundi kidogo cha watawala dhidi ya wananchi.

Hawa wa sasa wako kwenye pepo ya utawala . Wanachojuà wataishi milele
 
Countrywide

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Messages
3,700
Points
2,000
Countrywide

Countrywide

JF-Expert Member
Joined Mar 2, 2015
3,700 2,000
Ni kweli tena ukweli mchungu. Kikwete alifanya unafki kuvunjilia mbali katiba ya wananchi. Na yote hii ilikuwa ni kulinda machafu haya tunayoambiwa sasa juu ya uongozi wake. Lakini pia kuilinda chama chake ili isitenganishwe na dola. Ili kuilinda kikundi kidogo cha watawala dhidi ya wananchi.

Hawa wa sasa wako kwenye pepo ya utawala . Wanachojuà wataishi milele
Huu ubabe wa kuhoji hivi, mngekuwa nak huko chadema basi leo hii ingekuwa inatawala nchi na sio ccm
Mbowe kabadilisha katiba, anataka kutawala milele utafikiri hatakufa!
 
A

Arovera

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Messages
2,868
Points
2,000
A

Arovera

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2013
2,868 2,000
Jakaya atulie asiseme chochote yeye ni moja kati ya maraisi wabovu nchi hii atulie tu
 
Forum statistics

Threads 1,343,116
Members 514,943
Posts 32,774,403
Top