Majuto ni mjukuu, Kikwete ulikuwa na nafasi kutupatia Katiba Mpya

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
7,316
Points
2,000

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
7,316 2,000
Mwalimu Nyerere baada ya kutoka madarakani alitamka kuwa Katiba ya Nchi yetu ni vema ikabadilishwa maana katiba hiyo inamfanya Rais awe dikteta. Ni katiba inayompa Rais madaraka makubwa kupindukia juu ya nchi na wananchi wake. Na akasema kuwa kama siku moja ikatokea mkampata Rais asiye na hekima, Taifa litapata shida sana.

Lakini jambo la kujiuliza, Mwalimu hakuona tatizo hilo la katiba alipokuwa madarakani bali tu pale alipoondoka madarakani? Na kama aliiona katiba yetu ni mbaya, kwa nini hakuongoza mchakato wa kuipata katiba mpya yenye kutoa madaraka makubwa kwa umma badala ya mtu mmoja tu Rais, ambaye ni binadamu kama walivyo wengine?

Kikwete, kwa msukumo wa vyama vya upinzani aliamua kuanzisha mchakato wa kuipata katiba mpya lakini ni kama hakuwa amedhamiria. Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana. Na hoja kubwa ilikuwa ni madaraka ya Rais kuwa yamekuwa makubwa mno kupindukia. Lakini pia wakuu wa mikoa na wilaya, hawakuwa na majukumu ya msingi. Na hawa ilielezwa kuwa kuwepo kwao ni matokeo ya utawala wa kikoloni ambapo walitumika kama vibaraka wa gavana. Kwa sasa hawana kazi, na nafasi zao ikapendekezwa na wengi, ziondolewe.

Hata baada ya mchakato wa kupata katiba mpya kuanza, mambo mengi yaliyopendekezwa na wananchi yaliondolewa kiasi cha kulifanya zoezi la kupata katiba mpya kukosa maana na hamasa.

Jana tumemsikia Kikwete akilalamikia watawala kujiona ni watu zaidi kuliko Raia wengine. Wanajimbafaimwambafai. Ukiyasikiliza kwa umakini maneno ya Kikwete, Butiku, Membe, Nape, January, Kinana na Makamba mzee, bila shaka wanajutia kwa kushindwa kuhakikisha kuna kuwepo na katiba nzuri inayoweza kudhibiti madaraka ya Rais na wasaidizi wake katika mambo ambayo ni kinyume na katiba na matarajio ya wananchi walio wengi hasa kwenye haki za msingi za Raia. Hawa hawakuiona haja hiyo walipokuwepo madarakani kwa sababu madaraka hayo ya kupindukia yaliwapa wao nguvu kubwa pale ambapo wangetaka kuyatumia hata kama hawakuyatumia. Sasa amepatikana wa kuyatumia, na hakuna wa kumfanya kitu maana katiba inampa madaraka ya kifalme.

Yalitokea pia Zambia. Kaunda alishauriwa na wapinzania wake, wapate katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais, hakutaka. Mungu si Athumani. Kaunda akaupoteza Urais. Chiluba akawa Rais. Chiluba akayatumia madaraka ya Rais kwa kadiri ya katiba ya Zambia, akamweka chini ya ulinzi Kaunda. Ashukuru busara za Mwalimu, aliyemwombea kwa Chiluba. Akaachiliwa.

Leo, Magufuli anafurahia sana madaraka anayopewa na katiba. Anayatumia kwa kadiri atakavyo. Hakuna wa kumgusa. Na ametamka kuwa katiba mpya kwake siyo kipaumbele, na kweli siyo kipaumbele maana iliyopo inampa nguvu za kifalme. Lakini asichokijua kuna siku watakuwepo wengine ambao nao watayapata mamlaka ya kifalme. Kwa madaraka hayo ya kikatiba, watamfanya nini yeye, sidhani anaona haja ya kulifikiria hilo maana mamlaka hupofusha.

Mwalimu ulijutia kwa kutokuwaletea katiba ya wananchi Watanzania. Kikwete anajisikitikia kwa kugeuza maoni ya wananchi na kuchelewesha upatikanaji katiba mpya. Magufuli naye atajutia?

Siku za nyuma, kwa marais waliofuatia, pamoja na uwepo wa katiba mbaya, hakuna aliyefikiria kutumia madaraka ya Urais kumsumbua Mwalimu kwa sababu tu Mwalimu alitumia zaidi hekima yake kuliko nguvu za katiba, wakati wa utawala wake. Hakuna aliyemsumbua Mwinyi, Mkapa wala Kikwete maana hawa wote hawakutaka kuzifurahia haki za kikatiba zinazomfanya Rais wetu kuwa mfalme.

Rais Magufuli anazifurahia na kuzitumia hasa haki za kikatiba zinazomfanya yeye na wasaidizi wake kuwa wafame. Je, ajaye atafurahia kama yeye? Na je, atafanya nini kwa yale yatakayothibitika kuwa utawala wa sasa haukuwatendea haki baadhi ya raia? Maana ni ukweli uliothabiti kuna watu wametengenezewa kesi za uhujumu uchumi kwa chuki. Kuna watu wametengenezewa kesi za utakatishaji fedha kwa chuki. Kuna watu wametekwa na kupotezwa. Kuna watu wamekubali kunyang'anywa mali zao halali ili tu wazirudie familia zao. Lakini pia kuna maamuzi yaliyotakiwa kufanywa kitaasisi yanafanywa na mtu mmoja au kikundi cha watu kinyume cha sheria.

Kama Mh. Rais ni muumini mzuri wa dini, atafakari mfano wa mtumishi aliyeambiwa atafukuzwa kazi, naye akaamua kuwaendea wote waliokuwa wakidaiwa, akaamua kuwapunguzia madai yao ili atakapoondolewa kazini awe na kundi kubwa la marafiki.

Mungu awajalie viongozi wetu hekima ili wawatendee watu wote haki bila ya kujali vyama vyao, dini zao, makabila yao, maeneo yao na jinsia zao maana ndivyo walivyoapa.
 
Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
7,316
Points
2,000

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
7,316 2,000
Kwa vile nchi ilifikia pabaya, unaamini ni sahihi kuwaonea watu, au hata kuwakomoa watu ambao kwa sababu zako tu huwapendi.

Rais alitamka, 'katika utawala wangu, tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote. Unaelewa utekelezaji wa kauli hiyo ulivyoleta madhira kwa baadhi ya watu, siyo kwa sababu wana makosa, bali kwa vile tu wanasadikika kuwa ni matajiri?

Rais hapangwi na mtu Rais huletwa na Mungu

Kwa nchi ilivyofikia 2015 Magufuli ndio alikuwa best choice

Tofauti na hapo nchi ingekuwa failed state kwa sasa

2015 Nchi ilikuwa shimoni,kongole kwa Magufuli kwa kuirejesha nchi pahala pake
 
Ngwanakilala

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Messages
686
Points
1,000

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2011
686 1,000
Ni kawaida

Power corrupts but absolute power corrupt absolutely. Viongozi wa Afrika wana absolute power hivyo hulewa madaraka na kuchanganyikiwa wanapokua madarakani. na viongozi wote wa Afrika hupata busara na hekima punde wanapoondoka madarakani. Wote

Afrika nzima serikali hazina sheria zenye nguvu wala taasisisi zenye nguvu bali kuna watu wenye nguvu waliolewa madaraka na suala hili ni kama kesi ya kuku na yai nani alianza kwanza. Mtu mwenye nguvu akileta katiba, sheria na taasisi zenye nguvu zitampunguzia nguvu zake yeye na chama chake na kuwaangusha. Again kuku na yai nani wakwanza alikua nani
 
jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
21,264
Points
2,000

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
21,264 2,000
Mhn! Mada fikirishi hii. Anafahamu akitoka mapema na katiba hii wanaweza kupinduwa kila alichofanya na pengine uongozi wake kuwa matatani wakishaondoka madarakani... Nadhani hata Maghufuli mwenyewe keshafikiria hili ndo maana kuna dalili za kujiongezea muda kwa kubadili katiba. Yani kwa style hii inawezekana ana mpango wa kuwa rais maisha yake yote! Yani akistaafu aendelee kuishi na kuwa mkuu wa malaika”...Nadhani anaipenda katiba hii kasoro hapo kwenye ukomo wa kuongoza.
 
dega

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Messages
1,989
Points
2,000

dega

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2012
1,989 2,000
Rais hapangwi na mtu Rais huletwa na Mungu

Kwa nchi ilivyofikia 2015 Magufuli ndio alikuwa best choice

Tofauti na hapo nchi ingekuwa failed state kwa sasa

2015 Nchi ilikuwa shimoni,kongole kwa Magufuli kwa kuirejesha nchi pahala pake
Naaam kabisa kabisa hivi sasa Ben hasumbui tena Nzory kanyamaza Tundu hayupo tena Viongoz wa Chadema hawaondoi mguu mahakamani kila Leo Wabunge wa upinzani baada kuhongwa HELA na uongozi Leo wamekua wa bunge bila mchakato wa kura za maoni
HONGERENI
 
jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
21,264
Points
2,000

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
21,264 2,000
Kutakuwepo na mtifuano mkali sana huko ccm. Kuna wale wanaotaka katiba ya Warioba, halafu kuna wale wanaotaka katiba ibadilishwe ili rais aliyepo aendelee kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi. Ngoja tuone mchakato wao.

Ila watayakumbuka sana maneno aliyowahi kusema Lissu, maaana wakati upinzani unadhibitiwa, wao walisema “hao ni chadema sisi hatuna shida”
 
Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Messages
5,559
Points
2,000

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2019
5,559 2,000
Wabunge wa upinzani baada kuhongwa HELA na uongozi Leo wamekua wa bunge bila mchakato wa kura za maoni
HONGERENI
Kama kuna mtu amefikia level ya juu ya Uongozi km ubunge na anakubali kuhongwa pesa huyo utamwita mbunge?

Anyway this is conspiracy theories
 
Joined
Jun 25, 2019
Messages
46
Points
95
Joined Jun 25, 2019
46 95
Kwa vile nchi ilifikia pabaya, unaamini ni sahihi kuwaonea watu, au hata kuwakomoa watu ambao kwa sababu zako tu huwapendi.

Rais alitamka, 'katika utawala wangu, tajiri anaweza kufanywa chochote wakati wowote. Unaelewa utekelezaji wa kauli hiyo ulivyoleta madhira kwa baadhi ya watu, siyo kwa sababu wana makosa, bali kwa vile tu wanasadikika kuwa ni matajiri?
magufuri haonei watu isipokuwa kitu ambacho hujakierewa yeye ana pambana na mafisadi wara rushwa mabwenyenye nawasiyo ritakia mema taifa retu upo mukuu
 
Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
16,168
Points
2,000

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
16,168 2,000
Kutakuwepo na mtifuano mkali sana huko ccm. Kuna wale wanaotaka katiba ya Warioba, halafu kuna wanaotaka katiba ibadilishwe ili rais aliyepo aendelee kukaa madarakani kwa muda mrefu zaidi. Ngoja tuone mchakato wao.

Ila watayakumbuka sana maneno aliyowahi kusema Lissu, maaana wao walisema hao ni chadema sisi hatuna shida.
Mtifuano ndani ya CCM utaleta Tija sana kwa Tanzania yetu. Uongozi utakuwa ni wa vitendo na sio kulindana
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
4,750
Points
2,000

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
4,750 2,000
Mwalimu Nyerere baada ya kutoka madarakani alitamka kuwa Katiba ya Nchi yetu ni vema ikabadilishwa maana katiba hiyo inamfanya Rais awe dikteta. Ni katiba inayompa Rais madaraka makubwa kupindukia juu ya nchi na wananchi wake. Na akasema kuwa kama siku moja ikatokea mkampata Rais asiye na hekima, Taifa litapata shida sana.

Lakini jambo la kujiuliza, Mwalimu hakuona tatizo hilo la katiba alipokuwa madarakani bali tu pale alipoondoka madarakani? Na kama aliiona katiba yetu ni mbaya, kwa nini hakuongoza mchakato wa kuipata katiba mpya yenye kutoa madaraka makubwa kwa umma badala ya mtu mmoja tu Rais, ambaye ni binadamu kama walivyo wengine?

Kikwete, kwa msukumo wa vyama vya upinzani aliamua kuanzisha mchakato wa kuipata katiba mpya lakini ni kama hakuwa amedhamiria. Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana. Na hoja kubwa ilikuwa ni madaraka ya Rais kuwa yamekuwa makubwa mno kupindukia. Lakini pia wakuu wa mikoa na wilaya, hawakuwa na majukumu ya msingi. Na hawa ilielezwa kuwa kuwepo kwao ni matokeo ya utawala wa kikoloni ambapo walitumika kama vibaraka wa gavana. Kwa sasa hawana kazi, na nafasi zao ikapendekezwa na wengi, ziondolewe.

Hata baada ya mchakato wa kupata katiba mpya kuanza, mambo mengi yaliyopendekezwa na wananchi yaliondolewa kiasi cha kulifanya zoezi la kupata katiba mpya kukosa maana na hamasa.

Jana tumemsikia Kikwete akilalamikia watawala kujiona ni watu zaidi kuliko Raia wengine. Wanajimbafaimwambafai. Ukiyasikiliza kwa umakini maneno ya Kikwete, Butiku, Membe, Nape, January, Kinana na Makamba mzee, bila shaka wanajutia kwa kushindwa kuhakikisha kuna kuwepo na katiba nzuri inayoweza kudhibiti madaraka ya Rais na wasaidizi wake katika mambo ambayo ni kinyume na katiba na matarajio ya wananchi walio wengi hasa kwenye haki za msingi za Raia. Hawa hawakuiona haja hiyo walipokuwepo madarakani kwa sababu madaraka hayo ya kupindukia yaliwapa wao nguvu kubwa pale ambapo wangetaka kuyatumia hata kama hawakuyatumia. Sasa amepatikana wa kuyatumia, na hakuna wa kumfanya kitu maana katiba inampa madaraka ya kifalme.

Yalitokea pia Zambia. Kaunda alishauriwa na wapinzania wake, wapate katiba mpya itakayopunguza madaraka ya Rais, hakutaka. Mungu si Athumani. Kaunda akaupoteza Urais. Chiluba akawa Rais. Chiluba akayatumia madaraka ya Rais kwa kadiri ya katiba ya Zambia, akamweka chini ya ulinzi Kaunda. Ashukuru busara za Mwalimu, aliyemwombea kwa Chiluba. Akaachiliwa.

Leo, Magufuli anafurahia sana madaraka anayopewa na katiba. Anayatumia kwa kadiri atakavyo. Hakuna wa kumgusa. Na ametamka kuwa katiba mpya kwake siyo kipaumbele, na kweli siyo kipaumbele maana iliyopo inampa nguvu za kifalme. Lakini asichokijua kuna siku watakuwepo wengine ambao nao watayapata mamlaka ya kifalme. Kwa madaraka hayo ya kikatiba, watamfanya nini yeye, sidhani anaona haja ya kulifikiria hilo maana mamlaka hupofusha.

Mwalimu ulijutia kwa kutokuwaletea katiba ya wananchi Watanzania. Kikwete anajisikitikia kwa kugeuza maoni ya wananchi na kuchelewesha upatikanaji katiba mpya. Magufuli naye atajutia?

Siku za nyuma, kwa marais waliofuatia, pamoja na uwepo wa katiba mbaya, hakuna aliyefikiria kutumia madaraka ya Urais kumsumbua Mwalimu kwa sababu tu Mwalimu alitumia zaidi hekima yake kuliko nguvu za katiba, wakati wa utawala wake. Hakuna aliyemsumbua Mwinyi, Mkapa wala Kikwete maana hawa wote hawakutaka kuzifurahia haki za kikatiba zinazomfanya Rais wetu kuwa mfalme.

Rais Magufuli anazifurahia na kuzitumia hasa haki za kikatiba zinazomfanya yeye na wasaidizi wake kuwa wafame. Je, ajaye atafurahia kama yeye? Na je, atafanya nini kwa yale yatakayothibitika kuwa utawala wa sasa haukuwatendea haki baadhi ya raia? Maana ni ukweli uliothabiti kuna watu wametengenezewa kesi za uhujumu uchumi kwa chuki. Kuna watu wametengenezewa kesi za utakatishaji fedha kwa chuki. Kuna watu wametekwa na kupotezwa. Kuna watu wamekubali kunyang'anywa mali zao halali ili tu wazirudie familia zao. Lakini pia kuna maamuzi yaliyotakiwa kufanywa kitaasisi yanafanywa na mtu mmoja au kikundi cha watu kinyume cha sheria.

Kama Mh. Rais ni muumini mzuri wa dini, atafakari mfano wa mtumishi aliyeambiwa atafukuzwa kazi, naye akaamua kuwaendea wote waliokuwa wakidaiwa, akaamua kuwapunguzia madai yao ili atakapoondolewa kazini awe na kundi kubwa la marafiki.

Mungu awajalie viongozi wetu hekima ili wawatendee watu wote haki bila ya kujali vyama vyao, dini zao, makabila yao, maeneo yao na jinsia zao maana ndivyo walivyoapa.
JK alianzisha mchakato wa katiba, akausukuma mpaka rasimu ya Chenge (Japo haiko perfect lakini ni fair kuliko hii)

Ikawa imebaki phase ya kura ya maoni, ikashindikana kuifanya hiyo kura ya maoni kaa sababu ingecoincide na uchaguzi mkuu, mambo yangeingiliana sana na gharama ingekuwa kubwa kuendesha michakato miwili ambayo kila mmoja unahitaji ujisimamie.
 
mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
900
Points
1,000

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
900 1,000
Rais hapangwi na mtu Rais huletwa na Mungu

Kwa nchi ilivyofikia 2015 Magufuli ndio alikuwa best choice

Tofauti na hapo nchi ingekuwa failed state kwa sasa

2015 Nchi ilikuwa shimoni,kongole kwa Magufuli kwa kuirejesha nchi pahala pake
Mungu wa wapi alimleta Iddi Amin? Huenda huyo Mungu wa Iddy Amin ndio Mungu wa huyu mkuu wetu.
 
Forum statistics

Threads 1,378,783
Members 525,187
Posts 33,724,331
Top