Majungu ofisini....surviving

Majungu ofisini....surviving

madame x mbina unalea maradhi????

Niliwahi kukutana na hali hiyo.......

Mbaya zaidi bosi anapenda majungu usipime....

Nilichofanya niliwaita wote wawili bi shosti chaumbea na bosi nikatoa yangu ya rohoni with evudence na kupiga biti sitaki kupikiwa majungu tena....toka hapo hzta wakiniteta walikuwa wanahakikisha sitokuja kusikia....
 
Last edited by a moderator:
Wandugu Hamjambo....jamani hebu nisaidieni vipi niweze kuishi na watu wa majungu ofisini, kuna huyu jamaa yuko imara kuona makosa na kuyafikisha kwa Boss hata kama madogo madogo ili mradi nisiheme kwa raha.

Maaana hizi offfice politics siziwezi na wala sijazizoea.

Aisee hamna kitu kinaudhi kama majungu ofisini..yaani ukiamka asubui hutaki ufike haraka...inakua kama mtoto mdogo na shule.....mimi sasa ivi naomba Mungu nijiajiri tu.
Hapa kwetu tulikua na mswahili kijana mdogo tu..... sasa ofisi ina mademu wakali....basi kajamaa kenyewe kakija lazima kamchague mtu wa kumuoshea....anaweza akakutoa nishai ili mademu wasikie.....ukiwanya vizuri atahakikisha anakuchafulia basi tu...
Kama alivyosema Lara 1....tukatengenza kaumoja ketu tukamtengenezea JUNGU KUUU......akapigwa chini... sasa tuna mmama wa kizungu...yaani hana noma mpaka pombe ameweka ofisini kwake...full kujiachia....
 
afu tricky nayoipenda ni kutoonesha nimeudhika hata kama anayenipiga jungu kaniudhi

kutoonesha kama umekereka inasaidia sana, huwa inawakonfyuzi.


Inabidi kujifunza hii trick...kuna watu wanaenjoy suffering of others na mimi likinikera siwezi kujicha. Nitaanza kujirekebisha na hili.
 
Wandugu Hamjambo....jamani hebu nisaidieni vipi niweze kuishi na watu wa majungu ofisini, kuna huyu jamaa yuko imara kuona makosa na kuyafikisha kwa Boss hata kama madogo madogo ili mradi nisiheme kwa raha.

Maaana hizi offfice politics siziwezi na wala sijazizoea.
MadameX funga kwa wiki moja, mkabidhi Mungu ashughulike nae.
 
Last edited by a moderator:
Inabidi kujifunza hii trick...kuna watu wanaenjoy suffering of others na mimi likinikera siwezi kujicha. Nitaanza kujirekebisha na hili.


mie wameshanisema/pika majungu mpaka wamechoka aisee, na sitaki mazoea zaidi ya kikazi, nikiona unaniletea uswahili nakuchunia kabisa, nakupita koridoni kama sijawahi kukuona vile, nina sijui roho ngumu au ngozi ngumu, mie semaaa/pika majungu weeee sijawahi kuuliza lolote, sana sana nakuchunia tu, nilifunga mwaka na bifu la kutosha na FM, nani anataka ujinga, ninaoenda nao sawa poa, we ukiona nyamayao hivi na vile, pita hivi mana huniongezei siku za kuishi, nina amani kichizi!
 
Rekebisha my dear
Kama huwa unaonyesha unakereka basi utakufa kwa presha

Mie nina uwezo wa kuudhiwa na kujidai sijaudhika mkubwa sana
Inamfanya mtu ajione mjinga kwa kuwa hujali anayoyafanya

Inabidi kujifunza hii trick...kuna watu wanaenjoy suffering of others na mimi likinikera siwezi kujicha. Nitaanza kujirekebisha na hili.
 
Wandugu Hamjambo....jamani hebu nisaidieni vipi niweze kuishi na watu wa majungu ofisini, kuna huyu jamaa yuko imara kuona makosa na kuyafikisha kwa Boss hata kama madogo madogo ili mradi nisiheme kwa raha.

Maaana hizi offfice politics siziwezi na wala sijazizoea.

Potezea tu
 
Umbea na fitna kwa mwanaume aisee...yaani siwezi amini hawa wanaume wakoje, angefanya mwanamke nisingeshangaa

Wanabembeleza vyeo....ila ana bahati kama ningekuwa nae ofisi moja loooh! ningejitoa mhanga nimpe kavu kwani riziki ya mtu haipangwi na binadamu
 
Kwanza pole sana kwa mkasa huo,lakini pia the best way ni kuwa kimya na kufanya mambo yako kwa ufanisi wa hali ya juu.Yaani instead of meeting the deadline just be ahead of schedule.Watakushangaa na roho zao mbaya, pia ukiona hivo hiyo ofisi ni either imeajiri watu wengi wa kabila moja, ama imeajiri vihiyo kwa hiyo kuwaziba mdomo ni kupiga kazi kwa sana na achana na mambo ya kusocialize mpaka hapo utakapomjua mtu kwa undani.Pole ni mtihani tu lakini yanapita maana hata mimi nimekaa kwenye ofisi yenye majungu kwa miezi mitatu sasa lakini kwangu wamechemsha maana naonea kazi tu basi

Vihiyo zaidi, wana-survive kwa majungu.
 
Hivi huko unaishi hakuna mafundi wa kushusha watu VIBUSHA????
Try hiyo plan, kwa kuanzia unampa kabusha kadogo dogo...mwambie FUNDI, huyo mkuda jinsi atavyoongeza majungu basi na kabusha kaongezeka kama PIRA linalojazwa pumzi...
 
This dude has said it all..try this i guess it wanna help somehow....


Just keep it to yourself.

Ensure you do what you are supposed to do. Don't deviate from the SOP.

Always strive to get it right the first time.

Keep it professional. If possible don't fraternize with your co-workers.

Don't open up about your personal life because the more you do that the more you invite 'majungu'.

Last but not least, learn or try hard to overlook petty things.
 
Duh, sasa mie anaenipigia majungu kwao sumbawanga. Nikileta za kuleta si atanigeuza makalio mbele manyonyo nyuma?
Hivi huko unaishi hakuna mafundi wa kushusha watu VIBUSHA????
Try hiyo plan, kwa kuanzia unampa kabusha kadogo dogo...mwambie FUNDI, huyo mkuda jinsi atavyoongeza majungu basi na kabusha kaongezeka kama PIRA linalojazwa pumzi...
 
I hate my step mother! Kwa nini akili yako fupi kama yangu yaani? Leo mwenzio mpika jungu hajakuja kwa ofisi. Najitanua tu mie hehehe.
Rekebisha my dear
Kama huwa unaonyesha unakereka basi utakufa kwa presha

Mie nina uwezo wa kuudhiwa na kujidai sijaudhika mkubwa sana
Inamfanya mtu ajione mjinga kwa kuwa hujali anayoyafanya
 
MadameX - Wapotezee - I was told that we should appreciate those that are jealous of us cause they are the ones who think that we are better than them :wink:
 
Last edited by a moderator:
Majungu dawa yake ugeuke JUNGUUUU KUUUU!!!!!!!! Hahahaaaaaaaaaaaaa! Kuna mtu kapigwa transfer ya Mwanza kwa ajili ya Majungu.com afu busy kabisaa anajiandaa kuhama! Akaja kuniaga Kubwa la Maadui!Nikamwambia embu kafunguliwe kesi ya Madai hapo kisutu kwa hakimu mkazi fatsaaaa! Ukiwa na kesi huwezi hama coz kesi si inatajwa tajwa???? Hivo mlalamikiwa/Mdaiwa inabidi uwe unaattend mahakamani kufuatilia kesi yako! Utahama vipi na kesi ya madai?????? Miaka 5 hadi kesi ije iishe si ushaaresign na kazi kitambo!!!!!!!Basi ndo cousin wake kamfungulia kesi ya madai ya Million Moja taslimu! Hahahahahaaaaaaaaa!!!!!!!! Mjini mipango! Kuattatch documents na email ya uhakika, transfer kapewa mwingine! MJINI MIPANGO!!!!! La sivo Kwisha Habari Yake! (Japo keshaingia kwenye judiciary system data base!)

What an advise! Kweli wewe ni KUBWA LA MAADUI! BANDIDU WA BANDIDU! Lol!
 
wajinga km hao dawa yao ni kuwapotezea tu maana ukiamua kuwafatilia ndo unawapa nafasi ya kukusema zaidi.
Achana nao wajinga hao isitoshe inaonekana ht elimu zao hazijawasaidia.
 
Kwa upande wangu huwa sina subra wala uwezo wa kumvumilia mtu mwenye majungu, huwa siangalii sura yake, umri, jinsia wala rangi, namfva mchan wa juakali na kumpa makavu awe peke yake au mbele za watu baada ya hapo natulia, tena namwambia na hili kaliseme kwa boss. Siku nyingine akitaka kuleta umbea atajifikiria mara sabasaba
 
Umeona eeh. Ukikasirika unawapa ushindi. Nilijiskia kichwa tu kuuma nikanywa maji kibao na kujiambia i got a pizza on my plate, time to eat niachane na nzi. Aaah, nawaachia vumbi mie, sina machejo! Tena mmoja namuambia lets go lunch, akachomoa. Si nimeenda regular lunch place na mshkaji mwingine nikamkuta. Tukakaa nae. Nashangaa hakukabwa na thamaki hehehe

Mmh ama unajua kutesa mtu, angekwamwa mwenzio?
 
Wandugu Hamjambo....jamani hebu nisaidieni vipi niweze kuishi na watu wa majungu ofisini, kuna huyu jamaa yuko imara kuona makosa na kuyafikisha kwa Boss hata kama madogo madogo ili mradi nisiheme kwa raha.

Maaana hizi offfice politics siziwezi na wala sijazizoea.


Kuna sababu tofauti tofauti zinazosababisha watu wapike majungu
mojawapo ni kuwa inwezekena wanaokupigia majungu 'hawakufahamu vizuri'
wanakuchukulia poa
so sometimes kuwa invite a bit in your life inasaidia kuwa neutralize
mfano watu wanakuona labda una shida sana na hiyo kazi,kumbe wewe uko vizuuri mno na unaweza kuishi bila hata hiyo kazi
watu dizaini hii unatakiwa siku moja unawaalika hata kwenye 'sherehe za kwenu'
akupate pate wewe ni nani na it helps kwa wengine...

But the best way ya ku deal na majungu ni kutumia formula inaitwa
'Ninaongea na mwenye mbwa' siongei na mbwa'

wewe una deal na Boss personally...unamsoma weakness zake
unajua his fears,his plans..na wewe unajitahidi unaakuwa 'mtu wa yeye kukutegemea'
sio wewe umtegemee.....huku wapika majungu una deal nao kimya kimya
kwa kuwapiga vita bila kuongea kitu...
 
Back
Top Bottom