Majungu ofisini....surviving

MadameX

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2009
Posts
7,792
Reaction score
3,860
Wandugu Hamjambo....jamani hebu nisaidieni vipi niweze kuishi na watu wa majungu ofisini, kuna huyu jamaa yuko imara kuona makosa na kuyafikisha kwa Boss hata kama madogo madogo ili mradi nisiheme kwa raha.

Maaana hizi offfice politics siziwezi na wala sijazizoea.
 
umbea ofisini kitu cha kawaida madame!!!!!! we kuwa bize na mambo yako tu......
kuna mwanaume moja ofisi flani ni mmbea zaidi ya maelezo yani hata meseji tukichati anafoward kwa boss, sielewi huwa anamaanisha nini!!!
 

Huyo anajambo anakutafuta...!
Labda ni yeye mwenyewe au katumwa na huyo boss...`
Chukua tahadhari mapema
 

Just keep it to yourself.

Ensure you do what you are supposed to do. Don't deviate from the SOP.

Always strive to get it right the first time.

Keep it professional. If possible don't fraternize with your co-workers.

Don't open up about your personal life because the more you do that the more you invite 'majungu'.

Last but not least, learn or try hard to overlook petty things.
 
umbea ofisini kitu cha kawaida madame!!!!!! we kuwa bize na mambo yako tu......
kuna mwanaume moja ofisi flani ni mmbea zaidi ya maelezo yani hata meseji tukichati anafoward kwa boss, sielewi huwa anamaanisha nini!!!
Umbea na fitna kwa mwanaume aisee...yaani siwezi amini hawa wanaume wakoje, angefanya mwanamke nisingeshangaa
 
Huyo anajambo anakutafuta...!
Labda ni yeye mwenyewe au katumwa na huyo boss...`
Chukua tahadhari mapema

Anataka kuhakikisha I am not fit for the job
 
wewe usifuatilie kama kasema au la maana na yenyewe ndio itakauwa majungu plus, maana unakuta labda na wewe unajihisi umesemewa, kumbe hamna kitu, utazidisha majungu, cha kufanya subiri boss atakapokuambia live jaribu kumconfront huyo jamaa face to face tena ikiwa mbele za watu wengine na huyo boss ndio nzuri zaidi, panga maneno ya kumpa live lakini katika tone nzuri. Ila kubwa zaidi jitahidi usifanye makosa hata madogo madogo uliyosema kwa kweli utamuweza!
 

I am trying hard to get it right to avoid further disappointment, yaani mpaka some senior chap in the company kanifata kuchukua tahadhari jamaa anachonga ila mbaya.

Good thing we don't discuss personal issues and every petty thing bothers me
 
Majungu dawa yake ugeuke JUNGUUUU KUUUU!!!!!!!! Hahahaaaaaaaaaaaaa! Kuna mtu kapigwa transfer ya Mwanza kwa ajili ya Majungu.com afu busy kabisaa anajiandaa kuhama! Akaja kuniaga Kubwa la Maadui!Nikamwambia embu kafunguliwe kesi ya Madai hapo kisutu kwa hakimu mkazi fatsaaaa! Ukiwa na kesi huwezi hama coz kesi si inatajwa tajwa???? Hivo mlalamikiwa/Mdaiwa inabidi uwe unaattend mahakamani kufuatilia kesi yako! Utahama vipi na kesi ya madai?????? Miaka 5 hadi kesi ije iishe si ushaaresign na kazi kitambo!!!!!!!Basi ndo cousin wake kamfungulia kesi ya madai ya Million Moja taslimu! Hahahahahaaaaaaaaa!!!!!!!! Mjini mipango! Kuattatch documents na email ya uhakika, transfer kapewa mwingine! MJINI MIPANGO!!!!! La sivo Kwisha Habari Yake! (Japo keshaingia kwenye judiciary system data base!)
 
Kwanza pole sana kwa mkasa huo,lakini pia the best way ni kuwa kimya na kufanya mambo yako kwa ufanisi wa hali ya juu.Yaani instead of meeting the deadline just be ahead of schedule.Watakushangaa na roho zao mbaya, pia ukiona hivo hiyo ofisi ni either imeajiri watu wengi wa kabila moja, ama imeajiri vihiyo kwa hiyo kuwaziba mdomo ni kupiga kazi kwa sana na achana na mambo ya kusocialize mpaka hapo utakapomjua mtu kwa undani.Pole ni mtihani tu lakini yanapita maana hata mimi nimekaa kwenye ofisi yenye majungu kwa miezi mitatu sasa lakini kwangu wamechemsha maana naonea kazi tu basi
 
Coincidentally leo i walked into the office kuna mtu anamalizia kunisema na kapromo kangu. Nikamsalimia tu na kumuambia umependeza. All smiles nikaingia kukaa na business as usual. Nimemuachia homework kutwa nahisi kama nimesikia ama la? Hahaha. NN kasema vema, keep your butt clean all the time na weka records zako sawasawa. Outsmart them, kabla hawajafika wakukute na kiti ushapata.
 
Huyo mwanaume ukimfuatilia sana uwezo wake wa kitandani ni mdogo...
Nilishaambiwa hivyo na bosi wangu wa kwanza
 
::
Ukiona mtu anakufuatilia maisha yako ujue kuna kitu umemzidi,,timiza wajibu wako kila ofisi wapo watu wa aina hii.
=
 
afu tricky nayoipenda ni kutoonesha nimeudhika hata kama anayenipiga jungu kaniudhi

kutoonesha kama umekereka inasaidia sana, huwa inawakonfyuzi.

Na kama una mipango ni kuipanga kimya kimya tu

 
Umeona eeh. Ukikasirika unawapa ushindi. Nilijiskia kichwa tu kuuma nikanywa maji kibao na kujiambia i got a pizza on my plate, time to eat niachane na nzi. Aaah, nawaachia vumbi mie, sina machejo! Tena mmoja namuambia lets go lunch, akachomoa. Si nimeenda regular lunch place na mshkaji mwingine nikamkuta. Tukakaa nae. Nashangaa hakukabwa na thamaki hehehe
afu tricky nayoipenda ni kutoonesha nimeudhika hata kama anayenipiga jungu kaniudhi

kutoonesha kama umekereka inasaidia sana, huwa inawakonfyuzi.

Na kama una mipango ni kuipanga kimya kimya tu
 
he he he, basi mie ndio napendaga hizo

unakuta wanakuteta afu huulizi wala nini?

Ila kuna siku naweza watupia dongo wakabanwa na mashati mie nasepa.

Kuna mmoja niliondoka mahali, siku naondoka hadi akatoa machozi, nikajiambia lol

nilikuwa namnyima raha sana mbaba huyu.

 
... keep your butt clean all the time na weka records zako sawasawa. Outsmart them, kabla hawajafika wakukute na kiti ushapata.
true true

afu tricky nayoipenda ni kutoonesha nimeudhika hata kama anayenipiga jungu kaniudhi

kutoonesha kama umekereka inasaidia sana, huwa inawakonfyuzi.

Na kama una mipango ni kuipanga kimya kimya tu
mshikaji wangu ananiambia niwapotezee tuu, mwenyewe ataona aibu utakampomkaushia. lakini wanaume tumebaki wachache, wanapiga majungu kama mademu :angry:.
 
siku hizi waika majungu mashuhuri ni wanamme

hasa ukute mtu mzima na vidato havijapanda sana anatumia tu uzoefu

anaweza pika majungu hadi mdomo ukawa mrefu kama kibuyu tena bila aibu.

Potezea tu, ila kuwa makini na kazi zako tu.

mshikaji wangu ananiambia niwapotezee tuu, mwenyewe ataona aibu utakampomkaushia. lakini wanaume tumebaki wachache, wanapiga majungu kama mademu :angry:.
 
siku hizi waika majungu mashuhuri ni wanamme

hasa ukute mtu mzima na vidato havijapanda sana anatumia tu uzoefu

anaweza pika majungu hadi mdomo ukawa mrefu kama kibuyu tena bila aibu
.

Potezea tu, ila kuwa makini na kazi zako tu.
kha!! kumbe mie nime-retain sifa zinazokubalika, nashukuru sijafikia huko. dawa yao ni kupiga kazi na kujiendeleza, watabaki peke yao as everybody moves ahead in life except them
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…