Majungu kazini yamekua shombo ya samaki feri

Majungu kazini yamekua shombo ya samaki feri

Dashy 99

Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
23
Reaction score
9
jamani wanajamii wenzangu kazi tutafute ila tujipange na majungu ya humo ofisini,mtu akitoka kidogo anaanza kupigwa vijembe,alafu wewe mgeni unafikilia mmh na mimi nikitoka kumbe ndio inavyokuwa.sijui dawa ya majungu nini mana watu wanavyo jifanya wanamjua bosi kwa sana na wewe mgeni ukae chonjo.mmh tutafika ivyo ivyo ila tutakuwa tumechoka sana.

Hivi haya majungu na masufulia ni ofisini kwangu tu au kote jamani mana yamezidi?:bange:
 
majungu yapo kuanzia ngazi ya familia, makazini hadi makanisani na misikitini, hayakwepeki na wala YASIKUTISHE!!.
 
Ukiona hivo ujue unafanya kazi na darasa la saba ama wanaojifanya wamesoma kumbe wameiba vyeti, pole sana hata mimi kuna jamaa nakofanya kazi tokea day 1 naripoti yeye ni kunipinga tu, kwa kuwa sisi ni wazee wa MOSAD na CIA nikamchimbua vilivyo ndani ya siku mbili nimeshamfahamu nje ndani amejifanya amesomea sijui Learn IT kuanzi diploma kumbe wizi mtupu.Akiendelea tu naweka mambo hadharani asitake kucheza na maisha ya watu
 
Ukiona hivo ujue unafanya kazi na darasa la saba ama wanaojifanya wamesoma kumbe wameiba vyeti, pole sana hata mimi kuna jamaa nakofanya kazi tokea day 1 naripoti yeye ni kunipinga tu kisa eti nimeajiriwa mimi wakati yeye amekaimu nafasi hiyo for so long time eti lkn yeye hajapewa, kwa kuwa sisi ni wazee wa MOSAD na CIA nikamchimbua vilivyo ndani ya siku mbili nimeshamfahamu nje ndani amejifanya amesomea sijui Learn IT kuanzi diploma kumbe wizi mtupu.Akiendelea tu naweka mambo hadharani asitake kucheza na maisha ya watu
 
Tatizo kubwa makazini ni wale watu wanaoletwa na vimemo hau ndio chanzo kikuu chaa matatizo makazini, wao hutengeneza mtandao na ndugu zao waliowaleta kazini na kupewa kipaumbele kwa kila fursa hao wasio na ndugu wanabaki wanaumia nakuchukia kazi!
 
Kuna wengine watakuloga au kuchafua nyota yako kabisa. We usiache kusali maana hali ni mbaya kwakweli
 
Hayo mambo serikalini ndo usiseme kazi haziendi kisa majungu.

Madogo kazeni mpate kazi kwenye corpolate world, majungu yataanzia wapi.. Although kuna stress za kazi za presha but dissapora hawajui majungu zaidi ya mchaka mchaka tu wa kazi..

Nina office mates wangu kazaa hawaongei na mtu zaidi ya hi tu mkikutana.. Watu wameshakaa sana majuu huko mda wa majungu watautoa wapi... Wao wanachojua ni maisja yao tu.

Mtu anafanya kazi mda wote, akichoka au kazi zikiisha anachezea I pad yake.. Hakuna stories na mtu.
Mwanzo nilisema watu wanaringa sana kumbe ndo maisha waliyoyazoea pande za north america and europe so wata wakirudi bongo hawataki kujuana juana..

Sisi wa vyuo vya kata kama kawa kupiga majungu
 
Dawa yao hao ni kuwapotezea tu...yaan we jidai hujali mwisho wa siku utaona wataacha wenyewe. Mm hapa ofisini kwetu hiyo tabia ipo sana tena boss ndo anaendekeza sn hz mambo za majungu, basi niliporipot kazini na kumsoma nikajidai sijali japo wakati mwingine vinauma ila nilikomaa na msimamao wangu....na sasa wameona sijali hadi wameacha wenyewe!!!!!!
 
we bwana fanya kazi kama hayo ni majungu wewe si msomi bwana...yatakusaidia nini?ukijali utaacha kazi bila kupenda yani cha msingi wewe ni kupotezea mana na wewe ukianza majungu hapo ndo bas tena
 
Hao wanaokupiga majungu jua kwamba wameajiriwa kama wewe hawatafanya lolote, hawawezi kukufukuza kazi wala nn, wewe umeajiriwa kama wao na umeajiriwa kwa kushinda katika interview, fanya kila ambacho mwajiri wako anategemea umfanyie angali your JD(job description). Watachoka wenyewe na watanyamaza.
 
Hizo zitakua ni kazi za serikali ndio zenye watu wapuuz kama hao,huku private ni kazi tu,majungu utayafanyia nyumbani kwako ukiwa na mkeo.
 
Weee acha kabisa, kuna ofisi moja hiyo wapiga majungu ndio dili, wale wanaojitia wanajua kazi mbona inakula kwao!
 
Kweli majungu ni wale wanaopata kazi kwa vimemo,mimi nilikuwa nafundisha shule moja maarufu sana hapa dar ipo Tabata ya Munyambo wa Karagwe,sasa pale walimu kwa primary nilikokuwa karibia 86 percent ni wanyambo,na cha kushangaza wewe unaweza ukaja pale kuomba kazi interview ukapgwa ya darasani na ukapewa mtihani,lakini baada ya siku akaja mwenzio mkakutana darasani hakuna cha interview hasa wa karagwe.Sasa wale jamaa wana mtandao na mwenye shule hata ukiugua jipu matakoni watamwambia boss.Wao ndo wanjifanya wanajua kufundisha na kuripoti wasi jua kazi,n.k.Sasa mie kipindi kile ndo nina bachelor yangu na wakaniweka primary nkaona hapa nikuharibiana C.V nkaondoka zangu nipo serikalini .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom