tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,494
MAJUKUMU YA MSINGI YA JESHI LA KUJENGA TAIFA -JKT
1. Malezi ya Vijana
Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kasumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (Nationa Service Act) ambayo ni sheria No 16 ya mwaka 1964. Sheria hii inatoa uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kuandikisha vijana wa kulitumikia Jeshi hilo. Aidha, sheria hii imeendelea kufanyiwa marekebisho kutokana na mahitajio.
Jeshi la Kujenga Taifa limekuwa chimbuko la kuandaa vijana kuajiriwa na vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini kama JWTZ, Polisi, Magereza, Usalama wa Taifa na taasisi binafsi za ulinzi. Hivyo Jeshi la Kujenga Taifa linachukua vijana wa kujitolea na mujibu wa sheria.
Kuanzishwa kwa JKT, kulitokana na mawazo ya Umoja wa Vijana wa Chama cha TANU (TANU Youth League), katika Mkutano wao Mkuu uliofanyika mjini Tabora tarehe 25 Aug 62, chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja huo, hayati Joseph Nyerere.
Kwenye uzinduzi wa JKT, Mwalimu Nyerere alisema Umuhimu wa JKT unatokana na Taifa kuhitaji huduma ya vijana na vijana kuitikia wito huo wa kulitumikia Taifa lao kwa jukumu lolote lihitajiwalo.
1. Malezi ya Vijana
- Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato
- Kupenda kazi za mikono.
- Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
- Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.
- Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
- Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbalimbali.
Ili kuwafanya vijana wa kitanzania waepukane na kasumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKT linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKT. Uzalishaji mali unaofanywa na JKT ni pamoja na:-
- Kujenga na kukarabati majengo
- Viwanda na Kilimo
- Madini na Nishati
- Utalii
- Ulinzi kwa Taasisi binafsi (Security Guard Services)
- Maduka (Super Market)
- Kuunganisha magari na mitambo
- Huduma za elimu