Majukumu ndani ya nyumba. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majukumu ndani ya nyumba.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jaguar, May 4, 2011.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ndani ya nyumba,mume na mke wote mmeajiriwa na kila mmoja ana kazi yake.Inawezekana mshahara wa mume ukawa mkubwa kuliko wa mke au vice versa.Nimekuwa nikisikia akina mama wengi wakisema,mshahara wa mume ndo kila kitu,kuanzia matumizi madogo madogo ndani ya house mpaka yale makubwa ya kimaendeleo,mshahara wa mke hauhusiki,ana uhuru wa kuutumia atakavyo tena bila kuhojiwa.Hili swala limekaaje au ndo utamaduni wetu wa Tanzania?
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  mwanaume ndio kichwa cha nyumba_remember!,....hata hivyo kusaidiana muhimu
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Huo utamaduni unatumika kwa baadhi,sioni tatizo kama mwanaume ana uwezo au ameridhia hilo lifanyike.Nafikiri si sahihi kumuachia majukumu ya kifedha mwanaume unless kama situation ya mume ni mtu kama Mengi na mke ni mwalimu wa primary,otherwise ushirikiano ni muhimu kutegemea na kipato....
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Familia ni two way traffic,mnatengeneza budget na mnaiwezesha kwa pamoja kutokana na kilichopo.Km mama anategea na ana kipato hiyo ni policy yenu.
   
 5. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hayo maneno,kama mimi ndo kichwa cha nyumba inamaanisha ninajukumu la ku control everything in the house mpaka vipato vyetu sote wawili.
   
 6. KWI KWI

  KWI KWI JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Baba katika nyumba....hatambuliki kwa jina bali kwa majukumu yake.Pia makubaliano katika nyumba ni jambo la watu wawili...sababu shughuli za kuendeleza familia hazina ''nembo'' kwamba hizi ni za mama hizi ni za baba.
   
 7. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye bluu ni sahihi kabisa, otherwise unasaidiwa tu, Lakini mwisho wa siku zengwe likiibuka mnagawana mali sawa kwa sawa! upo hapo kaka? that is life.
   
 8. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni sahihi au ndivyo ilivyo?,mi naona si sahihi ila haikwepeki!
   
 9. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Majukumu kusaidiana jamani.
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Haki zinakwenda pamoja na wajibu! Lazima kuwepo na balance kuhusu haya mambo mawili. Huwezi kuchukua moja ukaacha jingine.
   
 11. N

  Ngo JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Elia;1930233]Hapo kwenye bluu ni sahihi kabisa, otherwise unasaidiwa tu, Lakini mwisho wa siku zengwe likiibuka mnagawana mali sawa kwa sawa! upo hapo kaka? that is life.

  Kama ni kusaidiwa utasaidiwa tu kaka haijalishi unatowa pesa ya kutosha au hapana. Ni wangapi wana kila kitu katika familia zao nikimaanisha mali lakini wanasaidiwa?

  Zaidi mimi Naona ni makubaliano mlio nayo kwenye ndoa yenu. Kuna wengine wanapenda ushirikiano ikiwa na maana mke na mme mnaweka budget yenu na plan mlizo nazo. Na budget inakuwa na mapato na matumizi yenu. Ukikuta mke anasema kipato chake ni chake na cha mme ni chake mara nyingi haya masuala ya budget shirikishi hayapo. Mtakuwa mnabudget nini wakati budget member mmoja hatowi ushirikiano wa kuwezesha budget? Mara nyingi katika situation kama hii ambayo mme anakuwa ni kila kitu hata chumvi na nyanya na mke anacho kipato kunakuwa na matatizo hata kwenye projects wanazofanya.Nikiwa na maana unaweza kukuta baba anafanya mambo bila ushirikishwaji mzuri wa mke. Itaonekana pia kuwa hiki ni cha baba na hiki ni cha mama, chanzo cha ubinafsi katika ndoa.

  Kushirikiana naona ni vema hata kama kipato cha mke ni kidogo ukilinganisha na cha mme.Kwa kuzingatia vipato vyenu mtajuwa kipi kiende wapi na kipi kibaki wapi. Na hii pia inasaidia kuwaweka karibu kama mambo yenu mnayafanya kwa pamoja.
   
 12. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Akhsante mkuu!
   
 13. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mwanaume anaweza kuwa na mashati manne na suruali nne na akaonekana smart kila siku .mwanamke sasa nguo mpya kila kukicha maurembo, ndio maana tunajikuta tunatumia vipesa vyetu kwa mambo kama hayo, ila kama unamshahara mkubwa si vibaya kusaidiana na mwenzako
   
 14. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hilo nalo neno asante Michelle.
   
Loading...