Majizzo ni Ruge aliyebaki duniani

sangujoseph

Senior Member
Nov 30, 2015
164
183
By Sangu Joseph
.
Duuh kwanza nianze kwa kushangaa, kama ambavyo wengi tulishangazwa kuona taarifa ya kutua kwa BDozen, #DozenAmetua kwa Waswahili @efmtanzania na @tvetanzania hii taarifa kubwa kwa Wapenzi wa Media na Tasnia ya Burudani Bongo.

Kabla ya kwenda mbali uwezo wa Bdozen hakuna ambaye haufahamu, kwanza anaheshima kubwa sana Kwa wasanii imefika hatua kuna wasanii hawamuiti jina lake la Dozeni wanamuongezea Brother Dozeni.

Kuathirika au kutoathirika kwa Clouds Media Group hiyo tuttabonga siku nyingine , leo tumjadili Boss Francis @majizzo
Unaweza ukajiuliza kwanini huyu jamaa anasajili Giants kwenye Kituo chake, kwani haoni Watangazaji wachanga mpaka anasajili Giants, naikumbuka kauli moja ya Majizzo wakati wa kumuendeshea Mchango Boss Ruge #JasiriMuongozaNjia alisema kuumwa kwa Ruge game kwake ilikosa ushindani Kwa sababu Ruge alikua akimpa changamoto sana, nadhani Kwa sababu alishawahi kukiri Ruge ndiyo alisababisha na yeye kufungua Kituo cha Radio hivyo alikua akipita kwenye miguu yake.

Nadhani kwa sasa naweza kusema game ni kama nyepesi kwake, kwa sababu anaweza kumng'oa Mtangazaji yeyote wa Media yeyote amtakaye, hatua ambazo zilikua za #JasiriMuongozaNjia.
.
Game imekua ya kawaida kwake ndiyo maana unaona kaleta #HomaTVE na atawaleta Waimba Kwaya kwenye kipindi cha Vijana na Vijana wakatamani waimba Kwaya warudi tena.
.
Ili media iwe na impact kwanza lazima uwe na watu wasikilizaji, pili uifanye iwe media ambayo hata Mtangazaji /Mwandishi anayechipukia ahisi hicho Kituo ni sehemu ya Ndoto yake anayopaswa kuifikia, na anawezaje kuhisi hilo kwa kuvutiwa na Watangazaji wakubwa kwenye hicho kituo, Activities za Kituo, Flow ya upatikanaji wa Watu maarufu kwenye hicho kituo, ambayo kwa sasa unaiona Majizzo anaipeleka huko EFM, itawafanya Watangazaji na Waandishi Chipukizi waseme Efm ni moja ya vituo ambavyo unaweza kufikia Ndoto zako.

Nicheki Instagram : Twitter : FB Sangu Joseph
0712861292
.
.
#KijanaMzalendo #IloveTZ
 
Xxl anaachiwa nani sasa au mina ally ndo akiongoze make adam kile kichwa kingine
 
Unaizungumzia efm ambayo mwanzoni ilikuwa inasikika Dar pekee na baadaye kuanza kusikika baadhi ya mikoa kisha kwa Sasa haisikiki tena.
 
Wewe jamaa unamaandiko ya ovyo Sana sijui unawaza kwa kutumia Nini nje ya akili?
 
Afanye mpango amrudishe na kicheko alafu ampachike kwenye kipindi chake kile cha mwanzo cha singeli (genge)huyu bwana alifanya e.fm ikapaa gafla ruge alipoona hivyo akamchomoa hapo kaenda kumficha leo hii hasikiki kauwa na nyota yake kabisa
 
Bado sama kumfananisha na Ruge unamkosea sana marehemu wemjinga usajili wa Dozen unazani ndio utaweza kushindana na Clouds 🤔 wanawanatakiwa wapambane sana kuwafikia Clouds.
 
Afanye mpango amrudishe na kicheko alafu ampachike kwenye kipindi chake kile cha mwanzo cha singeli (genge)huyu bwana alifanya e.fm ikapaa gafla ruge alipoona hivyo akamchomoa hapo kaenda kumficha leo hii hasikiki kauwa na nyota yake kabisa
Jamaa yuko kwenye kamati ya fiesta
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom