Majini ndani ya mwili wako

Majimoto

Senior Member
Nov 22, 2007
138
146
Wachawi wanaofunga majini mara nyingi hukosa mahali pazuri pa kuhifadhi majini yao; hivyo hutumia miili ya binadamu kama zizi la kufugia majini yao; utajuaje kama ndugu yako, mke wako au mume wako amefanywa zizi la kufugia majini.

Ziko tabia zinajitokeza kwa mtu aliyefanywa zizi la majini; mtu wa namna hiyo akiwa amelala usiku utamsikia akitafuna tafuna kitu ambacho huwezi ukakiona kwa macho ya kawaida; na tabia hii inakuwa ni jambo linalojirudia rudia kila siku; kama ilivyo kawaida kwa wafungaji wowote wa mifugo kama mbuzi, ng'ombe, kuku nk. ni lazima ulishe wanyama wako na uwape maji kila siku; ni kawaida hiyo hiyo wanayotumia wachawi kulisha majini yao chakula kupitia midomo ya watu waliogeuzwa mazizi; chakula wanacholishwa ni nyama za watu waliokufa pamoja na damu za watu.

Watu waliofanywa mazizi baada wa wachawi kuondoa majini yao mwilini mwa mtu, mtu huyo anapata ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa mwili wake, fanya utafiti utagundua idadi kubwa wa watu walioadhirika na ugonjwa kwa kupooza walikuwa wanatafuna tafuna vitu usiku. Ni sawasawa na ukinunua maji kwenye mfuko, ukimaliza kuyanywa yale maji ule mfuko utabaki umesinyaa, hali hiyo hiyo ndiyo inayowapata watu waliofanywa mazizi pindi wachawi wanapo ondoa majini mwilini mwao.
 
Watu waliofanywa mazizi ya kufugia majini, miili yao inakuwa mizito sana, wenyewe wanajiona kama wamebebeshwa kitu kizito kichwani na huwa hawezi kusimama wima kwa muda mrefu ni lazima atafute mahali akae chini, pia wanapata taabu sana kama wanapita eneo la kupanda ngazi za nyumba au kupanda mabasi makubwa.

Wachawi wakiona mazingara ya zizi lao liko vizuri wanaongeza majini hadi kufikia idadi ya majini 1000+

Mwili wa mtu aliyegeuzwa zizi unapoanza kuchoka husikia maumivu makali sehemu mbalimbali za mwili wake, na anapoenda kwenye matibabu, vipimo vyote vile atakavyofanyiwa hakuna ugonjwa utakaoonekana, sababu bado hakuna maabara inayoweza kuona majini.
 
Duuh! Kwa hiyo mtu afanyeje baada ya kugundua kuwa yeye ni zizi yan anatafuna usiku,akipanda ngazi anachoka,anajihisi mzito,hawezi kusimama kwa muda mrefu etc, tiba yake nini ili hayo majini yaondoke na mtu asipooze??
 
Hizi elimu zenye lengo la kutia hofu watu sijui chanzo chake ni wapi, na zinavyopendwa sasa.
 
Ni ngumu kumeza sababu: Kuna imani kuwa mtu anaekula nguruwe hapati majini, je hakuna walioopararaizi wanakula nguruwe, pia hapendi bangi hakuna waliopata maradhi haya wanaovuta bangi.
Tabia hii ya kutavuna tavuna ipo kwa watoto wadogo sio watu wazima, je inamaana hao wachawi hutumia sana watoto?
 
Kuna makala moja niliisoma inaonyesha majini wanaishi katika Majumba, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa, kwa hiyo hii ya kuishi kwenye miili ya mtu basi mfugaji anakuwa amelituma kwa makusudi maalum ya kumtesa huyo mtu na ndo maana mwishowe huwaachia huo ugonjwa mfano wa kupooza
 
Bado hakuna tiba ya kuondoa majini ndani ya mwili wa mtu, kwa tiba za waganga wa kienyeji au tiba za hospitali. Tiba ya uhakika au kiboko ya majini kwa asilimia zote ni kwa njia ya YESU Kristo pekee.
Ila kuna ma-sheikh nao huwa wanatoa watu majini, je wao wanatumia njia gani?
 
Naketi kitako kuongeza maarifa mengine kuntu...maarifa ya bure yanayotolewa kwa upendo na unyenyekevu mkuu
Ukiendelea kuongeza elimu juu ya haya makitu utakuwa zaidi ya chizi, kwa uelewa ulio nao acha kabisa usije geuka jini nawe.
 
Bado hakuna tiba ya kuondoa majini ndani ya mwili wa mtu, kwa tiba za waganga wa kienyeji au tiba za hospitali. Tiba ya uhakika au kiboko ya majini kwa asilimia zote ni kwa njia ya YESU Kristo pekee.
Swali: Nimeona hasa akina mama na akina Dada wahudhuriaji wazuri wa kanisani, na bado wanatolewa mapepo kila mara, tatizo nini ikiwa wapo sehemu ambapo pepo hafanyika kazi.
 
Hahhahahaaaa mwasu hii kitu ni kama cocaine ujue...seriously najizuia mno lakini Nashindwa
Ridhika na elimu uliyonayo ukiendelea kuongeza weweza hamia baharini maana nchi kavu yote utaona karaha maana utakuta na mauzauza kila siku ushindwe kuendesha maisha.
 
Ridhika na elimu uliyonayo ukiendelea kuongeza weweza hamia baharini maana nchi kavu yote utaona karaha maana utakuta na mauzauza kila siku ushindwe kuendesha maisha.
Noted n appreciated...am humbled
 
kuna mtu namjua ana tabia hiyo, yaani akilala anatafuna hadi anasaga meno kabisa, au sio hiyo?
 
Back
Top Bottom