Majini & Mapepo 👻🤔

Majini & Mapepo 👻🤔

umeshachunguza kila kitu kwenye dini zote ukaona hakuna majibu au ume conlude kwa mistari michache tu uliyoona
Najua nina chokisema nimesoma mdrassa na kuhifadhi Qur'an nimesoma bible pia na ku spend kwa muda kanisani
 
Sijasema naogopa ila nataka kuona mawazo ya mtu kwenye Wino sio mawazo ya AI hivyo tu
Mimi pia nataka tujadiliane kwa hoja na mawazo yetu wenyewe. Lengo langu si kushindana, bali kuelewana na kuchunguza maswali haya kwa kina. Ndiyo maana niko tayari kusikiliza hoja zako na kutoa mtazamo wangu."

Shukran sana
karibu kwenye mjadala mkuu

Kujua jambo kabla halijatokea si sawa na kulisababisha, nakubali

Lakini huu mfano wa rafiki uliouweka hauendani na hoja hii

Kumbuka Mungu anajinasibu kuwa yeye ni muumbaji wa kila kitu
Nadhani nikisema muumbaji wa kila kitu unaelewa ninachomaanisha, si ndiyo mkuu?

Kwa hiyo, si kwamba Mungu alijua tu kila kitu kitakachotokea kama ulivyosema kwenye mfano wa rafiki, bali yeye ndiye muumbaji wa hayo yote
kwa mantiki hiyo angeweza kuzuia

Nakubaliana kwamba Mungu si mtazamaji tu, bali ndiye Muumbaji wa kila kitu. Hata hivyo, kuumba kiumbe mwenye uwezo wa kuchagua si lazima kumaanishe kwamba Mungu ndiye anayemchagulia kila kitendo.

Lakini hoja yako ya msingi bado ipo: Ikiwa Mungu alijua viumbe wake wataasi na alikuwa na uwezo wa kuzuia hilo, kwa nini aliruhusu litokee? Hilo ndilo swali linalohitaji majibu. Nikipata wasaa tutalijadili kwa urefu


Yes, sasa swali linakuja, kwa nini Mungu aumbe viumbe wenye uwezo wa kutenda maovu?

Kwa nini asingewaumba viumbe ambao hawana kabisa huo udhaifu wa kutenda maovu?

Kumbuka Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu
Kwanini mwanadamu awajibike kwa udhaifu alioumbwa nao?

Lakini kama Mungu angeumba viumbe wasioweza kutenda uovu kabisa, kusingekuwa na uchaguzi wa kimaadili. Katika Uislamu, mwanadamu hawajibiki kwa kuwa na udhaifu, bali kwa maamuzi na matendo anayochagua kufanya ndani ya uwezo aliopewa.

Shetani mwenyewe anasema hakuwa na mamlaka ya kuwalazimisha wanadamu kufanya maovu, bali yeye anachofanya ni kuwaita na wao wanaitika

Kwa nini Mungu amuache Shetani aendelee kuishi huku akijua wazi kwamba ataendelea kuwarubuni wanadamu na kuwafanya waanguke dhambini?

Cha kushangaza zaidi Mungu aliwaangamiza watu wa Sodoma na Gomora, lakini akamwacha Shetani, ambaye ndiye chanzo I mean mdanganyifu


Katika Uislamu, Shetani mwenyewe aliomba apewe muda hadi Siku ya Kiyama, na Mungu akampa katika (Qur'an 7:14–15). Hiyo haimaanishi Mungu anakubaliana na matendo yake, bali hukumu yake imeahirishwa. Swali ni je, kuahirisha hukumu kunamaanisha kukosa haki?

Hapa hata siongei sana Shetani alipaswa kuuwa mapema kabisa sioni mantiki ya kumuacha aishi

Sijawahi kuelewa yaani

Nakuelewa mkuu. Lakini katika Uislamu, Mungu alimpa Shetani muda aliouomba. Swali la msingi ni kwa nini Mungu aliruhusu hilo huku akijua madhara ambayo Shetani angesababisha kwa wanadamu.


Kwa nini mwanadamu aadhibiwe kwa makosa yake wakati yeye ndiye aliyeumbwa akiwa na matamanio, wivu na madhaifu mengine kibao?

Kosa lake hasa liko wapi ikiwa hakujiumba mwenyewe wala hakuchagua kuwa na hizo tabia na madhaifu?

Kwa nini Mungu asingemuumba mwanadamu akiwa mkamilifu, asiye na matamanio yanayovuka mipaka
wivu na mielekeo ya kutenda maovu?

Yaani Why Why nashindwa kuelewa


Katika Uislamu, kuwa na matamanio na udhaifu si dhambi. Mwanadamu anawajibika kwa namna anavyotumia uwezo wake wa kuchagua. Mungu hamwadhibu mtu kwa jambo lililo nje ya uwezo wake.

Kulikua na haja gani ya kuumba vitu complicated mkuu?
Na uwezekano wa kuumba vitu straight upo?

Mungu alikuwa na uwezo wa kuumba viumbe wasio na udhaifu. Lakini alichagua kuumba viumbe wenye hiari. Swali ni kwa nini alichagua mfumo huu? Hapo ndipo tunapojadili hekima ya Mungu.


Yaani kama haya majanga ndio kabisaaa nashangazwa na namna Mungu anaacha dunia iwe uwanja wa fujo na mabalaa je anafurahia

Mungu hafurahii mateso wala uovu. Lakini swali ni kwa nini anaruhusu majanga wakati ana uwezo wa kuyazuia? Hapo ndipo tunapojadili hekima ya Mungu.


Hakuna majini hakuna mapepo
Ukitaka unaweza kuvitengeneza kwenye akili yako
Kama una amini vipo weka ushahidi

Mkuu, kutokuona kitu hakumaanishi hakipo. Katika Uislamu, majini ni viumbe wa ghaibu, na ushahidi wake ni Qur'an. Swali ni je, unakubali kwamba si kila kitu kilichopo lazima kionekane kwa macho?


Hizi dini nazo ni za wapiga dili tu mie hata siziamini nimetumia bible kukujibu kwa sababu mada inahusu hivyo vitabu vitakatifu kama msemavyo

Na pia ujue Qur'an ni copy end paste ya bibilia agano la kale

Nakuheshimu mkuu, lakini kufanana kwa simulizi za Qur'an na Biblia hakuthibitishi kwamba Qur'an imenakili Biblia. Kuna pia tofauti kubwa kati ya vitabu hivyo.


Sababu kama zipo ziainishe nipo tayari kujifunza mkuu

Karibu mkuu. Kwa mfano, kuna tofauti kuhusu Yesu, kusulubiwa kwake na nafasi yake kama nabii au Mungu. Tunaweza kuzichambua moja baada ya nyingine kwa kutumia Qur'an na Biblia.


Ingekua bora tungeumbwa kwa ukamilifu Yes kuliko hizi songombingu

Nakuelewa mkuu. Lakini katika Uislamu, dunia si mahali pa ukamilifu bali ni sehemu ya mtihani. Ukamilifu wa kweli unahusishwa na maisha ya Akhera.


Kwako Jagina

Alooo nimetumia muda kuandika nandika nafuta naandika nafuta 🙌🏼🙌🏼🙌🏼
Nimetumia hiyo style yako haraka haraka labda utaridhika
 
Back
Top Bottom