Majina ya wagombea Ubunge jimbo la Kinondoni yatoka, Mgombea wa UKAWA akatwa

Ukawa mnatukatisha tamaa namna hii jimbo langu kinondoni nilivyokamia kumuondoa Azan Daah
Alafu hivi wagombea wa ccm hawakosei kwenye hizi form ni wapinzani tu jmn
 
kwa hili viongozi wa cuf ni lazima muwajibike. kwa nini huu uzembe unatokea? wanasheria wa ukawa kateni rufaa. hatuwezi kukubali upuuzi huu kamwe...
 
Kwani UKAWA si na CDM wapo. Tena Makao makui yao pande hizo, mlikosa hata afisa mmoja wa kuhakikisha mambo yanaenda sawa? Ubunge hivi, Udiwani itakuwaje?
 
Hawa wagombea wa CUF wameamua kuhujumu UKAWA kwa maelekezo ya Lipumba na mabwana zake Wa ccm
 
Lazima huyo mgombea atupe maelezo ya kutosha
pia kuna mihuri ya mahakama hapo, kwanini tume iruhusu vitu vidogo kama hivi vifanyike ili kuwaondoa watu lazima nec ifanye marekebisho kanuni zake, haiwezekani nini maana ya uchaguzi sasa sinibora uchaguzi uhairishwe ili wateuliwe tu watu.
 
Kitu ambacho kimenifurahisha kuona mgombea wa ACT-Wazalendo naye katupwa nje kwa mujibu wa pro Chadema/Ukawa walituaminisha kuwa ACT-Wazalendo ni CCM
 
kama ni pesa watahonga hadi basi, ila kura zetu zitaenda kwenye chama kingine ila siyo ccm

Huo ndio ukweli kama wamemuengua mgombea wa ukawa basi tumchague mgombea wa chama kingine kuliko ccm
 
eti jibu ni hapana!! watu smart hua wanawajua viongozi wao kwa sura mkuu,,, sasa mgombea ubunge mzima kutomjua hakimu we haikuumizi kichwa hata kidogo au ndo zile tabia zetu za kila siku za kuwapa lawama wengine kwa kila ujinga tunaoufanya? ni kweli huelewi mkuu ama unajitia tu hamnazo?
Kwani hapo suala ni kumjua kiongozi kwa sura? Kwani hapo alitakiwa kumjua hakimu kwa sura? Mimi sijaona mahali ambapo wamesema kwamba amewekewa pingamizi kwa vile alishindwa kumjua hakimu kwa sura!! Suala hapo ni kutoandikwa jina la hakimu ingawa maelezo yanasema imetiwa saini mbele yangu: Jina la Hakimu........................Sasa hapo kumjua kwa sura imetoka wapi? Huyu mgombea naye katia aibu kwa kweli unashindwa kuona vitu kama hivyo? Wewe unabebelea li-fomu ambalo halina jina!! Shame on him! Na huyo Mkurugenzi naye kasaidia sana hilo jimbo lichukuliwe bila kupingwa, kwa nini alipoona hizo kasoro hakumweleza huyo mgombea arudishe hiyo fomu ili ikaandikwe jina? Mbona tume wenyewe walimruhusu Rungwe kurudia picha alizokuwa amezisahau nyumbani? Nafikri kwa wakurugenzi wetu wao wangepokea tu hizo fomu ili iwe rahisi kwa maccm kuweka pingamizi. Hapa NEC inatakiwa itumie tu akili ya kibinadamu kumrudisha huyo jamaa kwenye kinyang'anyiro!!

UKAWA ikiingia madarakani wakurugenzi wote wafanyiwe vetting ili tujiridhishe kabisa kwamba hatuna ma-DED wenye harufu ya ccm!!
 
Kama ni mtu makini,kwann afanye makosa ya kijinga ktk masuala muhimu,hii inaonesha hata angepata uongozi,asingeweza kuwa serious,msitee uzembe...

Afadhali tuwachague PPP kuliko kuipa ccm kura,wamejichosha
 
UKAWA kama wana wanasheria wazuri, huyo mgombea wa UKAWA atarudishwa na NEC.

Kwani muhuri unaonekana ni wa HAKIMU kama sheria inavyosema.

Kama aliyeugonga sio HAKIMU mwenyewe ni karani, that is none of mgombea wa UKAWA business. Mgombea ana deal na ofisi sio individual person!

Huyo mgombea atarudishwa kama Wenje wa Nyamagana na atamshinda Idd Azan, kwani pamoja na kupigiwa kura za UKAWA pi atapigiwa kura za sympathy kwamba alitaka kuonewa

Mark my words.
 
mbona hausemi bungeni napo kuwepo na kitengo cha kusaidia wabunge kusoma miswada?hv mbunge mzima anashndwa kuhoj kama huyu ninayeruhusu anisainie ni hakimu ama sio hakimu mpaka kitengo cha usaidiz kiwepo kwel??hv viongoz wake walikua wap kuliona hili kabla hajarudisha,inaonesha viongoz waukawa hawakukagua na kujiridhsha ujazwaj wa fomu hzo!
Huu mjadala ni wa watu wenye ubongo mpana. Sidhani kama unaweza kuona mantiki kwenye hoja yake
 
Hizi sheria za NEC za kuweka mapingamizi ni kubaka demokrasia ni kiasi cha kuelekezana jinsi ya kijaza fomu, NEC walitakiwa kuwa na kitengo cha kusaidia kujaza fomu kama vile uhamiaji

Hakika,naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom