majina ya vijiji vya vya hanang'

mkuu mulbadaw ulikatiza miaka gani?

nilipoa hapo kwenye miaka ya 91 mpaka 93 nilikua naenda nakaa kama wiki nakurudi arusha ndio palikua home,jamaa flani walikua wahasibu hapo,walikua wanaitwa james kashaga,kamote,na mwingine abdalah alikua manager wa timu ya mulbadow ndio walikua wanapeleka huko,mimi nilikua dogo nipf standard seven meru primary arusha.asante ndugu.
 
basi ukitoka pale karatu unafika gongali unafika ayabut unaingia bassodawish unatermkia barai. Toka barai unaenda endabsh then ukatiza ngaidadu mpaka kansay unafika barakta. Toka hapo unaenda mbele mpaka gwandumehhi unavuka kale kamto hahay unaingia daudi unaendelea mpaka bargish antsi unaingia mbulu pale kuna wakwe zangu wanaishi endagikot na wajomba zake mke wangu wanaishi ay mami. Shemejii upo!
hapo endabash kwa bibi yangu,umenigusa kweli,asante shemeji ila majina zaidi yameniishi.thanks alot
 
Oh my dear!nimekumbuka mengi jamani!miez miwili tu imepita tangu nitoke huko,nimefanya kazi hosptali ya wilaya,Tumain.Jamani WABARBAIG,JAMAn WAIRAQ!!!OHOO KATESH MISS U MUCH!BUT U WIIL LIVE FOR EVER IN MY LIFE!NATUMAI NTAOA MSICHANA NILIYEMPATA KATESH!
 
hapo katesh nilishafika....pana upepo na baridi kali sana...

Mzee alihamishiwa hapo miaka hiyo lakini tulikaa miezi 6 baridi lilimshinda maza,duh nalikumbuka kanisa katoliki likiwa mlimani..afu na sauti za fisi usiku...
 
Mh!inamaana wairaqw walirithi majina ya wabarbeig?mbona maeneo yote yaliyotajwa wanaishi wao?naomben ufafanuzi
 
Manyara nimekumbuka mbali wakati nafanya kazi kwenye mradi wa Maji wa kanisa Katoliki la Mbulu,tunaenda Hydom,huko Hanang kupitia Dareda,kule tulikuwa tunalala Katesh,Qurus,uuh majina hayo siwezi kuyataja sana ila Qandach kama unaelekea Hydom Hospital,Mkoa wa Manyara umejaaliwa na ardhi nzuri yenye rutuba,nimewakumbuka sana na salamu zao Baba Lawai/yi.
Pia kufanya mkutano wa hadahara lazima niwe na mkalimani hasa kule kwa Waman'gati
 
Basi ukitoka pale Karatu unafika Gongali unafika AYABUT unaingia Bassodawish unatermkia Barai. Toka Barai unaenda ENDABSH then ukatiza Ngaidadu mpaka Kansay unafika BARAKTA. Toka hapo unaenda mbele mpaka Gwandumehhi unavuka kale kamto Hahay unaingia DAUDI unaendelea mpaka Bargish Antsi unaingia MBULU pale kuna wakwe zangu wanaishi ENDAGIKOT na wajomba zake mke wangu wanaishi AY MAMI. Shemejii upo!
majina haya yananikumbusha Abyssinia na Somaliland
 
Mi nilikuwa kwa kampeni mwaka juzi hanang nilizzunguka kata zote 25 paka zile mpya za simbay na gisambalang kule mppakani na kondoa,getanuwas...dah acha tu thanx kaka!
 
Mh!inamaana wairaqw walirithi majina ya wabarbeig?mbona maeneo yote yaliyotajwa wanaishi wao?naomben ufafanuzi

Kweli. Historia inasema Wairaqw walivamia maeneo ambayo yalikaliwa na Wabarbaig. Na kwavile Wabarbaig ni wafugaji kiasili,ilikua sio rahisi kwao kuishi pamoja na Wairaqw,ambao wenyewe kiasili ni wakulima na wafugaji.

Hivyo maeneo mengi ya Manyara Wairaqw walivamia Wabarbaig na kufanya Wabarbaig sasa kuwepo katika maeneo machache sana ya Manyara,haswa Katesh na Hanang' kidogo.
 
Back
Top Bottom