Majina ya michepuko kwenye simu

Majina ya michepuko kwenye simu

BABA E's

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2012
Posts
354
Reaction score
136
Dunia hii watu wanaubunifu sana. Kuna jamaa ni engineer kasave mchepuko wake kwenye simu kama engineer fulani, kwahiyo siku zote mchepuko ukipiga simu hata wife akiona anamwambia 'engineer fulani anakupigia' na Mume anajibu 'Mwache tu huyo msumbufu sana nitampigia baadae' basi ndio maisha yakawa hivyo.

Sasa kuna siku jamaa kasahau simu nyumbani na wife alishindwa kumjulisha mumewe kwamba kasahau simu nyumbani akawa anasubiri labda mumewe ndio atampigia. Bahati mbaya mchepuko nao ukapiga simu kama kawaida kwenye simu

Jina limetokeza ni engineer fulani, wife hana jinsi ikabidi apokee ili amjulishe kwamba mumewe kasahau simu nyumbani, ile kupokea na mchepuko nao ndio ukaanza kuongea kimahaba.Dah kilichofuata nadhani kinaeleweka,ndio hivyo za mwizi ni arobaini.

Tuache michepuko Jamani
 
Pole yake...
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1426673104.112724.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1426673104.112724.jpg
    40.7 KB · Views: 430
Back
Top Bottom