Nyingi hazina mvuto,weekend niliona movie moja kipande tu katika chanel ya sinema zetu,madada watatu wamekodi taxi umbali kidogo dreva kaenda kichakani kuchimba dawa,akiwa huko kakutana na zimwi likamuuwa,wale wadada kuona kachelewa mmoja kamfuata na kumkuta amekufa huku kajaa midamu,kichekesho ni reaction ya yule mdada ,hakushtuka inavyotakiwa,na anajifanya kupiga kelele na kuruka ruka kama mtoto wa chekechea,hakuna uhalisia wowote,analia huku mashavu yanatabasamu,kwa kweli nilichukia na kushtukia nahamia channel nyingine kwa hasira.Kuna umuhimu wasanii wetu wapite bagamoyo,sio awa wetu wengi ni division 5,wengine classless wanaona hiyo ni ajira isiyohitaji elimu.Kama sikosei Nigeria actors wengi ni graduates waliosomea fani ya uigizaji na ndio sababu movies zao zina mvuto na uhalisia.